Mapenzi ni huruma!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,671
Ni asubuhi ya Ijumaa Tar. 2/09/2011. Rafiki yangu kaniita Tabata
Anasema ana mazungumzo na mimi. Ninapofika nyumbani kwake
Simkuti, namkuta mkewe naye anajiandaa kuondoka, anamsindikiza
Jirani yake Hospitalini MUHIMBILI. Ninashawishika kuongozana nao.
Najiunga kwenye safari hii nikiwa sijui uhusiano wa mgonjwa na jirani
wa mwenyeji wangu, ni kukosa kazi ya kufanya ndiko kunakonipa
msukumo wa kutembelea wagonjwa Muhimbili. Safari inachelewa
hatimaye tunaondoka saa 10 Alasiri.

NDANI YA MOI (MUHIMBILI ORTHOPEDICS INSTITUTE)


Tumefika SEWA haji bahati mgonjwa karuhusiwa.
Ili kuutumia Muda wangu vizuri naamua kutembelea
Wagonjwa kwenye Wodi mbalimbali. Kweli hospitali
ni sehemu ambayo inaweza kukufanya utafakari upya
mambo mbalimbali.

Nachukua Lift hadi Ghorofa ya Tatu. Naelekea Wadi
No. 24 katika jengo hili la SEWA HAJI ni wadi hii
Ndiyo iliyonipa uchungu na kunifanya nije huku
MMU kujadili na wenzangu. Nimefika kitanda no.
(8 no 10) Juu kuna karatasi imeandikwa no 10 chini
Kuna maandishi ya ukutani no.8, nashindwa kuelewa
Kama kitanda hiki ni no.8 au 10. Hapa nakutana na
Wahida Mwalim Binti wa miaka 11(Kumi na mmoja)

Namsogelea ana majeraha ambayo yanatoa harufu
Mbaya. Ninapouliza kilichomsibu naambiwa ni waya
Wa umeme wa Tanesco ule mkubwa sijui mnauitaje
Kitaalamu ni ule umeme ambao haujafika kwenye
Transfoma, ule waya ulikatika ukamgonga mkononi
Maskini……. Binti mikono yote imeoza na anatakiwa
Kukatwa mikono. Bado hajakatwa, madaktari ‘wanazingua'
Binti anaendelea kuoza pale kitandani, labda ni taratibu za
Kazi zinawataka wasubirie siku kadhaa sijui………
Anazidi kuumia, Tanesco wametoa kipunguza uchungu
cha Tsh 500,000/=

ninapofikiria haya nalazimika kuingia jukwaani na kuwauliza
wenzangu, Hivi tunapozungumzia Mapenzi, mahusiano na
Urafiki tunafikiria kwa upana kiasi hiki. Tunajua kuwa hujafa
Hujaumbika? Kama ni hivyo napenda niwashauri ndg zangu
Tujenge utamaduni wa kwenda kuangalia wagonjwa na kujua
Matatizo yao. Kama tunashindwa kuwahurumia wenzetu
Ambao wengine wamening'iniza miguu yao vitandani n.k
Basi hata sisi hatustahili kuhurumiwa. Si huko tu! Pia si vibaya
Tukajenga utamaduni wa kutembelea tukajenga utamaduni wa
Kutembelea watoto wasio na makazi maalum na kujua matatizo
Yao kule sokoni Kariakoo n.k Tukirudi huko na kupeana taarifa
Na kushauriana namna ya kutatua nafikiri MMU litakuwa
miongoni mwa majukwaa bora kabisa.

NAWASILISHA
 
Kaka unalosema ni kweli kabisa. Watu wanashida sana hasa mahospitalini ni balaa tuu. Kama kweli tukiwa na moyo wakutembelea na kuwafariji nazani tunaweza songa mbele kaka. Hila mm nionavyo hapa tz tumekuwa wabinafsi sana hadi inakuwa hali nimbaya sana. Wewe angalia tu kwann hawa watu wanapangiana mishahara mikubwa sana mil7 hadi mil14 wakati kuna mwalimu anakamata laki2 hadi laki3, kunamwingine anahata kipato nakapata tatizo kweli kunakupona hapo?
Namuomba sana mungu atubariki watz tuache ubinafsi hili tuweze songa mbele. Nasema kama atuta acha ubinafsi kamwe atutasonga mbele hata tukibadilisha uongozi wanchi.

