Mapepo matano yanayoitesa dunia

Mapepo matano yanayoitesa dunia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,461
Reaction score
829,854
1.Pepo la uongo

2.Pepo la uzinzi

3.Pepo la pombe na madawa

4.Pepo la wizi

5.Pepo la kisasi na malipizi

Haya ndio mapepo matano makuu tunayoyaabudu na kuyasujudia kuliko hata dini na imani zetu; ni mapepo yaliyotukamata hasa. Pepo la uongo likiwa ndio kubwa lao. Hakuna ambaye si muongo, mwizi, mlevi nk, hata ukikuta mmoja hana pepo hili basi utamkuta na pepo/mapepo mengine na wengi wetu tunayatumikia kwa utiifu mkubwa kabisa lakini bila ridhaa zetu tuko chini ya himaya zao.

Chunguza maisha waishiyo watu, mambo wafanyayo nyuma ya pazia na vile wanavyojiweka mbele ya kadamnasi utashangaa mno. Tuna watu ambao hawapitwi na Chupi wala suruali, kuna watu ambao bila kupata japo tusker baridi hawawezi kupata usingizi, tuna watu ambao wana mali nyingi tu lakini ameshazoea kuiba, yeye asipoiba anakosa amani kabisa, anaiba hata visivyoibika.

Kuna wale ambao wasipodanganya wanaugua kabisa, anadangaya familia, kazini, mtaani kwa jioni boss wake yeye anadangaya tu. Ni pepo sio yeye.

Haya yote yameleta matatizo makubwa kabisa tuliyonayo duniani kwa sasa. Visasi na malipizi vimeleta vita visivyoisha, ngono, wizi na ulevi vimeleta matatizo si haba.

Cha kushangaza ni kwamba ukiacha pombe labda na sigara wengi wetu hatuko tayari kuyasema waziwazi mapepo yetu.
 
Hivi ni pepo au mashetani? Peponi si ndio huko mbinguni au?
 
Hivi ni pepo au mashetani? Peponi si ndio huko mbinguni au?

Shetani ana makao na ni ukoo mmoja na ibilisi na mapepo
Peponi ni mahali kama Tanzania nk, pepo ni dubwana in the sense of conscious energy that can lure your life whatever it want or in any way
 
Mshana umenena,kuna watu huwa wananishangaza sana,wao huwa wanaona kuwa dhambi ni kunywa pombe tu labda na wizi na uzinzi,kumbe hapo kuna msongamano wa mambo,nashukuru umegusa penyewe,kwa heshima yako naomba uongezee pepo jingine la-Kutowajibika(hapa anzia kwa mtu mmoja mmoja,jamii na viongozi wetu kwenye mataasisi ni uozo).
 
Mkuu naona J/pili ilikuwa swadakita kwako.

Tunahitaji msaada wa Mungu 100%.
 
Mshana umenena,kuna watu huwa wananishangaza sana,wao huwa wanaona kuwa dhambi ni kunywa pombe tu labda na wizi na uzinzi,kumbe hapo kuna msongamano wa mambo,nashukuru umegusa penyewe,kwa heshima yako naomba uongezee pepo jingine la-Kutowajibika(hapa anzia kwa mtu mmoja mmoja,jamii na viongozi wetu kwenye mataasisi ni uozo).

Haya mapepo matano ndio yanatengeneza ukoo mzima wa hao wote ukichanganya na husuda,choyo, majivuno,uzandiki ma mambo yote yafananayo na hayo
 
