Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Wana CCM karibu wote tunakubali na kuthamini kwa asilimia zote mchango wa Nape na Mzee Kinana kufufua CCM kipindi kile, ILA hiyo haina maana kwamba yeye Nape ni untouchable na anafanya chochote na Rais akubaliane nae tu. Busara ingekuwa Nape kama msaidizi wa Rais angeendana na mtazamo wa Rais aliyemteua kwa ku-balance mambo badala ya ku-turn against the president and his governement simply because of misunderstanding between him and the RC whom they both at same level.
 
Hoja nzuri kaka, lakini ukimsoma Nape kwa makini ni kana kwamba alikuwa anawasilisha malalamiko ya Baraza la Mawaziri, ni kama inaonyesha Mawaziri wengi hawako happy na jinsi Raisi anavyoendesha nchi, sio kwa issue ya Makonda pekee bali pia kwenye maamuzi mbalimbali, yaani Mawaziri wanakosa ile hali ya kujiamini, issue ya Makonda kuendesha zoezi la Madawa ya kulevya bila kumshirikisha Waziri mwenye dhamana ni tatizo kubwa
Nape amekuwa kama Kondoo wa kafara na sababu kubwa ni kuwa Nnape sio mwoga hivyo aliamua kupambana na Magufuli kupitia vituko vya Makonda
Shida kubwa iko kwa mawaziri wenzie, je watamuunga mkono nao wajihudhuru? Ili kuonyesha hawakubaliani na jinsi Raisi anavyoendesha nchi
We kweli kituko!unalazimisha mawazo na ndoto zako ziingie kichwani mwa Nape na wengine wenye akili kama zako.
Eti ukimtizama Nape ni kama anawakilisha malalamiko ya baraza la mawaziri!.Haupo makini mkuu
 
Sikutegemea siku moja toka kwa Nape (mzee was bao la mkono akilalamika kuitetea ccm kwa kulala polini) kumbe huwa maslahi unayatetea ili nawe uje kutetewa baadae sasa kafanyiwa ya upinzani akapanic baadae akili ikamrudia na kuanza kulainisha maneno. Udhaifu wenu wote utakuwa wazi safari hii.
 
Mleta mada umeona mbali sanaaaa....Bravo.
Hizi huwa zinaitwa " calculated moves". Mh Rais anahujumiwa dhahiri,halafu kuna watu wanatetea upuntunyu na kuhemka kwa mambo wasiyoyajua.

Kuna dots ukiweza kuziunganisha utamuelewa Mh Rais na kauli yake aliposema "CCM kuna Wasaliti".
Tatizo letu Watanzania huwa tunapenda kukurupuka na mihemko inayotuvuruga akili na kutuvua busara na UTU pale tunapoletewa jambo geni. Leo hii ikiletwa au ikitengenezwa habari ya "Nyama ya Nguruwe yakutwa ndani ya Msikiti wa Mtoro"...hiyo ndio itakuwa habari ya mjini na haya mengine yote yatasahaulika!

Tujifunze kutafakari na kufikiri nje ya boksi. Kuna mengi tunayajua na mengi hatuyajui....Mh Rais anapelekewa taarifa, sidhani Kama huwa anakurupuka kama Wanaharakati wanavyotaka kuuaminisha UMMA wa Tanzania. Muda ndio utaongea. Tuache kuishi kwa mazoea,tuishi kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni za Nchi.

UZALENDO KWANZA VYAMA VYA SIASA BAADAE.
Kabisa Mkuu. Rais wetu ana access ya information nyeti sana. Sisi kwa kukurupuka kwetu daima tunaishia kukosoa. Ingekuwa ni rahisi yeye kuziweka hadharani tungelia kweli. Mungu aendelee kumlinda tu Rais wetu. Huko mbele tutazidi kumuelewa.
 
Huyu ni kiongozi mkubwa katika nchi na amepitia katika kipindi cha presha

Kwa nini hakutulia??? au kulikuwa na ulazima wa yeye kusema kitu? what if kama Magufuli alikuwa anataka ampe nafasi ingine ya serikalini?

