Ulimjuaje marehemu jasson kaishozi-wakili kesi ya zombe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimjuaje marehemu jasson kaishozi-wakili kesi ya zombe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaijabutege, Nov 16, 2010.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jasson Kaishozi nilimjua hivi:

  Shule ya Sekondari (O-Level)------------Ihungo 1982-1985
  Shule ya Sekondari (A-Level)------------Umbwe 1986-1985
  UDSM BA Ed ---------------------------------1988-1992 (Alifukuzwa na Mzee Mwinyi)
  UDSM LLB--------------------------------------1997-2000

  Jasson Kishozi alikuwa Rais wa DARUSO (Overall-Mlimani na Muhimbili) kwa kipindi cha siku tatu 6-9 Februari 1992. Alifukuzwa Chuo Kikuu na wenzake 9 ambao walisimama kidete kupinga mfumo mbovu wa uchangiaji wa gharama za elimu ya juu na kutetea uanzishwaji wa vyama vingi. Wanafunzi hao 10 walifukuzwa tarehe 10 Februari 1992.

  Waliofukuzwa tarehe hiyo ni hawa:

  1. Mh. James Mbatia (Electrical Engineering-4th year)-Mwenyekiti NCCR-Mageuzi
  2. Dr. Harun Kimaro (MD 5th year)-Marehemu (Alikuwa mshauri wa MDC Zimbabwe)
  3. Fabian Lutalemwa (Pharmarcy 4th year)
  4. Rwekamwa Rweikiza (B.com Marketing-2nd year)-Alikuwa Rais wa Daruso Mlimani siku 3.
  5. Idrissa Alnoor Ruta (Engineering Civil 4th year)-Mrehemu
  6. Ludovick Kashaju Bazigiza (BA Ed 4th year)-Marehemu
  7. Mosena Nyambabe (Engineering-Civil)
  8. Dr. Kelivin Mmari (Electrical Engineering-2nd yr)-Ni lecturer wa IT Oregon University, USA
  9. Jasson Kaishozi (BA Ed-2nd yr)-Marehemu
  10.......Kimweri (BA Economics 3rd year)-Marehemu

  Baada ya kukuzwa alikaa mtaani na baada ya miaka mitano alirudi kusoma sheria. Alipomaliza alipata kazi kwa mwanasheria mkuu wa serikali, kama wakili wa serikali.

  Kesi iliyompa umaarufu ni ile ya ZOMBE, ambapo yeye ndiye alikuwa mkuu wa jopo upande wa mashitaka (serikali).

  Wengine mlimjuaje?
   
 2. o

  omuka Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RIP jasson! Amekufa lini? Nini kimemuua?
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  R.I.P Mr. Kaishozi, tutakumbuka kama mpiganaji mahili na mwanaharakati aliyependa kusimamia haki. Kuna wakati kisukari kilimsumbua lakini hatukutegemea kama ingefikia kiwango cha kutoa uhai wake.

  Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa hiyo kesi ya Zombe si ndio walichemsha?
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Mbona kwenye hiyo list, marehemu ni wengi???
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  I remember those good old days when we were fighting for DARUSO

  R.I.P Jason Kaishozi
   
 7. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nawahaya pia ni wengi hii inamaanisha nini?
   
 8. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mapenzi ya Mungu.:bowl::bowl:
   
 9. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mapenzi ya Mungu vile vile.
   
 10. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Rip jasson
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Waitu kibao....why?...hata mtoa post waitu?
   
 12. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kusikitishwa na habari hizi mbaya za kifo cha Kaishozi, nimesikitishwa zaidi na habari kwamba mpiganaji Harun Kimaro naye ni marehemu kwa sasa. Huyu alikuwa mpiganaji wa kweli na ndiye aliyeongoza maandamano pamoja na Prof. Shaba kwenda Ikulu kuitaka serikali ifute mpango wake wa kuchangia elimu na kuwaachia madaktari wanafunzi kadhaa waliopakiwa kwenye basi moja na kudai walikuwa wanapelekwa makwao. Yalikuwa ni maadamano ya kwanza ya bila kibali cha serikali kufanyika na yakafanikiwa.

  RIP Kimaro, RIP Kaishozi.

  Tiba
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha mbali sana - wengine hapo nilikuwa nao JKT, hasa huyo James Mbatia , tulikuwa naye JKT Ruvu C-Coy , lakini yeye alikuwa "serule" na kubaki kulinda hanger.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Please mtoa hoja..kwanza tupe taarifa ya msiba. Amefariki lini huyo mpiganaji?

  RIP Jasson...Nilipata bahati ya kusimuliwa habari zake miaka ya 1985. It's really sad to loose him.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Does it matter to you?
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  It does...thank you for the reminder
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Thanks and pole sana....Wangekuwa wengi ni wakwere ungepata ujumbe gani?
   
 18. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Kifo chake nahisi ni damu ya wale vijana wanne wa Mahenge!!
   
 19. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kaishozi alikuwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Nilikutana naye kwa mara ya mwisho huko Arusha sehemu ya Mianzini ambapo alinipiga ulabu wa nguvu ingawa yeye alikunywa soda water. Akaniambia kuwa alikuwa amehamishiwa Musoma.

  Tarehe 1 Novemba 2010 nikampigia simu nikifiri yuko Musoma ili anipe habari za uchaguzi Tarime na Musoma Mjini. Kaishozi akapokea simu akiongea kwa shida sana na kuniambia yafuatayo kwa kifupi: " rafiki yangu tangia nilipoti hapa Mbeya sijawahi kukaa ofisini, hali yangu ni mbaya sana, yaani sijui nikwambieje....". Nilimuaga kwa uchungu.

  Jana saa mbili nikatumiwa message na advocate mmoja aliyesoma naye Ihungo na kunipa taarifa ya msiba wa Kaishozi. Leo asubuhi nimesoma kwenye gazeti la Tanzania Daima na kusikia kwenye taarifa ya habari ya Redio One. Bado nafuatilia mipango ya mazishi.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana mkuu,

  Nashukuru sana kwa taarifa. Ningeomba uanzishe thread nyingine au urekebishe msg yako ya kwanza ili uweze kwanza kutoa hiyo taarifa ya msiba halafu tunaweza kuchangia mengine baadaye. It's shock kumpoteza mtu muhimu kama huyu na katika umri ambao kwa kweli ndo anaanza kulitumikia taifa.
   
Loading...