1.Pepo la uongo
2.Pepo la uzinzi
3.Pepo la pombe na madawa
4.Pepo la wizi
5.Pepo la kisasi na malipizi
Haya ndio mapepo matano makuu tynayoyaabudu na kuyasujudia kuliko hata dini na imani zetu, ni mapepo yaliyotukamata hasa. Pepo la uongo likiwa ndio kubwa lao
Hakuna ambaye si muongo, mwizi?mlevi nk , hata ukikuta mmoja hana pepo hili basi utamkuta na pepo/mapepo mengine na wengi wetu tunayatumikia kwa utiifu mkubwa kabisa lakini bila ridhaa zetu tuko chini ya himaya zao
Chunguza maisha waishiyo watu mambo wafanyayo nyuma ya pazia na vile wanavyojiweka mbele ya kadamnasi utashangaa mno tuna watu ambao hawapitwi na Chupi wala suruali kuna watu ambao bila kupata japo tusker baridi hawawezi kupata usingizi, tuna watu ambao wana mali nyingi tu lakini ameshazoea kuiba yeye asipoiba anakosa amani kabisa, anaiba hata visivyoibika
Kuna wale ambao wasipodanganya wanaugua kabisa anadangaya familia kazini mtaani kwa jioni boss wake yeye anadangaya tu ni pepo sio yeye
Haya yote yameleta matatizo makubwa kabisa tuliyonayo duniani kwasasa visasi na malipizi vimeleta vita visivyoisha, ngono wizi na ulevi vimeleta matatizo si haba
Cha kushangaza ni kwamba ukiacha pombe labda na sigara wengi wetu hatuko tayari kuyasema waziwazi mapepo yetu

Wagalatia hili ndio lilikuwa somo la leo !?
 
Na pasipo msaada wa Mungu, hatuwezi kushinda. Hebu fikiria, hata kama shetani asingekuwa na uwezo upitao ule tulio nao binadamu, lakini katika uzoefu, ni zaidi ya uzoefu. Hebu fikiria, alidanganya wangapi wazini, waibe, waue, wamuasi Mungu kabla sijazaliwa, na tena unakuta, wengine aliowadanganya, kabla ya hapo walikuwa ni watu mashuhuri kwa habari za Mungu (mfano Yuda Iskariote hadi alitoa mapepo na kuponya wagonjwa). Tunapigana na nguvu zilizo juu yetu, hivyo pasipo kutafuta nguvu ya ziada (Kutoka kwa Yesu Kristo) hatuwezi kushinda, yeye alishinda(Yesu) ili na sisi tushinde.
 
Halafu watu wanaona Ni sifa kuwa hivo
 
Mi nahisi yote hayo yanachangiwa na Pepo moja kuu ambalo ni TAMAA...ukiwa na tamaa utakuwa muongo, mwizi, mzinzi na mengne ya kufanana na hayo...!!
 
logframes
Wana pepo la usongombingo unaotokana na husuda, wivu, kijicho na mtindio wa fikra!
 
Last edited by a moderator:
1.Pepo la uongo

2.Pepo la uzinzi

3.Pepo la pombe na madawa

4.Pepo la wizi

5.Pepo la kisasi na malipizi

Haya ndio mapepo matano makuu tunayoyaabudu na kuyasujudia kuliko hata dini na imani zetu; ni mapepo yaliyotukamata hasa. Pepo la uongo likiwa ndio kubwa lao. Hakuna ambaye si muongo, mwizi, mlevi nk, hata ukikuta mmoja hana pepo hili basi utamkuta na pepo/mapepo mengine na wengi wetu tunayatumikia kwa utiifu mkubwa kabisa lakini bila ridhaa zetu tuko chini ya himaya zao.

Chunguza maisha waishiyo watu, mambo wafanyayo nyuma ya pazia na vile wanavyojiweka mbele ya kadamnasi utashangaa mno. Tuna watu ambao hawapitwi na Chupi wala suruali, kuna watu ambao bila kupata japo tusker baridi hawawezi kupata usingizi, tuna watu ambao wana mali nyingi tu lakini ameshazoea kuiba, yeye asipoiba anakosa amani kabisa, anaiba hata visivyoibika.

Kuna wale ambao wasipodanganya wanaugua kabisa, anadangaya familia, kazini, mtaani kwa jioni boss wake yeye anadangaya tu. Ni pepo sio yeye.

Haya yote yameleta matatizo makubwa kabisa tuliyonayo duniani kwa sasa. Visasi na malipizi vimeleta vita visivyoisha, ngono, wizi na ulevi vimeleta matatizo si haba.

Cha kushangaza ni kwamba ukiacha pombe labda na sigara wengi wetu hatuko tayari kuyasema waziwazi mapepo yetu.

Daaah namba 2&1 vinanihusu sana... Mkuu ungemalizia kbs amri kuu 10 za Mungu......... Ngoja nimrudie Mungu kabla sijaangusha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom