Marekani kutoa Dola Mil 800 kuchangia miradi ya maendeleo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Taarifa ya Ikulu inasema kuwa balozi wa Marekani amefanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa serikali ya Washngtone itataoa Dola Mil 800 kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo, pia huu ni uthibitisho wa kuwa baada ya kusitishwa kwa fedha za MCC awamu ya pili hakujaathili mahusiano baina ya mataifa haya mawili.


==========

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Marekani itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo. "Tumezungumza mambo kadhaa, na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu Ia misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani llll MCC.

"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafinikiwa" Amesema Balozi Mark Childress muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Rais Magufuli. Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania .

"Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410, anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na Marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za HAPA KAZI TU zinaendelea" amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo viongozi hao wamezungumzia kuendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususani katika maendeleo.

Pamoja na kuzungumzia miradi ya ushirikiano inayotekelezwa kati Tanzania na Ubelgiji katika mkoa wa Kigoma, viongozi hao pia wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara na uwekezaji ambapo Mhe. Didier Reynders ameahidi kushawishi kampuni nyingi za Ubelgiji kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameagana na Balozi wa ltalia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitatu.
Balozi Luigi Scotto amesema katika kipindi chake amewezesha kuongezeka kwa biashara kati ya Italy na Tanzania kwa asilimia 35 na ameielezea Tanzania kuwa ni nchi nzuri aliyoipenda na kwamba ataendelea kutangaza fursa zilizopo Tanzania huko Italia na kwingineko.

Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini kitabu cha maombelezo katika Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Nchi za Kiarabu ya Saharawi iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Mohamed Abdelaziz aliyefariki dunia Jumanne iliyopita tarehe 31 Mei, 2016.

Rais Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Saharawi hapa nchini Mhe. Brahim Salem Buseif amesema Marehemu Mohamed Abdelaziz ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Polisalio Front, atakumbwa kwa juhudi zake za kupigania ukombozi na uhuru wa Saharawi.

"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania napenda kutoa salamu zangu za pole kwa Serikali na wananchi wa Saharawi kwa kumpoteza kiongozi umbaye ulijitoa kwa ajili ya kupigania ukombozi na uhuru wa Jamhuri ya Saharawi.
"Namuombea kwa mwenyezi Mungu, aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina" Amesema Dkt. Magufuli katika salamu hizo.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam
06 Juni, 2016



CkRQhc0XIAAnfid.jpg
CkRQhfDWsAAT-em.jpg
 
sisi huku tunataka bunge live, pili hatumtaki Tulia, tatu dr. nadalichako ni jipu na nne div o na 4 waruhusiwe kuchukua degree msiwanyanyase serikali. hayo ndo mambo ya msingi sisi ukawa tutayasimamia kufa na kupona mpaka kieleweke. kwikwikwi....
 
Hatuhitaji misaada yao....kauli hizi zilisemwa na baadhi ya Waheshimiwa ......na wakaongeza kusema makusanyo ya kila mwezi yanatosha.
utakuwa ulisimuliwa ila muhongo alisema kunyimwa misaada hakutazuia kasi ya umeme vijijini
 
Safiiiiiii... safiiiiiii... JPM.. U.S.A wako very straight, ukifanya vizuri kama Rais wetu JPM, wanatoa millions of dollars to support development in various sectors...!!

Hii iko vizuri sana sana.. Serikali sasa itakuwa na afya sana sana...!! Excellent..✔✔✔
 
Niliposoma soma taarifa rasmi kutoka Ikulu nikajiuliza yafuatayo yanayo andikwa kuhusu JPM:
  • "Kiingereza cha Rais JPM"
  • "Serikali ya Udikteta"
  • "Rais hajasafiri kwenda Ulaya"
  • "Uvunjaji wa haki za binadamu"
  • "Serikali ya kukurupuka"
  • "Tanzania kutengwa na jumuhia za kimataifa"
  • etc.
Labda somehow hiyo taarifa ni cracking joke. Vingenevyo, nitashangaa kama kuna mdau atakuja tena hapa JF na hoja on any of the above.

 
Marekan baada ya kuona jamaa hatanii wameamua kulegeza mikanda.
Ile kauli ya mataifa makubwa yaige mfano toka china naona umewakuna.
 
" No Country Is an Island'' either U.S.A or else where we are in interdependent world.
Kwa hiyo iwe U.S.A, EU, Asia tunahitajiana kwa maendeleo yetu sote. Kwa hiyo tusishangae kuona U.S.A wanatoa hela nyingi na ujue pia wanachanganyikiwa namna ya kuwa karibu na Tz endapo tutakaza uzi wa kukataa kuomba /kutegemea misaada. Hapo wanakumbana na changamoto ya kutojua kuwa sasa hivi Tz tunapata wapi fedha kiasi cha kuwatilia shaka na misaada uchwala yao [uchalwa namanisha mashariti yao] Maana ktk hilo, hata ukiwa na rafiki alikuwa anakutembelea mara kwa mara ila ghafula akapunguza safari zake kwako , ni lazima utajiuliza nini kimemsibu ama kapata rafiki mwingine zaidi yako?

Lakini, ktk hili acha picha liendeleee maana misaada ya masimango bora ikome, wakitupatia kisha wakatusimanga TUNA WATIMULIA MBALI!!

Na pia uelewa China kakubali kushiriki ujenzi wa makitaba UDSM kwa asilimia mia , unadhani U.S.A akae kimya na huku anajua vyema kuwa chuo kikuu ni think thank ya Taifa tena chuo kikuu kama UDSM?

Wazungu, Wataisoma namba kwa TZ.

Haa haaa safi sana!!!
 
Back
Top Bottom