Maoni yenu tafadhali....

Maoni yenu tafadhali....

Smile my dear, its just happened mpnz, hata mm nilikuwa nawish ivo but ndo imeshakuwa ivyo.
ok my dear mchukue tu huyo mdogo wako ila akupe shikamoo yako kila siku asubuhi
 
huyo mtu wala hana tatzo na umri wako ila huko kujishuku kwako ndo utaanza kufanya hilo swala kuwa issue n believe or not ukipata mkubwa mwenzio utamuacha huyo mtu ws watu, yamenikuta hayo nilitafutiwa sababu tu kisa mtu hakuwa secured na umri wangu
 
Inaonekana umeshapata mwingine so unatafuta sababu ya kumtema!acha kumpotezea muda mwenzio
 
mwaka mmoja sio inshu kikubwa mnaishi kwa aman na upendo,ila angalia mwenyewe na ufanye uamuz
 
Bibie Nyamagembe, pole kwa yanayokutatiza na hongera hata kwa kuwa naye huyo ambaye wewe unamuona ni bwana mdogo wako.
Kiukweli wanawake wengi wangependa kuwa na wanaume/wapenzi wanaowazidi (ki-umri, kimo, ki-elimu, kipato etc), kinyume chake na wanaume wengi wangependa kuwa na wake/wapenzi ambao wako chini yao kwa mambo hayo hayo.
Siku hizi huko bongo ndo inazidi kuwa mbaya zaidi maana mtu kabla ya kujiangalia yeye mwenyewe na mpenzi wake anaangalia marafiki wa baa au saluni watamuonaje!
Na wewe unasumbuliwa na hiyo unwritten rule/law ya kutaka kuzidiwa. Lakini katika mahusiano kitu cha kwanza ni upendo na kukubali kukabili mapungufu yenu.
Hakuna mtu ambaye ni mkamilifu hivyo hata ambao unadhani wana wanaume/wapenzi ambao ni kama baba zao bado kuna mambo ambayo wanakubali tu kuchukuliana nayo.
Mambo ya kufanya wewe na mpenzi wako:

  1. Kaa chini mdefine uhusiano wenu ni kwa ajili ya nini?

  • Kama ni kuoana swala la umri sio issue labda kama ninyi mtaamua kulifanya liwe issue (Victoria anamzidi David Bhekam mwaka mmoja wameishi pamoja zaidi ya ten yrs na wana watoto wanne sasa)
  • Kama ni kwa ajili ya kufanyiana maonyesho tu, achana nae maana shoga zako wakijua tu wataanza kukuambia ‘nawewe nini ndio maana upo na Serengeti boy, ila wao wataweka na ‘s’.

  1. Mtu ambaye kweli ni mpenzi wako, ni muhimu kuwa huru kwake, tafuta njia mpaka nae ajue umri wako, sio kwa kueleza moja kwa moja- ila siwezi kuweka mipaka maana sijui mnaelewana kiasi gani, na wala sina haja y kukufundisha kupenda. Ukiona bado unaogopa eti atakuacha, basi jua tu umeachika hata kabla hujaona wala kusikia. (aonavyo mtu moyoni mwake ndivyo alivyo)
  2. Kama saikolojia yako haitokubaliana na umri wa huyo jamaa basi, usiendeleze uhusiano kabisa, maana kama mtu haumkubali, akikosea kuna siku utamwambia utoto unakusumbua.
Hitimisho

  • Choko mchokoe pweza binadamu katu – pamoja na niliyosema, inaelekea jamaa umemchoka sasa unatafuta njia ya kutokea, ndio maana hujui huyo jamaa unamzidi mwaka 1 au miwili, (soma uzi wako tena)
  • Mapenzi ni kufarahi, kama unaona wewe mwenyewe huwezi kufurahia mtu ambaye ni mdogo kwako kwa sababu umejengeka hivyo kisaikolojia, then hata yeye hutomfurahisha, piga chini as soon as possible
  • Pale Ilala Boma kuna kambi ya wazee, kachague kababu kamoja ili roho yako iridhike, maana mkataa pema…….
  • Usiwe kama Anna mwenye Makinda, akili ya kuambiwa tia na yako.
Ushauri
Siku nyingine ukiandika funguka zaidi, hasa kuelezea hatma ya mapenzi yenu ni nini (kugegedana tu au ndoa).
 
Back
Top Bottom