Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
wadau, hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la viongozi wa dini kuachana na kazi za kiroho na kuingia kwenye siasa. Hilo si tatizo kwani inaruhusiwa kwa mujibu wa katiba tuliyonayo. hata hivyo, pamoja na katiba kutoa mwanya huo, wengi wao wamekuwa wakitumia mwanya huo kutoa upendelea kwa wafuasi wa dini yao au kutumia majukwaa yao ya kisiasa kuponda au kukandamiza imani ya dini nyingine.
Ile dhana ya usichanganye dini na siasa inapotea. pia watu hawa ambao ni viongozi wa kiroho au waliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika jumuiya za kiroho wamekuwa wakitumika na viongozi wa dini au madhehebu yao kukandamiza dini nyingine au kutengeneza mipango michafu ili viongozi wa kisiasa dini au dhehebu jingine waonekane kuwa hawafai au wanatoa upendeleo kwa dini yao.
Kutokana na mkanganyiko huu, ni maoni yangu kuwa viongozi wa kiroho au waliowahi kuwa viongozi wa kiroho pamoja na jumuiya zake wasiruhusiwe kugombea nafasi za kisiasa kwa vile hawataweza kutenganisha nafasi zao za kiroho na za kisiasa. ni hayo tu wakuu kwa leo