Maoni yangu katika rasimu ya katiba 2013: viongozi na waliokuwa viongozi wa dini wasiwe wagombea

mkuu, waache viongozi wa kiroho wamtumikie Mungu na wanasiasa wafanye siasa
Mbona kilio chenyewe tunakisikia sasa hivi ambapo viongozi wa Kiislamu nao kutokana na rasimu mpya wanaweza kuingia bungeni kama wagombea binafsi?!

Ulikuwa wapi wakati kina Msigwa,Lwakatare na wengineo wakiingia bungeni?
 
dah. Nafikiri hujaelewa mantiki. Kila kitu unafikiria uchadema na uccm tu. Tunachotakiwa kufanya ni kuweka msingi imara ambao tanzania tutaendelea kuishi kama dugu moja. Wakati ule viongozi wa kidini walipojitenga na siasa, hatukuwa na malumbano makubwa ya kidini katika taifa. Ila baada ya hawa wanadini kujiingiza kwenye siasa ndotabia ya kunyoosheana vidole na kutoleana matamko imeanza

Basi pendekeza wapagani tu ndio wagombeee uongozi nchi hii.Elewa udini ni hulka na inaweza kuingizwa na yeyote mwenye mrengo huo, ukitaka kuelewa zaidi msikilize shehe mkuu wa Dar mitazamo yake kunapotokea mikanganyiko ya kidini husimamia ukweli na haki.Viongozi type hiyo wanaweza kuongoza jamii mchanganyiko na kutoa haki bila upendeleo kwa dini yake.Suala lililopo nchini ni product ya mambo mengi ikiwepo kutowajibika,kutofuata sheria na taratibu,kulindana n.k yote hayo kwa ujumla wake yameleta hicho unachokiogopa.Tungekuwa ma uwajibikaji yeyote anaeleta hiyo migawanyiko sheria ingenyoosha.Na watu wangfuata dira ya taifa,sasa kila mtu anafanya lake kutokana na mfano unaooneshwa na viongozi.
 
Mazindu umeongea vema,ila mtoa mada nimegundua ni kati ya wale wenye kupewa ujira 7000 Lumumba ndio maana anasimamia kucha msuala tata tangu asubuhi!msameheni bure.Kuzuia viongozi wa dini kuwa viongozi wa siasa ni kuliondoa taifa mikononi mwa Mungu na hili gharama yake ni kubwa!

nani kakwambia? Kwakua amepita mtakatifu nyerere sasa unataka aje na mtakatifu padri slaa? Hapana haiwezekani.
 
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria za nchi;
(b) ni mwenye akili timamu;
(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha
siasa au mgombea huru;
(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa
Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;

(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa;
(j) mwenendo wake binafsi hautiliwi shaka na jamii;
(k) hajatiwa hatiani kwa kosa lolote la jinailinalohusu kukosa
uaminifu; na
(l) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi
Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa
kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

HAPO PENYE RED KUHUSU IBARA YA 75 RASIMU YA KATIBA JUU YA SIFA ZA MGOMBEA URAIS NDO NDO HASA MAKUSUDI YA THREAD YANGU MAANA SIJUI KWA HAWA WAGOMBEA AMBAO NI VIONGOZI WA KIROHO WATAJITETEA VIPI KWA HILO

Dini si muhimili wa nne wa dola hivi kuipa mamlaka ya kutoingilia mihimili mingine. Na pia kila mmoja ni kiongozi katika dini yake maana kwa maisha ya dini unawaongoza wengine ili waige mfano wako na ukiweza unawashawishi ili waingie dini yako...ni kiongozi mwenye majukumu hayo. Dini zitabaki lakini mwenye misimamo ya dini zake asituletee fujo sisi tusiokuwa wa dini yake. Hao ndiyo viongozi tunaowataka. Tayari tumewaona baadhi ya viongozi waliotulazimisha kuvaa hijabu maofisini eti ndiyo kuwa waungwana...na hadi dressing code ikaundwa haraka haraka. Wapo waliotenga vyumba vya wizara kuwa nyumba yao ya ibada, wapo waliochukua fedha za serikali na kupelleka kwenye nyumba zao za ibada...hawa ndo tuwakatae lakini ukipata kiongozi asiyewadini yako na akakuheshimu kwa staili ya Ruksa juu ya nguruwe...kama alivyowahisema mzee Mwinyi...anayetoa tamko la kula nguruwe ni ruksa...! Kiongoziasiyetetea dini yake kwa vile ni wa dini hiyon n.k
 
Back
Top Bottom