Mapinduzi Yaliyoshindwa ya DARUSO 2002/3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi Yaliyoshindwa ya DARUSO 2002/3

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Dec 16, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka wakati niko Mlimani, mwaka 2002/3 kulitokea Mapinduzi yalishindwa dhidi ya Serikali Halali ya Wanachuo iliyokuwa chini ya Rais Francis Kayombo!

  Najiulizaga what was the Motive Behind that mapinduzi na nani waliokuwa Nyuma ya yale Mapinduzi(Ambayo hata hivyo hayakufanikiwa)? Mkuu Waberoya nadhani ulikuwamo katika ile Serikali iliyokoswa koswa kupindulia naomba unitoe Kizani
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kama Nakumbuka Vizuri Waliogombea nafasi hiyo walikuwa ni

  1: Francis Kayombo ( Mhandis) Mgombea Mwenza alikuwa binti wa Sheria

  2: Jamaa wa BCOM Simkumbuki jina lake

  3: Marry Mugulusi
   
 3. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Kuna kijana alikuwa anaitwa Msando kwa sasa sijui yupo wapi. Huyo ndo anaweza kutupatia kilichojiri
   
 4. R

  Reyes Senior Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kayombo alishinda kwa ujanja ujanja
  Aliyeshika nafasi ya pili nakumbuka alikuwa anaitwa DEOGRATIUS MTUI inasemekana kuwa hiki kijamaa ndicho kilikuwa kishindi halisi lakini aliibiwa kura na Zitto kwa nia ya kumsaidia Mugurusi na Kayombo akapeta...

  Alberto aliongoza mapinduzi ya kipuuzi akishirikiana na haka kajamaa basi nakumbuka tuliandamana.... Msando are you there? can you tell us what happened?
   
 5. m

  maselef JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilikuwepo siku hiyo wakati nikisoma degree ya kwanza. Nakumbuka aliyetangaza rasmi kuwa Kayombo amepinduliwa ni James Zotto pale Rodney Square na si Msando. Zotto kwa sasa ni Mhadhiri Msaidizi Idara ya Historia na Akilojia pale Mlimani. Kilichofuata katika orodha ya waloisimamishwa masomo baada ya mapinduzi hayo Zotto alikuwemo. Hivyo aliyefanya mapinduzi ni Zotto na si A. Msando. I know zotto si mtu muongeaji sana ila ni mtu anayependa kusema ukweli na hataki kuburuzwa. Masele-PhD candidate Univesrsity of Alberta Canada
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mapinduzi yamekuwa yakitokea Mlimani karibu miaka yote hasa kuanzia miaka ya 1990s mwanzoni. Nimekuwepo pale miaka ya 1990s katikati mpaka karibu na mwisho. Kuna sababu mbili: 1. ni pale serikali iliyochaguliwa na wanafunzi na kuonekana mwiba kwa utawala kununukiwa na utawala baada ya muda kama miezi sita na kushindwa kuwatumikia wanafunzi na kuegemea utawala, 2. ni pale kundi fulani la wanafunzi lilowania uongozi kwa maslahi binafsi na kukosa ridhaa ya kuongoza ufanya mbinu za mapinduzi ili waweze kula bure pale DARUSO bar, kupata mahitaji karibu bure kama accommodation.

  Ndio maana kulikuwa na chombo muhimu sana kilichokuwa kinashikisha adabu utawala, ma-lecturer, serikali ya DARUSO, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafunzi wote, wasaliti na mambo yote yahusuyo maadili ya Kitanzania - chombo hiki kilikuwa kinaiitwa Mzee Punch na logo yake ilikuwa hiyo hapo chini.

  Picture.JPG
  Hii kitu ilimfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi atoe machozi baada ya kuchorwa akiwa mtupu!
   
 7. n

  nkosiyamakosini Member

  #7
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimewapata barabara, in maana mugurusi alikuwa demu wa zitto? thanks
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Dec 17, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Wewe mchokozi sana, mapinduzi yaliongozwa na akina Zitto, Ridhwan Kikwete, A.Msando na Omary Lyas

  walikuwa wanasema tulishinda kijanja kijanja na hawakuwa na imani na ushindi wetu.

  Kumbuka kabla ya Kayombo alikuwepo Rugemarila na kabla ya Ruge alikuwapo injinia mmoja, the war was engineers will never take over the DARUSO again!

  Vita baridi au upinzani wa wahandisi na wasio wahandisi ( ambao tulikuwa tunawaita Mangwin) umekuwapo pale miaka mingi sana. cha ajabu hii vita iko mpaka level ya admistartion ya chuo.Utakumbuka walimu wa sociology, lawasa, FASS, Political science huwa hawapendi kabisa kuongozwa na wahandisi, na hii Luhanga alipata shida sana, mpaka kuliwa kichwa wakati anafanya degree ya sheria!

  Leo hii Mkandala anafanya madudu hutawasikia wahadhiri wasio wahandisi wakipiga kelele sana!!...ni 'wao'

  Back to the maada:

  Nilikuwapo wakati kura zinahesabiwa za urais wa Kayombo, sikuona mchezo mchafu. Ila Ruge alimpa shavu Kayombo na hii ikawahudhi baadhi ya watu. na Ruge ndiye aliyesaini mikataba ya bodi ya mikopo hii watu wanayolia leo, sasa hii ikafanya hata Kayombo aliyekuwa supported na Ruge kuonekana kuwa atafuata nyayo zake tu! sasa hii sababu changanya na ule upinzani wa jadi wa maininjia na mangwin basi hapakukalika. Zitto akaenda kutokea bungeni na kuwa kuliongoza bunge la wanafunzi ambapo kupitishwa kwa mawaziri kulikuwa kasheshe pia.

