Mapendekezo ya CHADEMA juu ya Miswada ya Sheria za Uchaguzi ambayo Kamati ya Bunge inazuia yasisomwe Bungeni

Jadili vitu kama mtu mzima na kutoa ushauri na hoja kama mtu uliye pevuka kifikra na kimawazo na siyo kuandika vitu na kuzungumza kama vijana waliozibuka akili na kukosa malezi bora ya wazazi wao. Ukubwa wa umri ni pamoja na kuonyesha uongozi katika kila jambo ikiwepo katika ujenzi wa hoja na kujadili hoja.siyo kuandika maneno ya kwenye kanga na vijiwe vya wavuta bangi.
Ulitangaza wewe mwenyewe na namba ya Simu ukaweka!
 
Mimi ni mlipa kodi na ninapinga mapendekezo ya kihayawani na kijinga yaliyotolewa na CHADEMA yanayotaka kutuongezea gharama za kuwahudumia wabunge badala ya kupeleka kwenye miradi ya maendeleo itakayo leta tija kwa wananchi

Mwaka huu umelipa bei gani, unatisha watu hapa? Unavuta pumzi bure ukijipendekeza ulipe kodi wewe?
 
Kama tunasoma vyuo vilevile bila kujali vyama vya siasa tunavyotoka, kwanini CHADEMA wawe na timu inayoweza kufanya uchambuzi wa kina na usio na upendeleo (biasness) kwa kiwango hiki?
Kweli wewe una matatizo kichwani. Kwa hiyo mawazo na maoni ya CHADEMA kuwa kwa kila jimbo kuwe na wabunge wawili ndio unaona mawazo bora? Huoni inaongeza gharama na mzigo kwa wananchi? Kwa hiyo kama kuna majimbo 250 unataka bungeni waingie wabunge miatano? Hapo bado viti maalumu walivyopendekeza vya 30% .una akili kweli wewe kuunga mkono ujinga huu? Unajitambua kweli wewe? Kwa hiyo mapato na makusanyo yote unataka yaelekezwe kuwalipa wabunge tu? Halafu pesa za maendeleo zitatoka wapi?
 
Mwaka huu umelipa bei gani, unatisha watu hapa? Unavuta pumzi bure ukijipendekeza ulipe kodi wewe?
Ujinga na mapendekezo ya kijinga ya CHADEMA kuhusu kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo pamoja na 30% ya wabunge viti maalumu hayawezi kuungwa na wenye akili Timamu. Labda yataungwa na akina Johnthebaptist anayewaunga mkono CHADEMA
 
Umekurupuka Kaka, hizo enzi zimepita.Angalia namna nyingine ya kuishi, mapema kabla uzee haujakuelemea.Kama mambo ni magumu sana, nenda ukawe hata CHAWA wa Mwijaku inaweza kuwa na tija kwako kuliko hii ligi unayoitamani.
Sasa umeandika nini hapa? Ukisoma ulichoandika unaweza kukielewa kweli?
 
Jibu swali eqe mmawia .niambie kuna sababu gani na umuhimu upi kwa utafiti upi mpaka jimbo moja liwe na wabunge wawili? Kwanini CHADEMA wanataka kuongeza gharama na mzigo kwa mlipa kodi? Je ndio maendeleo hayo?
Mngekuwa mnaogopa gharama msingepitisha malipo ya wenza wa wastaafu.
 
Ndivyo alivyosema Mnyika? Kwamba anataka wabunge wawili katika kila jimbo la Uchaguzi,mmoja mwanaume na mmoja mwanamke; na kwamba yule mwanaume awe kapogiwa kura na wanaume,; na yule mwanamke awe kapigiwa kura na wanawake? Ha ha ha.

Nadhani system ya sasa ndio nzuri.

Kura zinapigwa bila kutazama gender ya mtu.

Kama unataka wanawake wawepo bungeni unaweza kuwapa seat za upendeleo.
Mkuu kweli kasema hivyo?
Duh kweli hii nchi haitoboi. mzigo wa wabunge zaidi ya 300 hautoshi wanataka sasa wafike 600?
 
