Mapokezi ya CHADEMA Kigoma Yamshangaza Lema

Mapokezi ya CHADEMA Kigoma Yamshangaza Lema

Mtu mzima anapozungumza inatia hasira huyu molemo haoni aibu kuongea uongo?

Mbona magamba mnabisha tunapowambua kuwa zitto mmemtuma kuvuruga CDM?Unaona sasa mdada mzima mpaka kamasi zinakutoka kumtetea YUDA ESKARIOT(ZITTO),Yaani maamzi ya kiungwana ya CDM yanawauma sana,na ninyi kama vp mtimue MAMVI UMAGAMBANI,maana badala ya kujenga chama anajijenga yeye kama zitto vile.Inauma eeh? Lakini ndiyo hivyo tena imetokea,mpeni ajira huko.
 
R.I.P Msaliti Zitto, tena usilete ujinga, tulia kama unanyolewa, hayo ndiyo mavuno kwa kile ulichopanda, unamake kolabo na miccm unategemea nn.
 
Nyumba unaanza kuijenga yako kabla ya nyumba ya jirani yako..... unafiki weka mbali na mageuzi

Siasa za Kigoma we mchumia tumbo huwezi kuzijuaMwaka ujao siyo mbali utaona kitakachowapata Chadema. Kwa taarifa yako Manispaa ya Kigoma Uji inaongozwa na Chadema kwa juhudi za Zitto. Huyo Lema anaongea siasa rahisi kwa sababu ya uelewa wake mdogo. Ndo maana alifeli form four sababu uwezo wake mdogo.Tuulize sisi watu wa Kigoma tutakuambia Mziki wa zitto.
 
Kweli Vijana wa CHADEMA mmechoka akili. Ni tusi kubwa sana kumfananisha Zitto huyu kijana Msomi, mzalendo, aliyebobea katika siasa safi, mwenye rekodi nzuri ya kusimamia hoja bungeni kuliko wabunge walio wengi, na huyu kilaza wa Kimachame. aliyekuwa mwizi wa magari kabla ya 2005.

Huwezi kumlinganisha mtu aliyefeli form four na mtu anayemalizia PhD. Ni sawa na kulinganisha maiti na mtu aliye hai
 
Mtu mzima ovyo,molemo achakudanganya watanzania

Mwambie huyo mchumia tumbo. Kwanza Kagogo na iwamtima anapajua? Kazi kupayuka tu. Baada ya Uchaguzi wa Mwaka ujao ndo mtajua umhimu wa Zitto. Nakuhakikishia Mnyika mwenyewe harudi manake aliwadanganya wanachuo kuwa naye kamaliza degree Chuo kikuu cha Dsm. Sasa siri imeshafichuka kila mtu anajua alifeli
 
KIGOMA KASKAZINI
2000 - Madiwani 11
2005 - Madiwani 5
2010 - Madiwani 2
2015 - ???

Go to hell Zitto!!!!!!!

zito ndio anachagua madiwani? jimbo la mnyika ubungo kuna madiwan wangapi wa chadema? acheni kujitoa akili nyie mambururas
 
ngoja niwasubiri warembo wa Zotto waje wamtete......
 
Kuyu ZITTO ZIGO,kumbe alikuwa anachukua mabilioni kwa Magambaz alafu ile MIZIGO mengine anaikatia tu laki moja moja!
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema kuwa juzi walipata mapokezi makubwa mjini Kigoma na kwamba kila mtu akiwa katika chama afanye kazi ya kukijenga badala ya kukibomoa.

Alisema licha ya kuwapo na madai kuwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, ana umaarufu mkubwa mkoani humo, jambo hilo halina ukweli.

Alidai mwaka 2010 walitegemea kupata ushindi katika Jimbo la Mpanda, lakini Zitto aliandika barua akieleza kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, awe mgombea pekee.

Alisema baada ya chama kupata taaarifa na kutaka kumwajibisha Zitto, Mwenyekiti Mbowe, aliingilia kati na kusitisha uamuzi huo.

Alisema kutokana na waraka walioukamata aliodai uliokuwa na malengo ya kukisambaratisha chama, waliona hawana sababu za kuendelea na Zitto na kumvua nyadhifa zake na kwamba kitendo cha kuweka pingamizi mahakamani asijadiliwe kinamfanya awe mbunge wa Mahakama.

Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili, hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.

Katika hatua nyingine na mwendelezo wa M4C OPD Umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Bukoba jana walimiminika kwa wingi katika uwanja wa Uhuru kuwasikiliza Viongozi wa Chadema waliohutubia mkutano wa hadhara.

Kabla ya mkutano huo, yalifanyika maandamano makubwa yaliyokuwa yakiongozwa na vijana waendesha pikipiki.

Source: Nipashe Jumatatu.

too much "alisema".
 
Ubungo wapo 6 kuna swali la ziada?

Mnyika aliwapata kwa ulaghai. Alikua anadanganya kuwa ana degree! Kumbe aliangukia pua. Mi nilishangaa Mnyika kuwa na degree wakati up stairs ni mweupe kama karatasi
 
zito ndio anachagua madiwani? jimbo la mnyika ubungo kuna madiwan wangapi wa chadema? acheni kujitoa akili nyie mambururas

Zito tayari alikuwa maarufu na anajifanya mwamba...sasa kwanin asitumie uwezo wake kushawishi wanakigoma? hata mgombea wa ccm alikuwa ameng'ang'ania...eti tofauti ya about 3000? Hebu nenda kwa Myika aliwafanya nini magamba? Tena wakati huo akiwa junior kabisa...learn to argue
 
Back
Top Bottom