Marekani: Asasi za kiraia zatoa wito wa kutoathiriwa huduma ya intaneti Urusi. Matumizi ya VPN yaongezeka nchini humo

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
618
1,803
Haki za Kidigitali Rais Biden Marekani Watoa Huduma za Intaneti.jpg


Asasi za kiraia zimetoa wito kwa Serikali ya Marekani chini ya Rais Biden kuwalinda watoa huduma za intaneti nchini Urusi dhidi ya vikwazo. Mashirika hayo yameonya kwamba kukwamisha ufikiaji wa mtandao kutawaathiri wenye mawazo na misimamo tofauti.

Wito huo umekuja ikiwa vikwazo dhidi ya Urusi vikichochea kuondoka kwa makampuni yanayotoa huduma za mtandao nchini humo kama vile Cogent Inc. na Lumen Technologies Inc.

Kituo cha Demokrasia na Teknolojia (Centre fo Democracy and Technology - CTD), ambacho hupokea ufadhili kutoka kwa makampuni makubwa ya teknolojia nacho ni miongoni mwa mashirika yaliotoa wito huo kwa barua. CTD inaongoza zaidi ya asasi 60 za haki za haki za kibinadamu, haki za kiraia na mashirika ya mtandao huria.

Makampuni kama vile Microsoft Corp. na NetScout Systems, Inc. ni baadhi ya yaliyosimamisha biashara zao chini Urusi kwasababu ya vikwazo.

Barua hiyo iliyosainiwa na mashirika 41 yakiwemo Freedom House, Article 19 na Committee to Protect Journalists(CPJ), imesema Ili kulinda ufikiaji wa huduma ya intaneti nchini Urusi, serikali ya Marekani inapaswa kuidhinisha rasmi huduma, programu na maunzi muhimu kwa mtandao.

"Ni suala la maslahi ya umma kuhakikisha kwamba ufikiaji wa majukwaa ya kidigitali na teknolojia ya kisasa ya mawasiliano hauathiriwi na vikwazo," inasomeka barua ya wazi iliyotumwa kwa Rais Joe Biden.

Barua hiyo pia imesema sio tu kwamba vizuizi vya huduma ya mtandao vitawaathiri zaidi wenye mawazo na misimamo tofauti naserikali, bali vitaimarisha mtandao na vyombo vya habari vya Urusi ambavyo vinavyozidi kukaguliwa vikali (censored).

Kwa sasa, Warusi wengi wanatumia VPN, aina ya programu inayotumiwa kufikia maudhui yaliyodhibitiwa.

Ongezeko la watumiaji wa VPN Urusi.jpg

Matumizi ya VPN ya Psiphon nchini Urusi yameongezeka kwa kiasi kikubwa tangu Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine
(Chanzo: Psiphon)

Psiphon, huduma ambayo imepokea ufadhili kutoka kwa serikali ya Marekani, imeona watumiaji wake wakiongezeka karibu mara sita tangu Urusi ivamie Ukraine.

"Wakati biashara nyingi zikipima mustakabali wao nchini Urusi, ni muhimu Marekani itoe mwongozo wa vikwazo kwa kampuni za teknolojia hivi karibuni "badala ya kungoja mpaka Warusi kushindwa kufikia huduma hizi muhimu", imesema barua hiyo (ambayo imeambatanishwa katika PDF hapo chini)
 

Attachments

  • Barua ya wito kwa Rais Biden kuhakikisaha watumiaji wa mitandao nchini Urusi hawaathiriwi na v...pdf
    43 KB · Views: 12
Ukiondoa makombora ya nuclear Urusi ni sawasawa na South Africa
Kwakuwa walikataa kukupumulia kisogo we unadhani urusi biashara ya ushoga inadili? Jamaa wana wanawake wazuri balaa! Sasa wewe ukapeleka mavi pambaaf.
 
Back
Top Bottom