Mapenzi Na Mafanikio Ya Mwanamke

Wakuu...

siku za karibuni nimeona rafiki zangu wawili wakivunja ndoa zao baada ya kutoswa na wake zao, hao wadada ni wa shoka, elimu A, na kazi walizopata ni za kimataifa

Cha kushangaza mmoja wao hakuwahi kuwa na issue na mkewe zaidi ya kuburuzwa kwenye maamuzi tangu mama amalize PhD yake; sasa nimesikia mama kapata kazi nje ya nchi, kaondoka bila kumuaga jamaa na amepeleka watoto wote boarding na jamaa hajui afuate njia ipi

Sasa najiuliza, hivi kuna uhusiano kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa??? Nafahamu humu ndani kuna matawi yote na nategemea msaada maana mie nasomesha mke na nimeshaanza kuogopa

Please advice

Sidhani kama tatizo ni kusomesha mke; bali ni nini hasa kinachotembea kichwani mwake mnapojenga uhusiano wa mapenzi na hata kuoana. Nafikiri mke wa kukukimbia utamfahamu hata kabla hajaongezekewa na elimu au kipato.

Tatizo wengi wetu hupata wenza (mke/girlfriend) kwa kutumia kivutio cha ukwasi na/au wadhfa mkubwa hata kama ni illusion tu. Mke wa aina hiyo values zake zinakuwa finyu sana; atakuwa anakupima wewe na watu wengine kwa vitu hivyo hivyo tu. Akipata ufunuo mpya (elimu zaidi) na soko kubwa zaidi, basi wewe unakuwa na thamani ndogo sana kwake.

Na ikitokea uelewa wako (kielimu) ni mdogo zaidi na yeye sasa ndio yuko katika kiwango cha kuchangia mada na "maprofesa" na "vigogo" wengine, basi umeliwa.
icon10.gif

Nafikiri somo kubwa kwa mwanaume ni kujiamini na kujijengea uwezo (kisaikolojia) wa kukabiliana na mabadiliko yoyote ya maisha. Ukikimbiwa na mke mwenye mtazamo finyu, thank God; it's GOOD RIDDANCE! Tena huenda huko mbele ya njia akajuta kurahisisha maisha na kujikuta akitafuta njia ya kurudi (baada ya kupata "elimu dunia").

By the way, mimi mwenyewe nasomesha mke digrii ya kwanza na huwa na-enjoy sana kuona excitement yake tunapopata muda wa kujadili dhana na njia mbalimbali za kutatua mafumbo katika masomo yake. Atanikimbia au la? Hainiumizi kichwa sana.
icon12.gif
 
wengi wa wanawake ni sawa na mbuni. Wanatamani kupaa ila hawana uwezo. Wakipewa mabawa ya bandia wanapaa hadi karibu na jua. Jua linawayeyusha na kuwachoma. Wanaanguka. Haki sawa isiwapande kichwani kama malaria
 
Mtume Sauli-Paulo hakuwa mjinga kusema MUME ampende mke wake lakini MKE amheshimu mume wake. Wanawake hawana mkitu mapenzi wao maslahi zaidi na ndio maana Saini ya Firstlady inajinadi "2010 NIPO KIKAZI ZAIDI".
 
Wakuu...

siku za karibuni nimeona rafiki zangu wawili wakivunja ndoa zao baada ya kutoswa na wake zao, hao wadada ni wa shoka, elimu A, na kazi walizopata ni za kimataifa

Cha kushangaza mmoja wao hakuwahi kuwa na issue na mkewe zaidi ya kuburuzwa kwenye maamuzi tangu mama amalize PhD yake; sasa nimesikia mama kapata kazi nje ya nchi, kaondoka bila kumuaga jamaa na amepeleka watoto wote boarding na jamaa hajui afuate njia ipi

Sasa najiuliza, hivi kuna uhusiano kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa??? Nafahamu humu ndani kuna matawi yote na nategemea msaada maana mie nasomesha mke na nimeshaanza kuogopa

Please advice
Hakuna lolote mfumo dume tu unawasumbua
 
Sidhani kama tatizo ni kusomesha mke; bali ni nini hasa kinachotembea kichwani mwake mnapojenga uhusiano wa mapenzi na hata kuoana. Nafikiri mke wa kukukimbia utamfahamu hata kabla hajaongezekewa na elimu au kipato.