nawakilisha nami
 
Kwa ujumla hayo ni maisha ya watz wengi sana! Tunajisahau tu tunapopata access za ku brouse kama hivi, tunaojadiliana humu maisha wengi tuna maisha ya wastani ndio maana tunajisaha na kufikiri maisha ndio haya kwa kila mtz! Maisha ya ndugu zetu ni shida sana! Hata huyo ni bahati tu yupo dar angalau Tanesco wametoa.
Kuhusu member wa jf kujitolea kuwasaidia, nadhani wengi wanafanya but individually. Nadiani unafahamu wengi humu hawapendi kufahamiana kwa sababu mbalimbali ingawa tofauti ni kubwa kwa Arusha. Tungeweza kujiunga kwa pa1 na kulifanya hilo kwa pa1 lingeleta maana kubwa sana!
 
tatizo na huku mtaani tuna shida sana, tunauguliwa na ndugu marafiki, pesa nazo ni issue ndio maana unaona hivo mkuu
lakini pia sio kwamba htutembelei sehemu hizo tunatembelea sana tu kila tupatapo nafasi..ahsante sana
 
Ok,kwanza nikupongeze kwa hicho ulichokiibua. Watanzania wengu huruma yetu na misaada ni ya kukopeshana na kuaazimana,
kwani misaada mingi huenda kwa watu ambao wanauwezo wa kurudisha,maslani angalia watu wanapochangia vikao vya harusi,
tafrija nyingine kuliko kusaiadia wahitaji kama vile wagonjwa,wajane,yatima na wahanga wengine. Pia uwajibikaji cku hizi haupo
watu wanajali sana pesa kuliko utu, hasa secta hiyo utakufa unaangaliwa kama hauna kitu.
 
Nakupongeza kaka. Höngera sana. Nashukuru kwa ushauri wako.
 
Kwa ujumla hayo ni maisha ya watz wengi sana! Tunajisahau tu tunapopata access za ku brouse kama hivi, tunaojadiliana humu maisha wengi tuna maisha ya wastani ndio maana tunajisaha na kufikiri maisha ndio haya kwa kila mtz! Maisha ya ndugu zetu ni shida sana! Hata huyo ni bahati tu yupo dar angalau Tanesco wametoa.
Kuhusu member wa jf kujitolea kuwasaidia, nadhani wengi wanafanya but individually. Nadiani unafahamu wengi humu hawapendi kufahamiana kwa sababu mbalimbali ingawa tofauti ni kubwa kwa Arusha. Tungeweza kujiunga kwa pa1 na kulifanya hilo kwa pa1 lingeleta maana kubwa sana!
Lakini Mkuu, hao wanaotoa Individually wengi wao hutoa kwa watu
wanaowafahamu tu! Si watanzania wengi wenye utamaduni wa
Kutembelea wagonjwa, mara nyingi mtu mpaka asikie kuwa ni
jirani au ndugu yake na wakati mwingine hutokea mtu akaenda
kwa kuogopa kulaumiwa.
 
tatizo na huku mtaani tuna shida sana, tunauguliwa na ndugu marafiki, pesa nazo ni issue ndio maana unaona hivo mkuu
lakini pia sio kwamba htutembelei sehemu hizo tunatembelea sana tu kila tupatapo nafasi..ahsante sana
Watu hutembelea tu wanaposikia kuna mtu wanamfahamu
mara nyingi ni watu wa dini ndio nimeona wanatembelea
wagonjwa!
 
uislamu unaelekeza haya yote ya kutendeana wema ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa kwani inatukumbusha uwepo wa Mungu Muumba, na kila mara kujikuta ukirudi njia iliyo ya kheri hata pale unapokuwa unatetereka kiimani. pia inakumbumbusha kuwa sie viumbe hatuna mamlaka juu ya miili yetu na maisha kwa ujumla isipokuwa Mwenyezi pekee! Kweli Gazeti, tukifuata hayo tutakuwa ni watu wema na tutaogopa kutenda ubaya kwa wengine hivyo kufanya dunia mahali salama pa kuishi...Big up kwa Thread nzuri
 
sad story. ntaufanyia kazi kaka kwani mda mwingi tukitoka job tunawaza kuwahi bar na familia hatuwazi wagonjwa na wahitaji.jms nako tunatumia mafuta mengi kwenda club za mbali kustarehe lkn muhimbili tunaipita kwa mbali na huko tuendako tunatumia hela nyingi ambazo zingasaidia kuokoa maisha ya wahitaji.,MUNGU atusamehe.
 
kaka ulicho andika ni ukweli wala haupingiki Mungu azidi kukujalia na pia hata sisi azidi kututumia kuona wagonjwa na wenye shinda mbalimbali na kuweza kuwa saidia hujafa hujaumbika Mungu ndiye mtoa ridhiki tusaidie na wengine
 
Back
Top Bottom