Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,630
- 25,586
Kitengo cha serikali ya Marekani maarufu kama "State Department" kimetangaza kusitishwa kwa utoaji wa viza za kuingia nchini Marekani kwa nchi zipatazo 75 nyingi zikiwa ni kutoka barani Afrika Tanzania ikiwemo.
Sababu ilotolewa na kitengo hicho imesema raia kutoka katika nchi hizo wafikapo nchini Marekani baada ya kupewa viza hizo huanza mara moja mchakato wa kusaka msaada kutoka kwa raia wa Marekani (wakimaanisha kuomba ukimbizi na sababu zingine) ili wasirudi huko walikotoka.
Maelekezo kutoka kwenye idara hiyo yalotolewa jana Jumatano yametaka zoezi zima la kutoa visa katika balozi zilizopo katika nchi hizo lisimamishwe hatua ikiwa ni sambamba na zoezi linoendelea la kuhuisha maombi ya viza kwa raia wa nchi hizo linoendelea tangia mwezi November mwaka jana.
Kusimamishwa kwa utoaji wa viza huko kwapelekea kuongeza ugumu zaidi wa upatikanaji wa viza hizo kwa raia hao ambao wengi ni wa kutoka nchi za Afrika na zile za Asia.
Usitishaji huo hautawalenga waombaji viza waso wahamiaji kama watalii, wafanyabiashara bali wale wahamiaji ambao wana malengo ya kudumu, waendana na sera ya utawala wa raisi Donald Trump inolenga kulinda mfumo mzima wa utoaji viza na uhamiaji nchini humo ambao wafikiriwa kuwa umechezewa kwa miongo kadha.
Halikadhalika sera hiyo yalenga kuwazuia raia wa kigeni mara baada ya kuingia nchini humo kutokuwa na haki ya kupata huduma z bure kama vile bima, makazi na malazi pamoja na baadhi ya huduma za kiafya khasa hali ya kuwa na usonji.
Ujumbe mfupi au MEMO ilotolewa na State Department kwenda kwenye balozi za Marekani katika nchi hizo umeelekeza balozi hizo kutotoa viza zozote zile na kutoidhinisha viza katika muda usojulikana wakati zoezi la tathmini ya ufumo wa utoaji viza hizo ukiendelea na ujumbe huo haukutoa maelezo zaidi.
Miongoni mwa nchi hizo zimo nchi za Russia, Rwanda, Tanzania, Uganda, Ghana, Sudan, Nigeria na Somalia (Sio Somaliland).
Kuwekwa kwa Russia katika orodha hiyo ni kutokana na mgogoro kati yake na Ukraine, Uganda kutokana na harakati za kutaka kuvuruga uchaguzi, Rwanda kutokana na kushindwa kufuata makubaliano yalofikiwa nchini Marekani kati yake na Congo DRC.
Nchi ya Sudan pia ni kutokana na vita inoendelea nchini humo pamoja na Sudan ya Kusini, Nigeria kutokana na raia wake wengi kuhusishwa na wizi wa mitandaoni, Somalia kutokana na kuendelea kushindwa kuwadhibiti magaidi wa Al Shabab na Tanzania kutokana na kuwa na raia wengi waso na vibali halali vya kuishi nchini humo pamoja na vitendo vilotokea baada ya uchaguzi wa mwezi Octoba mwaka jana ambao imeripotiwa kuwa watu zaidi ya 10,000 waliuawa na vikosi maalum vya usalama.
Kenya, Botswana, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia na Msumbiji hazimo katika orodha hiyo.
Orodha ya nchi hizo 75 nyingi zikiwa ni kutoka Afrika na Asia Tanzania ikiwemo ni kama ifuatavyo:
Afghanistan, Albania, Algeria, Antigua and Barbuda, Armenia, Azerbaijan, Bahamas, Bangladesh, Barbados, Belarus, Belize, Bhutan, Bosnia, Brazil, Burma, Cambodia, Cameroon, Cape Verde, Colombia, Congo, Cuba, Dominica, Egypt, Eritrea, Ethiopia, Fiji, Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guatemala, Guinea, Haiti, Iran, Iraq, Ivory Coast, Jamaica, Jordan, Kazakhstan, Kosovo, Kuwait, Kyrgyzstan, Laos, Lebanon, Liberia, Libya, Macedonia, Moldova, Mongolia, Montenegro, Morocco, Nepal, Nicaragua, Nigeria, Pakistan, Republic of the Congo, Russia, Rwanda, Saint Kitts and Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, Senegal, Sierra Leone, Somalia, South Sudan, Sudan, Syria, Tanzania, Thailand, Togo, Tunisia, Uganda, Uruguay, Uzbekistan and Yemen.
Kwa uelewa zaidi kuhusu mambo haya soma hapa kutoka tovuti ya baraza la mahusiano ya kigeni ya Marekani.
www.cfr.org

A Guide to the Countries on Trump’s Travel Ban List | Council on Foreign Relations
The White House’s growing travel ban is now shutting down immigrant visa processing indefinitely for seventy-five countries, including Brazil, Iran, Russia, and Somalia, among several others.