Mara ya mwisho uliona lini ......!!!?

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,270
8,033
Mwanasiasa gani Tanzania anayeweza kuvutia umati mkubwa namna hii bila watu hao kuhongwa? Mimi nakumbuka nilikuwa Jamhuri stadium Dodoma mwaka 1989 au 1990 Nyerere akiagwa alipoamua kuachia uenyekiti wa chama na wakati alipohutubia baada ya Madiba kutoka gerezani. Sijaona nyingine tena kama hii.

71598_457101522471_823957471_5395767_2365798_n.jpg
 
hivi kweli hapo kwenye huo umati wa watu mie simo???? haiwezekani ngoja nikachungulie!!! lazima nimo tu.
 
Wingi wa watu kuhudhuria mikutano sio lazima wawe wote wanakukubali. Hapo wapo mchanganyiko wengine ni wasikilizaji tu, wengine wa vyama vingine. Na NOTE kuwa hali ngumu ya maisha inawavuta watu wengi kuja kusikiliza kama kuna jipya la kuwaboreshea maisha na sio kwamba wataamini kila unalosema. Wanapima, wanachuja. Hivyo wingi wa mahudhuria si hoja.
 
hivi kweli hapo kwenye huo umati wa watu mie simo????

haiwezekani ngoja nikachungulie!!! lazima nimo tu
 
Wingi wa watu kuhudhuria mikutano sio lazima wawe wote wanakukubali. Hapo wapo mchanganyiko wengine ni wasikilizaji tu, wengine wa vyama vingine. Na NOTE kuwa hali ngumu ya maisha inawavuta watu wengi kuja kusikiliza kama kuna jipya la kuwaboreshea maisha na sio kwamba wataamini kila unalosema. Wanapima, wanachuja. Hivyo wingi wa mahudhuria si hoja.

swala hapa ni wingi wa watu tu! hiyo kukubali au kukataa ni issue nyingine. unadhani wanaohudhuria kwingine huwa wote wanakubali au wanakataa?
 
Kipya kinyemi. Wanataka kusikiliza huyu mpya anayejitokeza anataka kutuambia nini, tofauti na wale ambao ameshazoea kuwaona kwenye majukwaa. Ni hilo tu.
 
Mwanasiasa gani Tanzania anayeweza kuvutia umati mkubwa namna hii bila watu hao kuhongwa? Mimi nakumbuka nilikuwa Jamhuri stadium Dodoma mwaka 1989 au 1990 Nyerere akiagwa alipoamua kuachia uenyekiti wa chama na wakati alipohutubia baada ya Madiba kutoka gerezani. Sijaona nyingine tena kama hii.

71598_457101522471_823957471_5395767_2365798_n.jpg

Siku zote ukiwa muongo muongo na msanii ndio unapata umati wa watu kukusikiliza, hakuna cha zaidi.

Mara oooh Dowans ya Kikwete, mara ooohhh Mkuu wa mkoa kafa. Mara ooohhhh, nimeoa mke wa pili!

Duhhh! Hata Nyerere alikuwa akivuta umma mkubwa sana watu, lakini ikifikia kwenye utendaji ni ZERO.
 
Hapa wapi mkuu!!
 
Wingi wa watu kuhudhuria mikutano sio lazima wawe wote wanakukubali. Hapo wapo mchanganyiko wengine ni wasikilizaji tu, wengine wa vyama vingine. Na NOTE kuwa hali ngumu ya maisha inawavuta watu wengi kuja kusikiliza kama kuna jipya la kuwaboreshea maisha na sio kwamba wataamini kila unalosema. Wanapima, wanachuja. Hivyo wingi wa mahudhuria si hoja.

Wewe una mawili, Haujasoma kabisa (hata chekechea) au umesoma kwa kukariri. Jibu swali MARA YA MWISHO ULIONA UMATI GANI MKUBWA WA MWANASIASA WA HAPA TANZANIA, AMBAYE HAJAWAKODIA WANANCHI MAGARI YA MJI MZIMA KUWAPELEKA KWENYE MKUTANO, HAJAWAHONGA WANANCHI MA-TISHIRT, KANGA, VITAMBAA ILI WAHUDHURIE, bali wameenda wenyewe.

Watu wenye makosa ya kiutawala kama wewe na wifi yako kikwete siku zote tutawajua tu, kila kitu nyie mnajua kujihami tu bila kuangalia kilichosemwa.

Mkuu UTINGO, kiu'kweli, nimeshasahau hata ni lini mara ya mwisho kuona umati mkubwa namna hii wa watu, ambao hawajahongwa, hawajakodiwa mabasi kwenda kwenye mikutano, hawajapewa tshirt, kanga, vitambaa, kuhudhuria mkutano wa mwanasiasa yoyote tanzania, nimesahau kwakweli.
 
Siku zote ukiwa muongo muongo na msanii ndio unapata umati wa watu kukusikiliza, hakuna cha zaidi.

Mara oooh Dowans ya Kikwete, mara ooohhh Mkuu wa mkoa kafa. Mara ooohhhh, nimeoa mke wa pili!

Duhhh! Hata Nyerere alikuwa akivuta umma mkubwa sana watu, lakini ikifikia kwenye utendaji ni ZERO.

mbona majamaa wa chama tawala ndiyo wasanii sana na hawapati watu?
 
Wewe una mawili, Haujasoma kabisa (hata chekechea) au umesoma kwa kukariri. Jibu swali MARA YA MWISHO ULIONA UMATI GANI MKUBWA WA MWANASIASA WA HAPA TANZANIA, AMBAYE HAJAWAKODIA WANANCHI MAGARI YA MJI MZIMA KUWAPELEKA KWENYE MKUTANO, HAJAWAHONGA WANANCHI MA-TISHIRT, KANGA, VITAMBAA ILI WAHUDHURIE, bali wameenda wenyewe.

Watu wenye makosa ya kiutawala kama wewe na wifi yako kikwete siku zote tutawajua tu, kila kitu nyie mnajua kujihami tu bila kuangalia kilichosemwa.

Mkuu UTINGO, kiu'kweli, nimeshasahau hata ni lini mara ya mwisho kuona umati mkubwa namna hii wa watu, ambao hawajahongwa, hawajakodiwa mabasi kwenda kwenye mikutano, hawajapewa tshirt, kanga, vitambaa, kuhudhuria mkutano wa mwanasiasa yoyote tanzania, nimesahau kwakweli.

Ukiulizwa swali, angalia hilo swali limebeba ujumbe gani, usiangalie tu unaulizwa nini. Ndivyo nilivyofanya mimi. Hapa ana ujumbe kuwa Umati huu ni kwa kuwa fulani ni maarufu sana, anapendwa sana, anafaa sana n.k. Kama nimesoma au sikusoma usijali, angalia hoja tu. Ni katika kuchangia na kupeana facts na kuelimishana. Usipoelimika wewe, wapo watakaoambulia chochote katika mchango huu. Ahsante.
 
Aahhh kumbe ni chuki tu binafsi, hakuna zaidi.

Point of correction,

SIo chuki binafsi, ila ni chuki ya kuibiwa haki zetu waziwazi, yaani chuki ya kutangaziwa raisi aliyeshindwa uchaguzi (kikwete) badala ya aliyeshinda (DR. (PHD) Slaa), ni chuki ya jinsi raisi aliyeiba kura anavyoshindwa kuiendesha nchi hali inayosababisha maisha kuwa magumu, ni chuki ya kuona asilimia kubwa ya ndugu zetu wakiishi kwa mlo mmoja wa kubahatisha huku wengine wakifa kwa njaa, ni chuki ya kuona asilimia kubwa ya ndugu zetu wanashindwa kununua hata nguo kwa ajili ya kujisitiri achilia mbali kuwapeleka watoto wao shule, huku wao wachache walioamua kuibaka nchi wakiwasomesha watoto wao kwa gharama kubwa katika nchi za watu japo hawana akili.

ni chuki ya kuona kwamba raisi aliyejitangazia ushindi, amewapa nchi wahindi 2 na mmasai mmoja (RA, Manji & Low-hasa)

Ni chuki ya kuona gharama za maisha zinapanda huku pato la mtanzania likiwa palepale, zaidi makato ya kodi yanaongezeka ili kukipunguza kipato kile kidogo unachopata.
 
Back
Top Bottom