Nyuma ya pazia kuna nini ambacho Nape anahisi kachukiwa sana wakati kitu alichofanya is obvious ilikuwa lazima ajiuzulu yeye , bila hata kuondolewa. Hakukuwa na haja ya Kamati wakati mwisho wa matokeo ya kamati ni kupeleka report kwa Rais ambaye aliishaamua na kusema pale ubungo

Naamini rais sio malaika, wala sio kuwa Nape hana namba ya simu ya Magu kiasi ambacho wangeongea kuhusu hili swala na kupata baraka zake, kufanya jambo kama lile au kuendelea nalo likiwa linakinzana na bosi wako lina maana gani?? (tuache mihemko wengi tuna mabosi hapa)

Namna ya kudeal na lile swala ilikuwa lazima kuwe na kamati? au angebadili methodology? what was the mission behind? tuwaze nje ya box

Nape inaonekana alijua anafanya nini, na alijua outcome ya mission ilikuwa aidha

1. Rais awe kwenye wakati mgumu wa maamuzi
2. au Nape aondoke yeye

mkuu kamuwahi

ila siamini kama kwa level ya Nape hakujua kuwa kuna kitu kinaendelea..(?????) Yes unaweza kuwa hero, unaweza kuwa na malengo mema na mazuri kabisa ( kutimiza wajibu wako) ila kufanikisha kazi yako kwa ufanisi kunahitaji akili pia na approach kufikia lengo

mimi mtu wa chini niliona kabisa Nape anakinzana na rais, yeye hakuona? au yeye anafanya kazi kama msaidizi wa nani? kama sio msaidizi wa rais....naona Logic inagoma kuona kama Nape alikuwa yeye kama yeye na hana affiliation na Magufuli ambaye ni bosi wake

Imani yangu na msimamo wangu, Makonda ataondoka kupitia mahakama kwa sasa, kuvamia clouds was the best opportunity ya kumuweka kwenye majengo ya mahakama....ingemlazimisha rais kumuondoa
Thank for the golden observation.
 
Jenga mazoea ya kujisomea vitabu itakusaidia zaidi kuliko mimi nikikufafanulia.
Ebu nitajie basi vitabu vitatu vya msingi ambavyo vitanisaidia kuelewa dhana ya uzalendo kwenye context ya Tanzania.
 
Kabisa Mkuu. Rais wetu ana access ya information nyeti sana. Sisi kwa kukurupuka kwetu daima tunaishia kukosoa. Ingekuwa ni rahisi yeye kuziweka hadharani tungelia kweli. Mungu aendelee kumlinda tu Rais wetu. Huko mbele tutazidi kumuelewa.
Tatizo siku hizi mitandao imevamiwa na watoto wadogo na wahujumu mkuu. Uwezo wao wa kufikiria nje ya boksi na kutumia busara ni mdogo sanaaaaa,ndio maana huwa wanatukana watu humu kutwa nzima.
Hawawezi kujenga hoja kwa hoja. Watamuelewa Mh Rais...mbona wanacheza ngoma yake kwa sasa. Ni tokomile kwenda mbele mkuu.
 
Nape alikua waziri wa habari sidhani kama kukaa kimya ilikua ni suluhisho.Maadam rais Magufuli ameamua kumkumbatia Mkuu wa mkoa wa Dar kuliko mtu yeyote, ngoja tuone mwisho wake.Ukweli ni kwamba Makonda na Magufuri wana siri nzito na tutaijua tuu siku wakikorofishana.Maana ulimi hupeleka chakula kwenye meno lakini meno yasivyo na shukrani huwa yanang'ata ulimi wakati fulani.
Hahahahahahah
 
Ebu nitajie basi vitabu vitatu vya msingi ambavyo vitanisaidia kuelewa dhana ya uzalendo kwenye context ya Tanzania.
Anza na kusoma hiki kitabu "Maisha na Harakati za Kazimoto" kimeandikwa na Nekemia Mussa Kazimoto. Unaweza ukapata mawili matatu ambayo yatakusaidia kujitambua na kujielewa. Kila la kheri.
 
