SoC01 Mapenzi Kinyume na Maumbile ni hatari, usijirahisishe

Stories of Change - 2021 Competition

Madam chopra

Member
Jul 27, 2021
5
46
Habari yako,

Kwa wakazi wa Bongo, neno Shivaz sio geni masikioni mwenu! Manka Mushi mie, mtoto wa kichaga huko na Mrina ndiyo yalikuwa machimbo yangu ya kujidai. Kiufupi nimeumbika, shepu mashallah! Msambwanda asilia nimejaliwa sio wezere la kuvalia kigodoro yaan nina kila kigezo cha kuitwa pisikali.

Wengi walizoea kuniita Mamaa wa Fastafasta kwasababu nilikuwa sichagui sura, rika au umbile zaidi ya kuangalia shilingi na nilikuwa siachi ela nyuma. Mimi ni mchaga halisi na mjini nimekuja kutafuta hela.

Siku moja niliotea danga la kishua, mtu na heshima zake! Mtu na hela zake! Mtu mzito! Tena kijana handsome, mbaya zaidi ni mume wa mtu! Walahi kama ni zali la mentali siku hiyo lilinidondokea. Mara baada ya makubaliano nikampatia huduma akanipa changu. Sikuamini nilichokiona, yaani nusu saa napewa bonge la burunduti na business card juu. Wacha we! Nikajiona nimepata nikampa overtime, kwani shi ngapi? Hapo akaniona namfaa akaongeza dau ili nitulie nae kwa siku kadhaa kwani alikuwa amekuja Arusha kikazi. Kwangu haikuwa shida kwasababu kiasi tulichokubaliana kwa siku ni zaidi ya madanga wa wiki nzima. Manka nikasema "yes I am here for you". Nikajituliza nae kwa siku alizohitaji, huwezi kuamini nilifungua akaunti nikaanza kuhifadhi fedha benki, apo natoka na msomi lazima anipeleke kisomi. Niligeuka dadapoa wa kishua kwa muda lakini siwafichi na kamwe sitokuja kusahau vitendo nilivyokuwa navifanya mpaka kupandishwa dau lote lile.

Yaan jamaa pamoja na hadhi yake hakupendelea huduma kwa muundo mtakatifu, alipenda kufanya kinyume na utaratibu tulioumbiwa wanawake. Na mamaa fastafasta kwa tamaa ya pesa! Ukicheki nina malengo ya kumjengea mwanangu niliyemzaa na simjui baba mtoto, nikajiambia kimoyomoyo "pesa hiyo kubali acha uzembe!" Nikamwambia mbele ya pesa hakuna linaloshindikana...... Nikajitutumua, nikakubali kuingiliwa kinyume na maumbile kwa mara ya kwanza, maumivu makali niliyoyapitia nilitamani kukimbia lakini kwa ufinyu wa akili nikavumilia baada ya muda kidogo nikaanza kuzoea. Ilikuwa kazi na dozi, kazi na dozi, mbele tembea, nyuma geuka, hatimaye nikabobea!

Mwisho wa siku jamaa akaniacha na kujichukulia sistaduu mwingine wa palepale viwanja! Nilijikuta naumia kihisia lakini nikapotezea maana nilishamisi kutangatanga na watu tofautitofauti.

Akili yangu ya kijinga ikawa imepanuka nikaanza kujinadi kivingine. Huduma asilia bei ya kawaida, ukitaka kinyume na utaratibu unaongeza dau. Nikapata wateja kama wote........ Hapo nimeshaanza ujenzi kwenye kiwanja nilichonunua kwa kubana boom langu la chuo kwa miaka mitatu kabla sijahitimu na kujiunga na genge la masista duu mguu juu. (Kutokutaka kufanya kazi ndogo ndogo zisizo za kisomi baada ya kukosa ajira ndio kulifanya nitake mteremko mpaka kubeba mimba iliyogomaga kutoka).
Ujenzi ulianza na kwakuwa nina kiwanja nikakiweka rehani na kukopa benki, biashara si imekua uhakika tena nagombaniwa maana natoa huduma mbadala. Kweli pesa nilipata na rejesho mwanzoni halikunisumbua.

Haukupita muda mrefu, hali ikabadilika, ule mtetemente niliokuwa naringia ukawa mzigo kwangu. Huwezi kuamini haja kubwa ikawa inatoka bila kunipa muda wa maandalizi, nikichelewa tu hiyoooo..... Nikaamua kuvaa nepi (pampas) za wakubwa na ilikuwa siri yangu, hakuna niliyemweleza lakini cha moto nilikiona , hali ile ilinikera sana. Siku si nyingi nikaanza kuwa mtu anayenuka harufu haziekeweki, madonda yalinitoka ikawa ni mimi na kijikuna, kujikuna na mimi mpaka na mwendo ulibadilika. Biashara ya kujiuza imesimama, ujasiri wa kutoka kukutana na wadau nautoa wapi? Benki nimekopa, rejesho nimekwama, uwiii na kajumba nilichoanza ujenzi hakajaisha na ndio nimeweka rehani hilo eneo. Nikahisi kuchanganyikiwa Ila sikuwa na la kufanya. Baada ya muda nikashuhudia nyumba iliyoniponza ikiuzwa mbele ya macho yangu tena nikiwa sina chochote na nimeanza kudhoofu.

Mungu si Athumani, majirani wakanigundua na kuripoti kwa ndugu zangu, nikasaidiwa na kupelekwa hospitali kupata matibabu, baada ya muda mrefu ndio nikapona kiasi walau nikaanza kuweza kuzuia haja kubwa na mfumo ukarudi sawa. Ndugu wakachanga fedha nikapatiwa mtaji nifanye biashara halali. "Woooi, yaan mimi niteseke na biashara ili nigundue nini? Huo ushamba ndio siwezi! Nakula ikiisha ntajua pa kuanzia" nilijiambia kimoyomoyo.

Sikio la kufa halisikii dawa, baada ya kujiona niko sawa nikaanza kudanga mitaa mingine na nilirudi kivingine, Danga moja kwa siku lilikuwa linanitosha kabisa. Lengo ni lilelile niweze kununua kiwanja na kujenga. Safari hii sikuwa na pupa na sijasahau yaliyonisibu nilijiapiza kutokurudia makosa, danga moja kwa adabu narudi nyumbani nalala fofofo, kesho nayo ni siku.
Kama ni hela nilipata si haba!

Ila jumapili moja nilipokuwa nimejipumzisha nyumbani nilipopanga, nikiperuzi na kutupia picha za mitego mitandaoni ndipo nikakutana na kurasa ya Jamii Forums nikasoma mada mbalimbali na maoni ya wachangiaji nikajifunza mambo mengi ambayo yaliikuna na kuizindua akili yangu. Nikaendelea kuperuzi nikaona kurasa nyingine inayoelimisha kuhusu saratani nikajikuta nimevutiwa kuikagua. Katika kukaguakagua nilijifunza mambo kama vile; SILAHA YA KUISHINDA SARATANI NI KUIGUNDUA MAPEMA, SI KILA UVIMBE NI SARATANI, SARATANI IKIGUNDULIKA MAPEMA INATIBIKA (mfano saratani ya matiti, ya mlango wa kizazi n.k), SARATANI YA INI HUWEZA KUSABABISHWA KWA KUSHIRIKI NGONO ZEMBE pamoja na sababu nyingine walizozitaja. Nilijifunza mengi kuhusu saratani ya koo na fangasi ( nikafikiria ukafiri wa ngono za mdomoni madadapoa tunavyozishiriki tuwapo mwezini (Hedhi) nami nikiwa mmoja wao! Astakafiri! Nilirudia kusoma, nikakodoa macho kuhakikisha nilichokisoma, nikarudia tena kisha nikaendelea kusoma " MADHARA YA KUJAMIANA KINYUME NA MAUMBILE"

Kwanza, kupata UTI sugu, hii hutokea baada ya kiingiliwa kinyume alafu mwanaume akafanya kitendo hicho kwa njia ya kawaida, bakteria waishio sehemu hiyo huleta madhara makubwa ukeni.

Pili, kutokwa na haja kubwa bila kizuizi, hatari zaidi ni wakati wa kujifungua, changamoto ya kutokwa na haja kubwa mfululizo wakati wa kusukuma mtoto hupelekea misuli kulegea na kumbana hadi kuweza kupelekea kifo kwa mtoto.

Tatu, Kupata magonjwa ya zinaa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi. Mchezo huu wanafanyiwa wanawake na wanaume tena wengi hawatumii kinga jambo linalohatarisha afya.

Nne, Huweza kusababisha saratani ya utumbo mpana, sehemu ya haja kubwa, uume, mlango wa kizazi na huchangia kwa asilimia kadhaa kupata homa ya ini.

Tano, Kupata msongo wa mawazo kutokana na aibu pamoja na majuto ya tendo hilo.

Sita, kwa anayeugua bawasiri atapata maumivu makali sana na kuvuja damu nyingi huko nyuma. Madhara ni mengi mno Ila haya ni baadhi ya niliyojifinza siku hiyo. Inasisitizwa tujiepushe na kukimbia ushawishi wa hili tendo na tujiongeze kupata elimu na kusambaza elimu juu ya madhara ya kujamiana kinyume na maumbile.

Binadamu hujamiana kwa mwingiliano wa uume kupitia ukeni vinginevyo ni ubatili mtupu"
Niliinama na ghafla machozi yalianza kunitoka ila kwa roho ngumu nilivyokuwa nayo nilijipiga makofi manne mfululizo kisha nikameza mate kwa nguvu na kuikamata simu yangu kwa umakini, kisha nikapangusa machozi na kuanza kugoogle kuhusu niliyoyasoma. Niliperuzi na kupitia mijadala mingi kujifunza zaidi kuhusu madhara ya tabia na matendo yangu. Sio kama nilikuwa sijui kabisa, ufahamu nilikua nao ila ni kujichetua na kupuuza mambo. Siku hiyo ilikuwa siku ya ukombozi wangu, akili ilizinduka, nililia sana, nilijidharau, nilijuta na kujilaumu kwa niliyoyafanya. Kweli nilijuta na tokea siku hiyo niliapa kuachana na uozo huo. Niliuza utu wangu sana sasa yatosha.

Nikajikaza kisabuni na kufanya kitendo cha kishujaa, nilitoa nguo zote za ajabuajabu na kuzichoma moto. Nilishindwa kustahimili maumivu ya ushenzi wangu, nilipasua chupa mbili za bia zilizokuwa kwenye friji, nikajikuta nimekanyaga kipande cha chupa na kuumia mguu lakini sikujali, nililia kwa maumivu sio ya kukatwa na chupa ila maumivu ya kinyaa na kujiona mwenye ushenzi na uchafu, nililia mpaka nilipopitiwa na usingizi.

Asubuhi kulipokucha ndio ulikuwa mwanzo mpya wa maisha yangu. Nilifanya maamuzi ya kijasiri na kiasi nilichokuwa nacho ndio ulikuwa mtaji wa kuanza biashara. Nilimtafuta rafiki yangu Rozina ambaye tulihitimu naye chuo akawa anajishughulisha na kuuza vitafunwa sokoni mpaka akamiliki mgahawa wa hadhi ya juu ili anipe elimu ya ujasiriamali. Hakusita kunishauri japo alishanikatia tamaa, kwanza alinipongeza kwa uamuzi ninaotaka kuuchukua na alinisihi niwe mvumilivu, nisiogope maneno ya watu (hapa kuna wale wanasemaga nakusoma kote unauza sokoni!! Wapuuze! Na kujiuza kote hujaambulia kitu!! Wapuuze!) Pia nisitake kujikweza, niishi maisha halisi na kupambana kama mwanamke jasiri. Ushauri wake niliufanyia kazi, nikaanza kwa kuagiza mchele kutoka Mbeya nakuja kuuza Arusha, nilianza na gunia la kilo mia na nikaagiza mafuta ya alizeti singida nikaanza kuuza. Sikumuangalia mtu usoni! Nilipambana hasa, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa hatimaye nikafungua duka.

Ni miaka miwili imepita, kwasasa ninaendesha maisha yangu kwa biashara ya kuuza nafaka, nina salooni ya kike ya kisasa nimeajiri mabinti watatu, pia ninaendesha kampeni ya kutetea haki, utu na usawa.

Hakika maisha ni matamu, niko huru, najiamini na kuheshimika tena nimegeuka mfano wa kuigwa mtaani ninapoishi, binti akianza tabia za wavulana utasikia anaambiwa "uhuni hauna maana, Manka amehangaika sasaivi amebadilika tulia soma utayakuta na kuyaacha".

Maisha yanaweza kubadilika ukiamua! Nikitembea najisikia raha pale ninapoona MANKA MUSHI BEAUTY SALOON! MANKA MUSHI SHOP AND STORE! Ni raha asikuambie mtu.

Kujiuza ni biashara haramu, inadhalilisha utu! Mwanamke unageuzwa dampo kila mtu anamwaga anachotaka. Baada ya kuona andiko hili, ninaomba kila mmoja awe balozi wa kushauri wanawake na mabinti wanaopotea, mtu akizinduka kifikra akawa timamu hawezi kuuza utu wake ata kama ana hali ngumu kiasi gani. Na nyie wavulana, kina kaka, wababa na wababu tulieni nyinyi ni wa thamani msile kila kinachojiuza mtakula mizoga, unajisikiaje kula chawote, kuweni na kinyaa! Baba mtu mzima unanunua binti, fikiria huyo ni kama binti yako (mtoto wa mwenzako ni wako). Wanawake tushauriane, tukanyane, ukiuza ni siri yako ila tambua umegeuzwa kifanyio!! Kifanyio mbele tembea, nyuma geuka!! Chacharika kazi halali zipo ni uvumilivu tu.

Tusaidiane, tushauriane, utu upewe kipaumbele!
 
Manka sasa una Mume? Hongera kwa Kukombolewa.

Ila hiki ni kizazi cha kujaribu na kujiridhisha hivyo hutaeleweka ni mpaka kijaribu na chenyewe kijionee hali halisi ila wewe umenawa tayari.
 
Ujumbe umefika..... Ila hapo kwenye kuchukua mkopo bank umetupiga..... Ulichukua mkopo bank kwa kuonesha biashara gani?
 
Back
Top Bottom