Tatizo wengi wetu hupata wenza (mke/girlfriend) kwa kutumia kivutio cha ukwasi na/au wadhfa mkubwa hata kama ni illusion tu. Mke wa aina hiyo values zake zinakuwa finyu sana; atakuwa anakupima wewe na watu wengine kwa vitu hivyo hivyo tu. Akipata ufunuo mpya (elimu zaidi) na soko kubwa zaidi, basi wewe unakuwa na thamani ndogo sana kwake.

Na ikitokea uelewa wako (kielimu) ni mdogo zaidi na yeye sasa ndio yuko katika kiwango cha kuchangia mada na "maprofesa" na "vigogo" wengine, basi umeliwa.
icon10.gif

Nafikiri somo kubwa kwa mwanaume ni kujiamini na kujijengea uwezo (kisaikolojia) wa kukabiliana na mabadiliko yoyote ya maisha. Ukikimbiwa na mke mwenye mtazamo finyu, thank God; it's GOOD RIDDANCE! Tena huenda huko mbele ya njia akajuta kurahisisha maisha na kujikuta akitafuta njia ya kurudi (baada ya kupata "elimu dunia").

By the way, mimi mwenyewe nasomesha mke digrii ya kwanza na huwa na-enjoy sana kuona excitement yake tunapopata muda wa kujadili dhana na njia mbalimbali za kutatua mafumbo katika masomo yake. Atanikimbia au la? Hainiumizi kichwa sana.
icon12.gif

Thanks Drifter... i think it all depends on several factors and complexity of the relationship as time goes by!!!

Kuna mama mmoja ni kibosile sana tu na jamaa kawa kama dereva wake lakini they really portray a very good image kwa watu wengine jinsi walivyo tight, ila sijui sasa huko ndani inakuaje
 
wengi wa wanawake ni sawa na mbuni. Wanatamani kupaa ila hawana uwezo. Wakipewa mabawa ya bandia wanapaa hadi karibu na jua. Jua linawayeyusha na kuwachoma. Wanaanguka. Haki sawa isiwapande kichwani kama malaria

Mh... umekuwa mkali
 
sio kweli wajameni, hiyo ni tabia ya mtu tu, mbona mie nimesomeshwa mpaka phD, wakati jamaa ni fprm four lkn heshima nampa zote mpaka jamaa haamini
 
Ukimfanya mwenzio mtumwa wako kwa sababu ya pesa, madaraka, sura nzuri au elimu, siku anapata uhuru lazima atoke akafurahie uhuru wake. Hii ni kwa wote wanaume na wanawake. Sasa hivi kinachotokea ni kuwa ile tabia wanaume walikuwa wanafanyia wake zao kuwatosa wakishapata madaraka na pesa, sasa imegeuka, wanawake wanafanyia waume zao wakipata hizo rasilimali
 
Hamna uhusiano kabisa kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa. Hii huwa individual attributes. Inawezekana wale wenye mafanikio hawana uvumilivu kwenye ndoa au they will not put a facade. Kuna wengine wanabaki tu kwenye ndoa lkn hawana raha kabisaaaa. Huyo mwanamke mwenye mafanikio anatoka maana ana stability ya kujitegemea.

Point nyingine ni kwamba mafanikio na elimu hayana uhusiano kabisa na Emotional Intelligence. Wengi wana I.Q lkn nafahamu alot of them huwa wanascore za chini kwenye E.I, ambayo ni muhimu sana kwenye relationships.

Kuna akina dada nawafahamu wamesoma kweli si mchezo na wana kazi nzuri na happy in marriages, because they also have E.I ya juu.

Sometimes ndoa inavunjika tu maana mtu mmoja anadevelop inferiority complex kwa sababu ya mafanikio ya wife...

Nakumbuka I was once told by a male friend - Divorce does not make you a failure, it just did not work. Does it make you a bad person? No...You are given a second chance to do it right.
 
kiasili, wanawake hupenda kutawaliwa. watanipinga ila wajue kwenye subconscious mind zao hili lipo. sasa inapotokea ombwe la utawala, basi yeye ataliziba kwa namna anavyoona yeye. mwanamke hapendi kuwa chini ya mwanaume 'dhaifu'. kwa lugha nyingine, mwanaume aliyezidiwa uwezo na mwanamke kwa maana kiasili mwanaume yuko juu ya mwanamke. anachukia bila kujua kuwa ni kwa nini mwanaume yuko chini yake kiuwezo? inaposhindikana kuwa na yule amtakaye atakuwa na huyo wa awali kwa shingo upande. ila hapa si wote walio hivyo bali ni asilimia kubwa!
 