  Kayombo ni mhandisi yuko kiwanda cha chai Iringa nadhani ina future ana mpango agombee ubunge kule sijajua kwa chama gani

  It was good days, memorable and from that generation today we have good politicians, I mean watu wanaojua siasa sio biashara, ukijua siasa tamu sana unaweza ukawapelekesha watu unavyotaka , na siasa ni hatari sana kama unapata viognozi wenye kujali maslahi yao, basi unaweza ukawapumbaza watu. Personally nimefanya kazi na Zito na Omar Lyas, Kizuri cha zito ambacho huwa nampa shavu, huwa anaquality ya kuangalia mbaaali sana, hili sina wasiwasi naye. Ridhwan nilijua tu alikuwa maneno mengi na misimamo, kama ya akina Zitto na nikajua labda atakuwa kiongozi mzuri, sijaona bado!! A. Msando is another 'animal' in politics sijui yuko wapi.

  Our tactic of ushindi ilikuwa kila second year engineering anaenda na watu wawili kupiga kura, tukaenda kuwabembeleza sociology (you know) na haikuwa shida kwa B.com kuwa upande wetu... ule uchaguzi ushindi haukuwa rahisi, lakini kura hazikuchakachuliwa, ILIKUWA TU NI MBINU YA waliotaka kupindua kujitetea katika hilo. HALI ILIKUWA TETE

  Marehemu Chachage ndio alituita kundi la serikali na wale waliotaka kutupindua kutusuluhisha na kuweka mambo asawa atleast. Ukweli Kayombo alikuwa na support ya administration si kwa ubaya.

  Siyo siri, DARUSO inasaidia sana ku-shape viongozi, kinachotia uchungu viongozi wengi waliopitia DARUSO wako CCM na unajua what is happening there...ufisadi tu

  kwani umekumbuka nini mkuu?
   
 9. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #9
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Historia ni nzuri sana. Nadhani wale tulioshiriki siasa za DARUSO tuandike ili kuweka kumbukumbu. Hata hivyo, mapinduzi yale mimi sikushiriki. Nilisimamishwa masomo kwa kudhani tu kuwa Zitto alishiriki.
   
 10. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #10
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Alberto sasa ni Diwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na leo anachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
   
 11. saed kubenea

  saed kubenea Member

  #11
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana wa chuo mna mambo sana. Nfanyia kazi hoja hii ya Zitto ya kuweka kumbukumbu kwa vijana wangu kisha nitarusha mkanda mzima hapa. Muda hautakuwa mrefu.
   
 12. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kudhurumiwa HAKI ya Ushindi, Mtui kama Dr. Slaa hakufa moyo wala kuhamasisha vurugu. Hekima yake ilimpelekea kuanzisha asasi ya kupambana na RUSHWA ndani ya UDSM. Kama nakumbuka vizuri inaitwa "Combined Efforts Organization Against Corruption-CEOC"
   
 13. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ZT kumbe upo bwana. Mambo vp? Kwanini Waberoya ktk comments zake huwa anamuinclude Ridhiwan kila mara? By the way we had a hot topic about you early this week but u didn't show up.......it's nice to hear from u again.
   
 14. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnaanza kujifunza ufisadi huko. Ndiyo maana mpaka leo mnajenga urafiki na mafisadi.
   
 15. c

  chief pembe New Member

  #15
  Dec 17, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona mnamsahau Mnyika John tuliyemsimika Urais pale Nkuruma hall kabla mapinduzi hayajafanikiwa? mshkaji alitushawishi kwa kupanga hoja mpaka tukamkubali, si mnamuona sasa anavyotisha Ubungo!
   
 16. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,279
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280


  Saed Kubenea Jr member? ama kweli wanafiki hawataisha nchi hii!
   
 17. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mbona mmetoweka jamani kutumia makini halisi raha yaani sijui na mm niingie na langu yaani kubadilishana maneno mkijuana ina utamu wake bwana
   
 18. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa Kayombo hapo hausemi ukweli. Kayombo ni mtu wa Watawala. Na hata akigombea uchaguzi leo hii sitashangaa kama atajitokeza kwa tiketi ya CCM. Hawezi kujaribu kuwa against watawala. Naongea hivi kwa sababu ni mtu ambaye nimesoma naye o-level, A-level na hatimaye UDSM.
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Dec 17, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Kaka inawezekana haukushiriki ila influence yako ilikuwa kubwa sana, pole sana kwa kusimamishwa masomo, na asante kwa hii info,but no one have ever told me different story, apart that you were masterminding every move! LOL! nimeipokea hii kaka

  Sawa ila uulize vizuri hasa muhusika mmoja mmoja,usije ukaweka recodi zetu za simu za miaka 7 iliyopita,mpaka ile simu niliyompigia bibi yangu kumuuliza kama yule bata wangu anataga mayai!!

  He! JF kata bwana! kila mara nina-muiinclude Ridhwan!

  Itafikia muda hautamuamini kila mtu-mpaka wewe mwenyewe,achilia mbali mama yako!

  Kama unasema atagombea kwa njia ya CCM , ni wewe umesema! mimi sijui hilo na sijaona kama nimedanganya ,na ni haki yake kugombea kwa chama chochote kile kikiwamo changu nitakachoanzisha hivi karibuni! sijaona discussion hapa
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa ninamaana njema kabisa kama wewe ulivyoonyesha hapo. Kayombo kuwa ni mtu wa watawala na hayupo tayari kuona wanapingwa. Muulize mgomo uliyotokea wakati yupo Njombe sekondari.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...