Mapenzi yanauma jamani

Dah. Mkuu kama wewe aisee. Mimi siku 5 zimepita. Sema mi nikaona isiwe shida nikaanzisha Mawasiliano na msamaha nikaomba mimi ingawa sio kosa langu.

Mwisho wa siku we only live once. Maisha mafupi.
sio kama usipoandika ndio utaonekana mwamba .
Linapokuja swala la mapenzi sisi sote ni wamoja tu.
Napita kwenye situation kama yako mzee
Tumepishana muda tu
Me naenda wiki ya pili hi
Teh teh Wakurungwa poleni
 
Kuna muda nataman anitafute aniombe msamaha yaishe!! ila ndo hivo kanilia buyu
 
Ujue nashindwa kuomba msamaha kwasababu hata sijakosa mm!! Unaombaje msamaha na huna makosa
Karibu kwenye ulimwengu wa mapenzi ambapo kuomba msamaha sio lazima umekosea.

Unaweza kuta meseji kwenye simu,na bado ukaomba msamaha kwa kumpekua bila ruhusa yake.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
hivi mnapataga wapi ujasiri wa kulia kisa mpenzi aloo?? Mimi mpenzi wangu sio kufumania nilipigiwa simu na bwana ake mwingine tukaonana na mchizi akanipa na uthibitisho ni demu wake akampigia simu demu anasema siwezi kukusaliti naanzaje kitu iko loud speaker halafu nilikua nampenda kinyama sijawahi penda kiasi kile.

Yani niliumia sana ila nikamwambia mchizi bro endelea nae mimi tangu leo simtaki na sikulia ingawa nilipata stress kama wiki halafu akanitafuta akaniomba msamaha si alikua anajua nampenda sana so siwezi chomoa wee nilimfurahisha, alinikumbatia na maneno mengi ooh kumbuka ulinifuatilia mwezi mzima , kumbuka siku ya kwanza nimekukubali tukahug na kiss mimi uso mbuzi.

Nikamwambia sikia nakupenda sana na unajua lakini mimi na wewe haitakaa itokee tena achia tu kuwa wapenzi hata kupasha kiporo hutakaa unione naked maisha yako yote hakuamini nikasepa hapo moyo unadunda kama speaker za kitambaa cheupe ikaisha hivyo mpaka leo miaka 7 sasa rafiki zangu tu huwa hawaamini kama nilimkataa maana walijua nampenda sana mpaka kesho wanasemaga sniper una roho ngumu sana bro kama yule mwanamke umeweza kumuacha hatujui nani atakaa akusumbue.

Acheni udhaifu sometimes kumuacha unaempenda huwa ni kitu bora inauma yes but tunasahau msiba mpenzi kitu gani.
 
Relaaaaaax ukijikaza sana sindano itavunjika
 
Ujue nashindwa kuomba msamaha kwasababu hata sijakosa mm!! Unaombaje msamaha na huna makosa
Jiongeze kaka,Omba msamaha ili mrudiane alaf tafuta mpenz taratibu alaf ndo uje umuache wewe
 
Ukiwa mzembe kihisia hivi hakuna mwanamke atakulewa. Unakuwaje mzembe hivi?! Ina maana kichwa chako kinawaza mapenzi badala ya maisha sasa mwanamke gani atakuhitaji wewe?!

Ninyi ndio mnajinyongaga

Mwanadamu yeyote anaumia
 
Ndugu zangu mapenzi ni shida sana, kila mtu na kilio chake
..
 
Bahati mbaya siku hizi wanawake wengi hawajali mapenzi wapo busy na ngono hivyo hawana hisia na hawaumii. Jaribu kusikiliza tungo nyingi za siku hizi za vijana utaona hilo. Pole
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…