GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,277
- 6,673
Ni asubuhi ya Ijumaa Tar. 2/09/2011. Rafiki yangu kaniita Tabata
Anasema ana mazungumzo na mimi. Ninapofika nyumbani kwake
Simkuti, namkuta mkewe naye anajiandaa kuondoka, anamsindikiza
Jirani yake Hospitalini MUHIMBILI. Ninashawishika kuongozana nao.
Najiunga kwenye safari hii nikiwa sijui uhusiano wa mgonjwa na jirani
wa mwenyeji wangu, ni kukosa kazi ya kufanya ndiko kunakonipa
msukumo wa kutembelea wagonjwa Muhimbili. Safari inachelewa
hatimaye tunaondoka saa 10 Alasiri.
Ili kuutumia Muda wangu vizuri naamua kutembelea
Wagonjwa kwenye Wodi mbalimbali. Kweli hospitali
ni sehemu ambayo inaweza kukufanya utafakari upya
mambo mbalimbali.
Nachukua Lift hadi Ghorofa ya Tatu. Naelekea Wadi
No. 24 katika jengo hili la SEWA HAJI ni wadi hii
Ndiyo iliyonipa uchungu na kunifanya nije huku
MMU kujadili na wenzangu. Nimefika kitanda no.
(8 no 10) Juu kuna karatasi imeandikwa no 10 chini
Kuna maandishi ya ukutani no.8, nashindwa kuelewa
Kama kitanda hiki ni no.8 au 10. Hapa nakutana na
Wahida Mwalim Binti wa miaka 11(Kumi na mmoja)
Namsogelea ana majeraha ambayo yanatoa harufu
Mbaya. Ninapouliza kilichomsibu naambiwa ni waya
Wa umeme wa Tanesco ule mkubwa sijui mnauitaje
Kitaalamu ni ule umeme ambao haujafika kwenye
Transfoma, ule waya ulikatika ukamgonga mkononi
Maskini……. Binti mikono yote imeoza na anatakiwa
Kukatwa mikono. Bado hajakatwa, madaktari ‘wanazingua'
Binti anaendelea kuoza pale kitandani, labda ni taratibu za
Kazi zinawataka wasubirie siku kadhaa sijui………
Anazidi kuumia, Tanesco wametoa kipunguza uchungu
cha Tsh 500,000/=
ninapofikiria haya nalazimika kuingia jukwaani na kuwauliza
wenzangu, Hivi tunapozungumzia Mapenzi, mahusiano na
Urafiki tunafikiria kwa upana kiasi hiki. Tunajua kuwa hujafa
Hujaumbika? Kama ni hivyo napenda niwashauri ndg zangu
Tujenge utamaduni wa kwenda kuangalia wagonjwa na kujua
Matatizo yao. Kama tunashindwa kuwahurumia wenzetu
Ambao wengine wamening'iniza miguu yao vitandani n.k
Basi hata sisi hatustahili kuhurumiwa. Si huko tu! Pia si vibaya
Tukajenga utamaduni wa kutembelea tukajenga utamaduni wa
Kutembelea watoto wasio na makazi maalum na kujua matatizo
Yao kule sokoni Kariakoo n.k Tukirudi huko na kupeana taarifa
Na kushauriana namna ya kutatua nafikiri MMU litakuwa
miongoni mwa majukwaa bora kabisa.
NAWASILISHA
Anasema ana mazungumzo na mimi. Ninapofika nyumbani kwake
Simkuti, namkuta mkewe naye anajiandaa kuondoka, anamsindikiza
Jirani yake Hospitalini MUHIMBILI. Ninashawishika kuongozana nao.
Najiunga kwenye safari hii nikiwa sijui uhusiano wa mgonjwa na jirani
wa mwenyeji wangu, ni kukosa kazi ya kufanya ndiko kunakonipa
msukumo wa kutembelea wagonjwa Muhimbili. Safari inachelewa
hatimaye tunaondoka saa 10 Alasiri.
NDANI YA MOI (MUHIMBILI ORTHOPEDICS INSTITUTE)
Tumefika SEWA haji bahati mgonjwa karuhusiwa.