My Experience
Na declare interest huyu baby mama wangu ninampenda sana. Mwanzoni wa uhusiano wetu tulikuwa tukizinguana hata kama yeye ndio mwenye makosa nilikuwa naomba msamaha mimi. Yeye kuomba msahama ni mzito kweli.
Basi Mungu sio athumani akapata ujauzito. Kama kumjali ndio nilizidisha mara 100. Yaan hapa sikutaka hata kugombana naye kabisa kidogo tu nisamehe hivyo.
Mtoto kazaliwa copy yangu. Ila sijui inatokea nini mwanamke akipata mtoto wako, kibao kimegeuka yaan kwanza hata kama nimezingua na najua nimezingua nakaza yeye ndio anaomba msamaha. Naomba msamaha pale tu ninapoamua kuomba msamaha. Nimemjengea kuwa nampenda ila akizingua tu naweza sepa vilevile.