Mkuu kweli kasema hivyo?
Duh kweli hii nchi haitoboi. mzigo wa wabunge zaidi ya 300 hautoshi wanataka sasa wafike 600?
Ndio kasema hivyo katika hoja yao namba tano. Na siyo kuwa wanaweza kuwa wabunge mia sita bali watazidi hapo maana bado na wa viti maalumu ambao nao wamependekeza wawepo ndani ya bunge
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimesoma mapendekezo ya CHADEMA yaliyowasilishwa mbele ya kamati ya Bunge neno kwa neno, msitari kwa msitari na kifungu kwa kifungu.nimesoma kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa kuwa mimi siyo mvivu katika kusoma na huwezi ukanificha jambo kwa kuliweka kwenye maandishi kwa matarajio kwamba sitasoma.

Hii ni kwa kuwa mimi ni mtu ninayependelea sana kusoma hasa vitu vilivyoandikwa kwa urefu sana ndio huwa napenda kuvisoma kwa utulivu ili kujuwa kilicho ndani yake.ndio maana napenda kusoma sana na kusikiliza vyema kilicho andikwa na kinachozungumzwa na mtu hata kama ni hotuba ndefu kiasi gani.

Ili andiko langu lisiwe refu sana basi Leo nitawapitisha katika hoja namba tano inayohusu aina ya wabunge na hoja namba nane inayohusu muundo wa tume na mapendekezo waliyopendekeza CHADEMA.

Ndugu zangu Watanzania imenisikitisha sana tena sana kunihuzunisha, kunishangaza, kuniduwaza, kunisononesha,kunipa mawazo, kunistajaabisha, kunipa maswali yasiyo koma niliposoma mapendekezo ya CHADEMA katika aina ya wabunge katika hoja yao namba tano.

Kwamba sasa CHADEMA wanapendekeza kuwa katika kila jimbo kuwe na wabunge wawili wawili watakaochaguliwa na wananchi kwa kufuata jinsia na makundi, yaani kutakuwa na mgombea mwanamke na mwanaume katika kila jimbo la uchaguzi ambapo mwanaume atapigiwa kura na wanaume tu na mwanamke naye atapigiwa kura na wanawake wenzake. halafu hapo hapo mwisho wa siku baada ya kumaliza uchaguzi mkuu CHADEMA wanataka na kupendekeza tena kuwe na wabunge wa viti maalum wasiopungua 30% ndani ya bunge letu.

Pia kwanini kuwe na viti maalumu tena wakati tayari mmeshapendekeza na kutaka kuwa kila jimbo lazima awepo mwanamke? Sasa hao viti maalum wanaingia kufanya nini tena bungeni? Kwani nini yalikuwa madhumuni ya kuanzisha viti maalumu? Si yalikuwa ni kuleta usawa wa kijinsia? Sasa kama mmependekeza kuwepo mwanamke kila jimbo halafu unataka tena viti maalum vya nini ? Hivi CHADEMA mna akili kweli ninyi?

Hivi nani aliyependekeza ujinga huu ndani ya CHADEMA? Kwa faida ya nani? Kwa jasho la nani ? Kwanini CHADEMA wanataka kutubebesha mzigo Watanzania walipa kodi? Kwanini wanaangalia maslahi yao na matumbo yao na kutusahau wananchi walipa kodi? Kwanini wanataka pesa zote na makusanyo yote ya nchi yaelekezwe katika kulipa mishahara na marupurupu ya wabunge? Kwanini tuache kufanya maendeleo na tujikite katika kulipa mishahara na kuwalea na kuwatunza wabunge kwa jasho letu? Yaani badala ya kufikiri namna ya kupunguza gharama wao wanaongeza gharama? Yaani jimbo liwe na wabunge wawili ? Halafu tena baadaye mpewe tena viti maalumu?

Hivi kwanini ninyi CHADEMA mbatupatia saba hasira na kichefuchefu Watanzania? Kwanini mnatia kinyaa? Hivi kama hamna hoja kwa nini msikae kimya? Hivi huu ndio ujinga na uhayawani mliokuwa mmekalia siku zote mnaujadili kwa ajili ya maslahi ya mimatumbo yenu kuijaza? Tutakuja kula kwenye matumbo yenu? Mtatuwekea bomba la chakula kutoka kwenye matumbo yenu? Yaani sisi tuhenyeke halafu ninyi mnataka kujiwekea uchochoro wa kutafuna pesa za nchi? Mna akili kweli ninyi?

