Watu wote wenye wapenzi wasio wake/waume wao wa halali ni sawa tu na wacheza mpira waviziaji, mara nyingi wakikamata mpira wafunge kipenga huwa kinapulizwa wameotea hata kama keshafunga goli, mimi pia ni mviziaji kama kina inzaghi, nina toto langu rembo tu ila bado lipo kwao, baada ya wazazi wake kusafiri kwenda kijijini basi tukapanga mikakati ya kuupokea mwaka mpya, kuwa tutaenda out kujirusha na mambo mengi tu na zaidi ya yote tutalala wote kuigiza maisha ya mke na mme. Cha kusikitisha leo mapema asubuhi wazazi wake wameingia ghafla toka kijijini tofauti na mipango ya awali ambapo walipanga kurudi tarehe 5 mwakani, mipango yote tuliyopanga imeyeyuka kabisa.