Mwanamke anapenda kulindwa na siyo kutawaliwa! Tofautishwa hivi vitu viwili. Kwenye bold ya pili umefafanua vyema.
MARA NYINGI MWANAUME asiyejiamini hulazimisha kutawala badala ya kulinda na kuongoza maana anajua sifa za uongozi hana na hawezi kutoa ulinzi pia.
 
sawa, kulindwa, ila hiyo 'dhaifu' ina maana yake kwa mtazamo wa kike. naweza kuwa na shahada moja na mke wangu akawa nazo mbili akaniona dhaifu. mwanaume hujiamini na kumsomesha mkewe/mwenza ila mwisho wa siku huwa hayo. hata kama mwanaume umemzidi kielimu na kifedha mruhusu basi akulinde kivingine. apewe nafasi yake kama baba/kichwa
 
Hamna uhusiano kabisa kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa. Hii huwa individual attributes. Inawezekana wale wenye mafanikio hawana uvumilivu kwenye ndoa au they will not put a facade. Kuna wengine wanabaki tu kwenye ndoa lkn hawana raha kabisaaaa. Huyo mwanamke mwenye mafanikio anatoka maana ana stability ya kujitegemea.

Point nyingine ni kwamba mafanikio na elimu hayana uhusiano kabisa na Emotional Intelligence. Wengi wana I.Q lkn nafahamu alot of them huwa wanascore za chini kwenye E.I, ambayo ni muhimu sana kwenye relationships.

Kuna akina dada nawafahamu wamesoma kweli si mchezo na wana kazi nzuri na happy in marriages, because they also have E.I ya juu.

Sometimes ndoa inavunjika tu maana mtu mmoja anadevelop inferiority complex kwa sababu ya mafanikio ya wife...

Nakumbuka I was once told by a male friend - Divorce does not make you a failure, it just did not work. Does it make you a bad person? No...You are given a second chance to do it right.

This is a very good advice/observation, na ndio haswa nilikuwa nataka kujifunza kutoka kwa hii mada... mara nyingi sisi wanaume tumekuwa tuki-assume vitu vinavyowatatiza wenzetu au sisi wenyewe.

I think it is ok to say that marriage is such a complicated institution that no written rules or regulation or even expectations/responsibilities could apply to everyone!!
 
Leo nimesikia habari ya kusikitisha jamaa amemuoa mke wake wa ndoa wameishi miaka 12 kwa kosa la mwanamke kutembea au kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa jamaa. Baada ya kumua nae akajipiga kisu. Imetokea huko Moshi jamani inasikitisha.
 
In anyway, mwanamke asome atakavyo, lakini asimzidi mume!

Akikuzidi madarasa tu, umeuawa, nina mifano mingi sana ya incidence hizi!..Wanakuwa uncontrollable, kelele mingi and so on!, na anakuwa free kukudanganya kuwa anaenda safari kikazi, kumbe wapi!

Ni asilimia 10 ya wanawake ambao watabaki kuwa waaminifu wapatapo mafanikio kielimu!

pakajimmy hebu tuwie radhi kwanza! alaaa! unataka wanawke wenye phd wasiolewe au?
mie kwa nafsi yangu nna phd na mume ndo kanza anamaliza degree yake ya kwanza na sijawahi kumsikia akilalama kuwa namletea dharau ya aina yoyote ile.
mikwaruzano mengine ya kawaida ipo...........ila i repeate kuwa haisababishwi na mwanamke kumzidi elimu au pesa mwanamme.
ni hulka tu
 
kingi umeongea pointi nzuri kuwa wanawake wanapenda Kulindwa.
wengi wanapenda mwanamme ndo awe kichwa cha ndoa, kutoa maamuzi mazito, pamoja na responibilities nyengine.
mwanamke anapoona huyu hawezi kunilinda ndipo inapotokea tatizo.
wengine wanastahamili na kubaki kwenye ndoa japo hawaoni raha, na wengine ( labda waliosoma ndio wengi hapa) wanaona bora waondoke wakatafute raha sehemu nyengne.
 
Haya mambo yapo Pande zote mbili. Tatizo linalojitokeza hapo ni mabadiriko ya maisha na umbali unaowatanganisha wapenzi hawa. Pamoja na sababu hizi hulka ya mtu ndiyo msingi mkubwa wa kudumisha mapenzi.
 
Nawapa big up sana wachangiaji... once again, it sjustify kwamba love/relationship ni complex engagement that has no formulae
 
Haya Mkuu De Novo,baada ya kupata michango mizuri ya members sasa ni wakati wa burudani.Pata kitu hapa chini.....

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=9I1d29RsKGQ"]http://www.youtube.com/watch?v=9I1d29RsKGQ[/ame]
 
Back
Top Bottom