Kwamba tuwe na wabunge wengi kuliko hata uingereza? Nani kasema na kwa hoja ipi na kwa utafiti upi na kwa ushahidi upi na kwa mifano ya wapi na kwa misingi ipi na kwa vigezo vipi na kwa namna gani? wingi wa wabunge katika jimbo moja kunachochea maendeleo katika jimbo? na vipi mbunge mmoja hawezi kuleta maendeleo katika jimbo mpaka wawe wawili? Kwa nini pesa za kumhudumia mbunge wa pili kuanzia mshahara,pesa ya usafiri au gari,posho za kikao,safari,kamati,kiinua mgongo zisipelekwe katika jimbo husika kuchochea maendeleo ya wananchi?

Kwanza kwanini mnataka mlete ubaguzi katika kupiga kura? Kwa kuwa pendekezo lenyewe ni la kibaguzi tu.utaanzaje kusema kila jinsia impigie mtu wa jinsia yake? Siyo ubaguzi huu? Siyo kuvunja umoja, mshikamano, upendo na nguvu katika majimbo na hatimaye Taifa zima kwa ujumla wake na hivyo kuzorotesha maendeleo katika majimbo na Taifa zima kwa ujumla wake?

Kwanini mnakuwa walafi sana na wenye uchu wa madaraka ninyi CHADEMA? Kwanini siku zote mnajifikiria matumbo yenu na familia zenu pekee? Mmegikiria kuwaza maisha ya watanzania na vipato vyao? Mngewaza maisha ya watanzania mngeanzia wapi kupendekeza ujinga wa namna hiyo?

Kwa hakika mlaaniwe kabisa ninyi mliokosa akili za kutambua maisha ya watanzania na vipato vyao na uzalendo kwa Taifa letu .Mungu awaalaani na kuwapiga upofu katika kila kitu. Nawaombea mpigwe pigo kama la 2020 msiwepo kabisa Bungeni ,maana hamna faida yoyote ile zaidi ya kujali matumbo yenu na maslahi yenu na kuja kuleta vivuli mtaani mkishavimbwiwa kodi zetu kama ambavyo mmekuwa mkitutukana kama alivyo fanya Godbless Lema kwa kusema kazi ya bodaboda ni ya laana.

Nitaendelea kuchambua hoja namba nane katika uzi mwingine.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
🚮
 
Ndio kasema hivyo katika hoja yao namba tano. Na siyo kuwa wanaweza kuwa wabunge mia sita bali watazidi hapo maana bado na wa viti maalumu ambao nao wamependekeza wawepo ndani ya bunge
Duh ama kweli hii nchi iko doomed. Badala ya vyama pinzani wawaze kupunguza mzigo kwa serikali kwanza hata viti maalum wangeondoa huo upuuzi. Nchi hii hadi sasa mishahara na posho za uendeshaji ni kubwa mno. Sasa wanataka waongeze wabunge kwani hilo linamsaidiaje mtanzania
 
Duh ama kweli hii nchi iko doomed. Badala ya vyama pinzani wawaze kupunguza mzigo kwa serikali kwanza hata viti maalum wangeondia huo upuuzi. Nchi hii hadi sasa mishahara na posho za uendeshaji ni kubwa mno. Sasa wanataka waongeze wabunge kwani hilo linamsaidiaje mtanzania
Wao wanachoangalia na kuzingatia ni maslahi ya matumbo yao tu na siyo kuona uchungu na kumuonea huruma mtanzania anayelipa kodi. Kwanini mapesa yote ya kumhudumia mbunge wa pili yasipelekwe kwenye jimbo husika kufanyia maendeleo?
 
Jibu swali eqe mmawia .niambie kuna sababu gani na umuhimu upi kwa utafiti upi mpaka jimbo moja liwe na wabunge wawili? Kwanini CHADEMA wanataka kuongeza gharama na mzigo kwa mlipa kodi? Je ndio maendeleo hayo?
Umeliona hilo? Leo hii kuna umuhimu gani wa serikali ya ccm kuwa na DED na DC wilaya moja?

Wote wanakuwa na magari ya kifahari huoni kuwa ni ifujaji wa rasilimali za taifa?

Wacha kujiondoa akili kwa sababu ya kulazimisha uteuzi
 
Binafsi sijaona hoja hata moja yenye maana dhidi ya Mapendekezo ya CHADEMA! Naona ni malalamiko yanayotokana na athari za Chademaphobia tu!
 
Back
Top Bottom