Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

 


Nime quote maneno yako mwenyewe unaonekana ku ji contradict! Naibu Spika alikuwa right kwa vipi? kwa nini hakumpa nafasi Mnyika kueleza sababu zinazofanya amwite raisi dhaifu? Kwani tofauti ya Mnyika na wewe si ni kwamba Mnyika amesema hiki ulichoandika wewe hapa, yeye ameongea bungeni? Kwani Mdhaifu si mdhaifu tu? Udhaifu ni tusi?Mdhaifu tumpake kilemba cha ukoka kwa kumwambia wewe ni imara sana hata mafisadi wakisikia jina lako tu wanatetemeka! Pasco acha kuwa mdhaifu wa kufikiri..
 
Kaka Pasco bado nataka kuendelea kukuheshimu, personally na michango yako hapa jukwaani, convince me please. Aisee!
Sr. Magdalena, nikuconvince nini?, Mnyika si ametolewa nje kwa kumuita JK 'dhaifu'!

Kuita mtu 'dhaifu', kama ni kweli aliyeitwa dhaifu ni dhaifu kweli, then sio lugha ya machukizo!, lakini kumuita mtu 'dhaifu', na kiukweli huyo aliyeitwa 'dhaifu' sio dhaifu, huko ni kumtukana!.

Udhaifu ni hali tuu (intangible state) na ni relative (huwezi kui quantify) kama nusu glasi ya maji, kwa mengine ni yamejaa mpaka katikati, na kwa mwingine, ni yamepungua mpaka katikati. (half full =full half) na wote wako right!.

Wakati mmoja anamuona mwingine ni dhaifu kwa kutofanya maamuzi magumu kuhusu jambo fulani, mwingine anamuona shujaa kwa uamuzi huo huo!.

Mfano kitendo cha JK kuyasamehe majizi ya EPA!, kwa mwingine huo ni udhaifu na kwa mwingine ni ushujaa, huruma na upendo!. Wakati mmoja anaona huo ni udhaifu kwa rais kuvunja katiba na kuyasamehe majizi yale kabla hayafikishwa mbele ya vyombo halali vya kisheria kwa mujibu wa katiba, kwa wengine, kitendo hicho cha rais akinatafsiriwa kuwa ni upendo mno na majizi ya pesa nyingi, kufuatia upendo huu, rais ameingia huruma watu hao anaowapenda wasiende kuteseka jela, hivyo akawasamehe kwa upendo na huruma!. Sasa unapomuita rais JK ni dhaifu kwa watu walikula upendo na huruma yake, huku kwao ni kumtukana, ndio maana nikasema Ndungai was right, Mnyika amemtukana rais mwema na mwenye huruma kuwa ni dhaifu!.
 
Mimi nadhani kutokana udhaifu wa kutojiamini au kukimbizana na kivuli chake analazimika kutumia mbinu/strategy ya divide and rule iliyotumiwa na wakoloni kujilinda. Na strategy/mbinu hii sasa ndo inakiua Chama chake. Yaani kama una ugomvi na Lowasa mweke adui wa Lowasa Kama Nape, Sitta, Mwakyembe ktk nafasi ya uongozi ili waendelee kugombana wewe unapeta. Hapa dhana yake ni kwamba wasije wakawa wamoja dhidi yake. Ni ktk serikali hii nimesikia mawaziri na manaibu wanagombana, mawaziri kwa mawaziri wanagombana live, mawaziri na makatibu wakuu au makatibu vs manaibu wao. Na kila mmoja anajiamini kwa sababu kila mmoja anadhani yuko na Rais upande. Kumbe Bosi wao anatumia uswahili au outdated strategy ya divide and RULE kupambana na kivuli chake - mitandao.Ifahamike kama uliingia madarakani kwa mtindo wa mtandao mpaka ukamshinda chaguo la Rais aliyeko madarakani, basi lazima ujue kwamba kitu cha kwanza utakachofanya ukiwa ikulu ni kuhakikisha kuwa fimbo uliyotumia (mtandao) kuwachapa adui zako isije ikatumika dhidi yako. Na ili mtandao mkubwa dhidi yako usiundwe ni kuhakikisha kuwa unatumia nafasi yako na ushawishi wako kutengeneza migawanyiko ktk makundi ya watu ndani ya serikali na ccm kuhakikisha kuwa hawaundi mitandao itayokudhuru wewe ukiwa madarakani au baada ya kustaafu. Na ndiyo maana kuna tetesi pia kuwa mbinu/starategy hii ya divide and rule ndiyo iliyotumika kumfitinisha na best yake Lowasa. Wakaamua kumtegesha wenyewe kwa kashfa ya kuchonga ya Richmond na EL akaingia line. Baada ya kuona kuwa Rafiki hana shukrani kutokana na yeye kumbebea kashfa ya wote majuzi kwenye NEC yao akaamua kumwaga ugali Lowasa aliposema, Mh. Rais wewe wajua kila kitu kuhusu Richmond hata nilipotaka kuuvunja mkataba wewe ulinikatalia. Huu ni mmoja wa udhaifu wa Kikwete.
 
Mkuu Mtanzania Imara, naomba unisome tena kwenye posti #104 kama bado hujanielewa nijulishe nitakuelekeza tana!.
 
Mkuu Mtanzania Imara, naomba unisome tena kwenye posti #104 kama bado hujanielewa nijulishe nitakuelekeza tana!.

Nimesoma nimekuelewa ila sentesi hii uliyomaliziana nayo nafikiri ungeiweka hivi ingeeleweka zaidi "Mnyika amemtukana rais mwema na mwenye huruma kuwa ni dhaifu mbele ya wale wanaomuabudu na kumheshimu katika udhaifu wake"!
 

hapo kwenye red:
Ikulu? Hii ni unpractical unless labda CCM na wapinzani ni mke na mumewe ambapo wote wapo Ikulu. Wapinzani wana wajibu wa kuwalazimisha CCM ama JK kusikia mawazo yao kwa kupitia wananchi na si kwa urafiki na JK au Ikulu.

Pia JK hana haja ya kuambiwa na wapinzani bali kukaa kikao na watu wake (CCM) na kufanya mambo tokana na uwezo wao au desturi zao (taboo zao) za CCM ili kuinua maisha ya raia. Anaweza sikia vilio vya raia (Wapinzani ni raia pia) lkn si kwa msingi wa upinzani. Wapinzani wapo ili kuiondoa CCM Ikulu sasa iweje JK awakaribishe chumbani kwake - labda ili kujua undani wao ili kuwabomoabomoa kwa amani.

CCM wamejaribu mengi kwa miaka mingi sana hivyo haiwezi okolewa na mawazo ya Wapinzani - JK na CCM yao haina uwezo tena wa kuijenga TZ imara na muda wa kumshauri JK ulishakwisha labda kama watz bado ni malimbukeni wa pilao la bure.
 
Mkuu Pasco, nilikuwa tayari nimeshaanda mada juu ya udhaifu wa Raisi wetu na nilitaka kunukuu mada yako Mada yako kuhusu miongoni mwa mazuri ya Raisi Kikwete, lakini katka kutafuta kumbukumbu nimeona tayari mada hiyo ipo na umenisaidia sana kwani ni yale yele uliyoyaeleza hapa ndio yalikuwa kiini cha mada yangu.

Katika kusoma mada yako nimekumbuka ule mzaha wa Mswahili unapomuuliza habari za Wife wako akakenua na ukimuuliza Habari za Mkeo akarusha ngumi. Hivi ndivyo ulivyofanya Mkuu wangu. Ulituhadharisha kwenye mada tusitumie lugha ya matusi na kebehi lakini wewe uliizimua yako kwa kumwita Weak baada ya Dhaifu. Unaweza kujitetea kwa kusema lakini wewe sio mbunge na uko sahihi, lakini mahali kama bungeni kulainisha lugha mpaka ikapoteza lengo lililokusudiwa pia ni kutowatendea haki Watanzania.

Pengine Mnyika asingetolewa nje kama angesema Our President is weak badala ya dhaifu. Unaona kwa nini Lissu hakutolewa nje?, kwa aliliita Silly Parliament badala ya Bunge la Kipuuzi.

Anyway, nakimbilia darasa zangu za Kingereza ili nisalimike na mikwanja ya Waswahili wenzangu.
 

Mkuu Mama Mia, naungana na wewe kuwa baadhi ya maneno ukiyatumia ya kizungu, unapunguza makali, mfano
shit, fool, weak, "slept", 'FU', gay, fox, etc!, leo katika mchango wake, Freeman Mbowe kumuunga mkono Nyika, ila yeye yeye amekuwa too general kuwa "serikali ni dhaifu", na "viongozi wake ni dhaifu" na hakukuwa na muongozo wa spika!, kosa la Mnyika ni kuwa very specific, Rais Kikwete ni Dhaifu"! Angeishia rais ni dhaifu bila kutaja jina, angesalimika!.
 
Nimesoma nimekuelewa ila sentesi hii uliyomaliziana nayo nafikiri ungeiweka hivi ingeeleweka zaidi "Mnyika amemtukana rais mwema na mwenye huruma kuwa ni dhaifu mbele ya wale wanaomuabudu na kumheshimu katika udhaifu wake"!
Mkuu Mtanzania imara, kama tumeshakubalia neno "dhaifu", ni relative, wengine wakiona udhaifu kama sifa, hivyo sentensi yako bado haijakaa vizuri, labda ingekaa hivi ingekuwa valid, "Me"nyika amemuita rais JK kuwa ni dhaifu, hivyo kuonekana kama ametukana, na kutolewa nje na wale wanaomuona ni rais shupavu, mwema na mwenye huruma"!, kumbuka udhaifu ni kwa macho ya Mnyika, kwa Lukuvi na Ndungai, ni Shujaa!.
 

Understood,agreed!
 
