Mara nyingi majina huendana na tabia

Mara nyingi majina huendana na tabia

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,969
Nimefanya kauchunguzi kangu kadogo tu. Nimegundua asilimia kubwa majina huathili maisha yetu ya kila siku.

Kwa mfano mimi Annael maana yake ni mtu aliye na Mungu. Limekuwa likinisaidia sana.

Unamkuta mtu kaitwa shida, matatizo nk. Asilimia kubwa mtu huyo atahangaika sana katika maisha.

Sisi wazazi tujitahidi sana kuwapa watoto majina mazuri.

Vilevile wa JF hapa jukwaani utagundua kabisa tofauti. Watu wamejipatia user name za ajabu ajabu ukiangalia hata tabia zao hapa jukwaani zinaendana na majina yao. Jaribu kufuatilia kido utaniambia.

Ni hayo tu.
 
Jakaya kikwete anakiwa na tabia gani?
 
Utanunua mbuzi kwwnye gunia. Hii ni mitazamo iliyoathiriwa na makuzi yetu.
 
Kuna kaukweli. Majina yanaendana na tamaduni. Na tamaduni zinabeba tabia. Kama wazazi wako ni wacha mungu, watakupa jina la hivyo na kukulea katika mlengo huo. Kama ni wanasiasa, watakupa majina ya kisiasa na huenda ukawa groomed hivyo pia.

Kongosho jina lake la nyumbani anaitwa kivuruge kipandauso. Unategemea nini?
 
Last edited by a moderator:
kinachotu shape ni socialization, hasa ya awali.

Vipi huyu kivuruge kipandauso angelelewa New York kwa Natalia tangu ana mwezi.0?

Labda ningekuwa Riri.
Kuna kaukweli. Majina yanaendana na tamaduni. Na tamaduni zinabeba tabia. Kama wazazi wako ni wacha mungu, watakupa jina la hivyo na kukulea katika mlengo huo. Kama ni wanasiasa, watakupa majina ya kisiasa na huenda ukawa groomed hivyo pia.

Kongosho jina lake la nyumbani anaitwa kivuruge kipandauso. Unategemea nini?
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hapa baadhi sijui hamjanielewa au sijaeleweka.
Nimesema mara nyingi sio mara zote.
Angalia trend ya majina ya steve mara nyingi wamekuwa watu maarufu.
 
La Familiaaaa Lamar Classmate King kong Tanzaniaaa Tanzaniaaaaaaa haaaaaaaaaa kwanza mie nina kipaji toka kwa mungu baba mama mzazi amenijalia nifike mbali nimewakamata level zangu hawanifikii napata heshima mafans wa kila aina silii njaa nipo peace linanilinda jina I'm king kong
 
Si kwel ni jamii inayomzunguka mhusika kuanzia wzaz, ndo inayoshape tabia ya mtu na mtu huyo anauwezo wa kubadika kulngana na mazngira
 
Hata kama jina ni la kienyeji maana halisi ya hilo jina. Mabula huendana na baraka.
 
Nadhani hapa baadhi sijui hamjanielewa au sijaeleweka.
Nimesema mara nyingi sio mara zote.
Angalia trend ya majina ya steve mara nyingi wamekuwa watu maarufu.

Oohps Steve nyerere,steven kanumba,Steve Steve !!!!!
 
Nadhani hapa baadhi sijui hamjanielewa au sijaeleweka.
Nimesema mara nyingi sio mara zote.
Angalia trend ya majina ya steve mara nyingi wamekuwa watu maarufu.

Namiye ntamuliza mwanangu kabisa kabla sijamzaa unataka kuwa maarufu? Akisema ndiyo nampa jina la Steve.
 
Back
Top Bottom