Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Tangu tupate maraisi hatujawahi kuwa na rais mnafiki, mzembe,dhaifu na ndumila kuwili kama kikwete uendeshaji serikali yake umejaa fitina dhihaka na upuuzi mwingi anyemshabikia huyu naomba aweke haya maelezo kwa kuprint au kucopy na baa ya 2015 mtaona kwa nini tz imefika hapa ilipo ni sababu ya huyu mr dhaifu hakuna alichowahi kuongoza kikafanikiwa zaidi ya kutengeneza makundi ndani ya chama na nchini ili awe madarakani kirahisi mungu ibariki tanzania kwa haraka sana tuondokane na huyu mnafiki

mjaka
Isije ikawa wewe ndio mnafiki na 1; tatizo lenu wanafiki mnakuwa hamjijui!!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
​ukweli unauma lakini ni ukweli tu mafiki tu huyo kama ni bwana wenu ni nyie tu mie sijamchagua huyu ****
mjaka
Isije ikawa wewe ndio mnafiki na 1; tatizo lenu wanafiki mnakuwa hamjijui!!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Naungana na ww mjata huyu jamaa,anapenda sana majungu naanayafanyia kazi,kisirani kama nyegeri.kamfanyi uzandiki nduguyangu mmja hatuna hamu nae huyujamaa!sijui ndio uswahili? Au kanywa sana madafu utoto hatasielewi!!
 
​ukweli unauma lakini ni ukweli tu mafiki tu huyo kama ni bwana wenu ni nyie tu mie sijamchagua huyu ****

Akili zako finyu sana wewe kama hukumpa kura yako ni haki yako ya kidemokrasia; mh. Kikwete ni bwana/mume wa Bi Salma sisi kwetu ni Raisi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
IlikuwanPombe nini maana wengine mna hasira na hamuelezi chanzo au mnataka nini ni matusi tu, Tumeyazoea hata Bungeni yapo lakini akitokea Livingstone au Mwigulu mnagwaya na kulalamika.
 
Ng`hily
Siongelei ushabiki leo hii nilikukumbuka sana mwanaforum Ng`hily heshima yako!

Chama
Gongo la mboto DSM

Nimekusoma mkubwa na nashukuru kwa kunikumbuka kamanda..Namshukuru Mwenyezi Mungu coz naendelea vema mkuu..Pamoja sana mkubwa chama...
 
Nimekusoma mkubwa na nashukuru kwa kunikumbuka kamanda..Namshukuru Mwenyezi Mungu coz naendelea vema mkuu..Pamoja sana mkubwa chama...

Ng`hily
Poa Mungu akujaalie na kukupa wepesi kwenye mipangilio yako!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Huu nao ni uhuru wa kutoa mawazo! Demokrasia kweli ina shida zake. Naambiwa wakati wa mfumo wa kisoshalisti huko ulaya mashariki ulikuwa huruhusiwi kuipinga serikali hadharani ama kutoa mawazo yako yaliyo tofauti. Lakini kulikuwa na viwanja ambavyo ulikuwa ukienda unasema kila unachokitaka; tukana, imba, weweseka, nk. hakuna hatua zozote dhidi yako. Naona hapa TZ hivyo viwanja ni JF! Tusigeuze JF uwanja wa matusi na kashfa. JF iendelee kuwa chemichemi ya hoja zenye masilahi kwa taifa badala ya uwanja wa matusi.
 
Acha kulia lia wewe,fanya kazi kwa bidii!kwani jk ndio aliekuzaa,mlaumu aliekuzaa na kukunyima misingi bora ya maisha yako inayokufanya leo utange tange bila mwelekeo wa maisha.
 
Mjaka!mjaka!mjaka!amini,amini nakwambia huyu dhaifu ndio anaelekea kuanguku yeye na utawala wake,,mkiyaona hayo basi mjipe nguvu kuvipiga vita dhidi ya madhaifu wote.
 
Kikwete ni chagua la Mungu. Mungu anataka awafundishe somo wa Tanzania.