Ingawa ninakubaliana nawe juu ya matumizi ya Politeness katika mazungumzo yetu, bado sioni kama Mnyika kwa kumwita Rais Kikwete dhaifu amekosa hiyo politeness; neno hawajibiki (irresponsible) ni kali zaidi. Nisichokubaliana na Mnyika ni kupewa fursa ya "kutubu" akaipoteza. Mnyika tayari alishapeleka ujumbe wake, waliosikia walishasikia, kwa hivyo athari ya maneno yake haifutiki kwa kusema tu "nafuta kauli yangu".

Bado naona kuna udhaifu wa bunge letu kwa kumruhusu mtu amwage "malusinde" anayotaka halafu aseme ninafuta kauli yangu, yamekwisha.
 
Pasco, thread yako nzuri kiasi; si kweli kuwa huruma na upole wa Mr. President ndo umepelekea haya yote. Mr. President ameshindwa kabisa kuchukua maamuzi magumu ktk mambo mengi ya msingi, kusamehe wezi wa fedha za EPA huwezi kusema ni huruma, not at all; fedha ya rada ilipelekea waziri kule England amabo wanatupa misaada kujiudhuru, but sisi haman kilichofanyika, no uruma wala upole hapo; kushindwa kufanya TZ inufaike vya kutosha na madini huo sio huruma wala upole, not at all. yaani, tukianza kuyataja hayo mambo hapa ni mengi mno. in short Mr. President hawezi kufanya maamuzi magumu, hii inapelekea wengi kuhisi kuwa na yeye ana hisa ktk mengi ya hayo yanayotokea!!!!!! anyway, I believe labda he'll change in the near future!!! Mungu ibariki JMT, Mungu mbariki Mr. President wetu, Amen.
 

Mie Wakuu sioni mantiki ya "Watendaji wanamwangusha"! Kwani hayo MADARAKA aliyonayo Rais kwa mujibu wa katiba yanatumikaje KUWASHUGHULIKIA wanaomwangusha? Kuhusu mission na Vision, sijasikia Rais akiongelele Maisha BORA kama alivyoahidi kwenye kutafuta nafasi hiyo, angalau kuonesha mwelekeo wa kufikia hiyo mission yake! Na je, hiyo ARI bado ni MPYA? Kasi je? Nguvu ziko kiasi gani? Pamoja na hayo sijamsikia Rais wangu tangu aingie madarakani, kutest uwezo wake wa kuchambua hali ya Vision yake kwa kuongea na kujibu maswali ya Waandishi wa habari. Nakumbuka Mkapa alishawahi hojiwa na Jerry Lary yule Mwamerika wa "Kiti moto". Je, katika ziara za nje Kurugenzi ya habari haitayarishi fursa hizi?Tusemezane, hapa hakuna udhaifu?
 
He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Why not this way?

Vision = maisha bora kwa kila Mtanzania
Mission = ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!
 
Kwani tulimuomba kuwa kiongozi wetu, mbona nyie watu mnajaribu kumpamba ? Rais maana yake ni nini ? ni kiongozi anayepashwa kutuonyesha njia, ndio maana tunamlisha na kumtunza maisha yake yote hili yeye akae atafakari awe makini , afikiri badala ya sisi na kutuonyesha njia ya kutupeleka kwenye neema na maisha bora. Sasa kama anashindwa anakaa kufanya nini, kama hawezi kuongoza vizuri anataka nini . Si apishe wenye uwezo wakafanye kazi , sio kutupotezea miaka kumi kwa kucheza kiduku.Jamani watanzania watu wenye uwezo mbona wapo kibao.Kwa nini mnataka kumpamba Kikwete kuwa ni mtu makini ? kafnya nini cha maana ?
 
Huyu jamaa ni bingwa wa propaganda. Alianza na ukanda haikufanikiwa sana. Akaja na udini, sasa inaligawa taifa vipande viwili. Sasa ameleta nyingine kali. Eti yeye ni mzuri ila watendaji wake ndio wanaomwangusha! Very foolish propaganda maana inathibitisha udhaifu wake. Kama kweli kinyago ulichokichonga mwenyewe hakiwezi kukutisha iweje watu aliowachagua mwenyewe wamwangushe nae awaache tu! Wanafanya madudu,anawaangalia tu, wananchi wanapiga kelele waondolewe, anawaondoa huku akiwatetea na kulalamika! Mara ni ajali za kisiasa, mara watendaji wa chini ndio tatizo, mara wamewajibika kisiasa tu! Huu ni udhaifu mkubwa!
 



Ikumbukwe siku zote, kikwete aliingia awamu hii akikabiliwa na tuhuma mzito na ya aibu ya "Kuchakachua kura" ama "kuiba kura" kwa kushilikiana na usalama wa taifa, Nec na ccm yake!
Kwa kusingatia tuhuma hii si halali kusema alichaguliwa na Wtz na kwamba wa kulaumiwa ni wapiga kura wake, ambao kimsingi maamuzi yao yalipotoshwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…