Ila clouds nao wanafiki kweli mpaka sasa kwanini wasifungue kesi
Wasitufanye wajinga sisi

Clouds ndo chanzo cha yote haya
 
Anza na kusoma hiki kitabu "Maisha na Harakati za Kazimoto" kimeandikwa na Nekemia Mussa Kazimoto. Unaweza ukapata mawili matatu ambayo yatakusaidia kujitambua na kujielewa. Kila la kheri.
Yaani hicho kitabu ndicho kitanipa uelewa wa dhana ya 'uzalendo'?

Kwa maelezo haya mafupi tu ya kitabu, I'm not tempted to read it:

"Hii ni historia ya Maisha na Harakati za Mtanzania mmoja. Ni safari ndefu. Ukikisoma unapata mafunzo mengi, mojawapo ikiwa kuwa kazi ndiyo humpatia mtu heshima katika jamii. Mvivu na mlevi hawana heshima."

Maana hapa sijaona ni namna gani nitaelewa juu ya dhana ya 'uzalendo'. Na pia kinaonekana kuwafaa lightweights...

Nimekuomba vitabu vitatu. Ungekuwa mwelewa, ungeelewa kwanini nimekuomba kitabu zaidi ya kimoja.
 
Soma kitabu acha ujuaji. Umeniomba vitabu vitatu mimi maktaba!?
Kama hujaona namna gani utaelewa then hakuna haja ya kuendelea na hii hoja kati yangu na wewe. Kila la kheri.
 
Mleta mada umeona mbali sanaaaa....Bravo.
Hizi huwa zinaitwa " calculated moves". Mh Rais anahujumiwa dhahiri,halafu kuna watu wanatetea upuntunyu na kuhemka kwa mambo wasiyoyajua.

Kuna dots ukiweza kuziunganisha utamuelewa Mh Rais na kauli yake aliposema "CCM kuna Wasaliti".
Tatizo letu Watanzania huwa tunapenda kukurupuka na mihemko inayotuvuruga akili na kutuvua busara na UTU pale tunapoletewa jambo geni. Leo hii ikiletwa au ikitengenezwa habari ya "Nyama ya Nguruwe yakutwa ndani ya Msikiti wa Mtoro"...hiyo ndio itakuwa habari ya mjini na haya mengine yote yatasahaulika!

Tujifunze kutafakari na kufikiri nje ya boksi. Kuna mengi tunayajua na mengi hatuyajui....Mh Rais anapelekewa taarifa, sidhani Kama huwa anakurupuka kama Wanaharakati wanavyotaka kuuaminisha UMMA wa Tanzania. Muda ndio utaongea. Tuache kuishi kwa mazoea,tuishi kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni za Nchi.

UZALENDO KWANZA VYAMA VYA SIASA BAADAE.
Hata mimi naona dalili za hujuma, hivyo mkuu aongoze kwa mkono wa chuma kama putin, ndo solution ninayoiona
 
Nape alikua waziri wa habari sidhani kama kukaa kimya ilikua ni suluhisho.Maadam rais Magufuli ameamua kumkumbatia Mkuu wa mkoa wa Dar kuliko mtu yeyote, ngoja tuone mwisho wake.Ukweli ni kwamba Makonda na Magufuri wana siri nzito na tutaijua tuu siku wakikorofishana.Maana ulimi hupeleka chakula kwenye meno lakini meno yasivyo na shukrani huwa yanang'ata ulimi wakati fulani.

Wana JF nilisema awali Nape hana mandate ya kuunda tume ya kumchunguza mteule wa rais kama RC bila kumshirikisha mkuu wake! Kama alikuwa hajui utaratibu basi hakufaa kuwa waziri pia hakumshirikisha hata mwanasheria mkuu wa serikali ambayo ni mbaya zaidi. Mimi nionavyo Nape hakufaa kufanyakazi serikalini angeendelea kuwa msemaji wa chama. Serikalini kuna utaratibu kitu chochote kinachohusiana na sheria lazima umshirikishe mwanasheria wa serikali ndo maana hata wajumbe wa tume yake walikuwa biased!!
 
Back
Top Bottom