Hapo umenenena.....................MUNGU ametupa JK ili iwe fundisho kwa karne ijayo. Tumekuwa tukichagua viongozi kama wasimamizi wa ''Kitchen party''. Sasa tangu 2005... mmepata somo la kuwatosha. Haiingii akilini eti mtu anachaguliwa simply ana sura nzuri...au uso wa tabasamu... Mbona aibu nduguzangu karne hii kutumia vigezo dhaifu kama hivo
 
Kikwetealichotaka ni kuweka historia kwamba nae alikuwa rais wa Tanganyika. Lengo la kugombea urais hakulijua alidhani urais ni kukaa Ikulu na kusafiri nje kama alivyokuwa waziri wa mambo za nchi za nje. Hakujua kuwa urais ni kazi kubwa kuliko yote kwani macho yote ya watanganyika wanakuangalia ww. Inabidi kichwa kifanye azi.
 
Wanabodi,
Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais weak"!,: asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

Nawatakia majadiliano mema.

Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

Wasalaam

Pasco wa jf.

NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.

Naomba usinichefue wewe:
1. Huruma kwa majizi ya EPA? kama unaweza kusamehe watu watano au kumi, ukaharibu uchumi mzima wa taifa lako huo
ni upumbavu. hata dereva anafundishwa kuwa ni bora ukamgonga mtu mmoja aliyeko mbele ya gari lakini ukaokoa
maisha ya wengi uliowabeba ktk gari lako.
2. Hao mawaziri unaosema kawahurumia, walikuwa wanafaida gani kwa watanzania? Kama alidiriki kuwasamehe
ilikuwa ni kwa maslahi ya watanzania?
3. Mpaka muda huu umesikia hatua alizochukuliwa Jairo? Ushahidi ulikwishapatikana kwa kupitia kamati ya bunge
iliyochunguza. Je utasema kuwa Jk ni mzalendo kwa nchi yake wakati analinda mchwa wanaolitafuna taifa?
Naomba utafute hoja zingine za kumlinda kwani hoja ulizotoa ni dhaifu ambazo haziwezi kumlinda kiongozi dhaifu.
 
Ni kweli kuwa rais wetu amekuwa na huruma sana mpaka kuwaidisha baadhi ya watu waovu. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa ni rais aliyefanya vizuri kuliko marais waliomtangulia. Kwani ni yeye pekee aliyeweza kuagiza vyombo vya dola viwaweke rumande na kuwafungulia mashitaka viongozi waovu hata kama watakuwa ni mawaziri. Serikali yake imeweza kuwashitaki wezi wengi kuliko utawala wowote uliotangulia. Kwa taarifa yako kuna mawazi kama Basil Mramba, Daniel Yona na Iddi Simba wanaendelea kupambana na kesi zao mahakamani. Vigogo wengine waliopambana na mkono wa dola ni Amatus Liumba, David Mataka, Shaban Malanda, n.k.
Mwezi uliopita pekee wakurugenzi wa halmashauri wanane walifukuzwa kazi kwa matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ubadhilifu wa mali ya umma. Wakurugenzi waliokwisha hukumiwa ni pamoja na Mohamed Masha aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma.
Hakuna Rais wa nchi hii aliyekwisha fikisha rekodi hii. Nakumbuka wakati wa Mkapa watu walipoleta malalamiko yanayohusiana na viongozi kujitajirisha, Mkapa alisema huo ni wivu tu kwani mawazi wake ni jeshi la mwamvuli la linalochapa kazi kwa ukweli na uwazi. Hii ni kinyume na ukweli kwani mikataba mingi mibovu imesainiwa katika kipindi cha mkapa; kumbuka mikataba ya madini na uuzaji wa mashirika ya umma kama NBC
 
Tatizo kubwa la JK ni kwamba hawezi kufanya maamuzi magumu na ni kigeugeu. Watu wote wa karibu yake wanasema hawezi akikuhaidi kitu, usimwamini. Ilimchukua mwaka mzima kuamua kumfukuza David Jairo ikulu hata baada ya kupata ushahidi kuwa alikuwa mla rushwa. JK alikuwa akilalamika kwa wasaidizi wake bila kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom