Agreed lakini pia inawezekana waliopita UDSM kabla ya hapo ndiyo waliopigania mazingira kuendesha hayo mapambano ya mabadiliko sasa. Wengine tumezeeka na kuwa wazee wa busara tuu, wengine ni marehemu kwa sasa na wengine wameamua kuachana kabisa na siasa kutokana na misukosuko waliyokumbana wakati ule wa mfumo wa chama kimoja.
Kama alivyosema
David Djumbe, "changamoto zinazojitokeza wakati wa uongozi vyuoni huwa ni mtihani sana na ndio maana wale wanaomaliza migogoro hiyo vizuri huwapa ujasiri zaidi na hatimaye wengi wao huweza kuwa viongozi wazuri...lakini wale wanaoumizwa na changamoto hizo wengi hukosa ujasiri wa kuongoza tena na hivyo kupotea kabisa kwenye siasa..."
Kuna mpaka wengine walishawahi kuwa Rais wa Duruso kwa siku tatu tuu kabla ya kufukuzwa chuo. Cheki hii post ya
Kashaijabutege, "Jasson Kishozi (RIP) alikuwa Rais wa DARUSO (Overall-Mlimani na Muhimbili) kwa kipindi cha siku tatu 6-9 Februari 1992. Alifukuzwa Chuo Kikuu na wenzake 9 ambao walisimama kidete
kupinga mfumo mbovu wa uchangiaji wa gharama za elimu ya juu na kutetea uanzishwaji wa vyama vingi. Wanafunzi hao 10 walifukuzwa tarehe 10 Februari 1992. Waliofukuzwa tarehe hiyo ni hawa:
1. Mh. James Mbatia (Electrical Engineering-4th year)-Mwenyekiti NCCR-Mageuzi
2. Dr. Harun Kimaro (MD 5th year)-Marehemu (Alikuwa mshauri wa MDC Zimbabwe)
3. Fabian Lutalemwa (Pharmarcy 4th year)
4. Rwekamwa Rweikiza (B.com Marketing-2nd year)-Alikuwa Rais wa Daruso Mlimani siku 3.
5. Idrissa Alnoor Ruta (Engineering Civil 4th year)-Mrehemu
6. Ludovick Kashaju Bazigiza (BA Ed 4th year)-Marehemu
7. Mosena Nyambabe (Engineering-Civil)
8. Dr. Kelivin Mmari (Electrical Engineering-2nd yr)-Ni lecturer wa IT Oregon University, USA
9. Jasson Kaishozi (BA Ed-2nd yr)-Marehemu
10.......Kimweri (BA Economics 3rd year)-Marehemu
Baada ya kufukuzwa Kaishozi alikaa mtaani na baada ya miaka mitano alirudi kusoma sheria [inasemekana baada ya Generali Ulimwengu kumwombea kwa Prof. Luwanga na Luwanga kumkubali on the condition kuwa hatajihusisha tena na siasa za chuo]. Alipomaliza alipata kazi kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, kama wakili wa serikali. Kesi iliyompa umaarufu ni ile ya ZOMBE, ambapo yeye ndiye alikuwa mkuu wa jopo upande wa mashitaka (serikali)."
Chanzo: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/87973-ulimjuaje-marehemu-jasson-kaishozi-wakili-kesi-ya-zombe.html.
Kwenye uzi huo huo,
Tiba nae anaongezea,