Mapendekezo kwa Rais Samia: Namna ya Kulimaliza Suala la Bandari kisiasa

Kimalingano

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
422
525
Mimi nikiwa Kada wa dhati wa CCM namshauri Mheshimiwa Rais afanye mambo yafuatayo kulimaliza jambo hili kisiasa;

1. Awatumbue Mhe.Waziri wa Ujenzi,Katibu Mkuu wa Ujenzi,Mkurugenzi wa TPA na wengine wote waliohusika kumshauri vibaya kuhusiana na jambo hili.

2. Ahutubie Taifa akieleza jinsi alivyoshauriwa vibaya.

3. Atafutwe muwekezaji mwingine wa kuboresha bandari na asiwe DP World.

Bila kufanya hivi kelele zitaendelea ambazo nyingi ni za upotoshaji.Bahati mbaya watanzania wengi ni wepesi kuamini porojo na uzushi zaidi ya mambo ya kweli.

Ni rahisi kwa mtanzania kuamini kuwa matatizo yake ya njaa,ufukara nk yanasababishwa na DPW badala ya ukweli kuwa ni uvivu wake.
 
Sawa,lakini si ndiyo wanaowajibika kumshauri Rais.Wengine wanaweza kuwa ni lobists tu ambao wanachochea kimya kimya.
Kwenye bandari hao ulio wataja sio washauri ila kinafasi zao inaonekana kama washauri.. Kwanza kama Rais alale mbele na baraza lake lote
 
Kutumbuliwa, sidhani kama ni rahisi. Labda kuwatoa wizara hiyo na kuwapeleka wizara nyingine. Fuatilia historia.

Ujue hao uliowataja, wanatoka Zanzibar.
 
hii issue ya DP world imeshika kasi kuzidi moto wa petrol,watanzania wanaamini bandari imeuzwa 😃 hilo ndio lilowajaa moyoni huu ufafanuzi unaotolewa na serikali sijui kupitia clubhouse sio wote wanaofuatilia na kujua wao wanachojua hii kitu ya dp ni BATILI.

INAHITAJIKA NGUVU YA ZIADA KUWATOA KATIKA MLENGO HUO
 
Mimi nikiwa Kada wa dhati wa CCM namshauri Mheshimiwa Rais afanye mambo yafuatayo kulimaliza jambo hili kisiasa;

1. Awatumbue Mhe.Waziri wa Ujenzi,Katibu Mkuu wa Ujenzi,Mkurugenzi wa TPA na wengine wote waliohusika kumshauri vibaya kuhusiana na jambo hili,

2. Ahutubie Taifa akieleza jinsi alivyoshauriwa vibaya,

3. Atafutwe muwekezaji mwingine wa kuboresha bandari na asiwe DP World.

Bila kufanya hivi kelele zitaendelea ambazo nyingi ni za upotoshaji.Bahati mbaya watanzania wengi ni wepesi kuamini porojo na uzushi zaidi ya mambo ya kweli.

Ni rahisi kwa mtanzania kuamini kuwa matatizo yake ya njaa,ufukara nk yanasababishwa na DPW badala ya ukweli kuwa ni uvivu wake.
Kushauriwa vibaya ni excuse ya uongo. Raisi ni mtu timamu kiakili na mwili
 
“ Bila kufanya hivi kelele zitaendelea ambazo nyingi ni za upotoshaji.Bahati mbaya watanzania wengi ni wepesi kuamini porojo na uzushi zaidi ya mambo ya kweli.”

Yawezekana unaufahamu, lieleze Jamvi. Ili huo upotoshaji ufutike.

“Ni rahisi kwa mtanzania kuamini kuwa matatizo yake ya njaa,ufukara nk yanasababishwa na DPW badala ya ukweli kuwa ni uvivu wake.”

Ni vema ukatuheshimu Watanzania.
 
Upotoshaji upi sasa?

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
hii issue ya DP world imeshika kasi kuzidi moto wa petrol,watanzania wanaamini bandari imeuzwa 😃 hilo ndio lilowajaa moyoni huu ufafanuzi unaotolewa na serikali sijui kupitia clubhouse sio wote wanaofuatilia na kujua wao wanachojua hii kitu ya dp ni BATILI.

INAHITAJIKA NGUVU YA ZIADA KUWATOA KATIKA MLENGO HUO
Hebu nisaidie majibu ya hizi hoja...

Back
Top Bottom