Maoni ya wananchi: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

Shadow,
Mkuu, kwani mpango wa njia tatu bado unatumika? mbona nasikia uliondolewa kama alivyoondolewa mbunifu wake au?..
 
Zimeshaondolewa isipokuwa zinatumika kwa Magari ya Jeshi,Ya Mawaziri na wakati mwingine kwa Ambulance na Fire... Au Shadow anamaanisha ile tunayoiita "Tatu-Bila" Mwenge hadi Junction ya Kawawa na AH Mwinyi Road???
 
Tatizo tulishalisema zamani.
Traffic Engineering ni somo gumu sana. Mhandisi wa kawaida wa barabara hawezi kulifanya hili somo. Linataka pia uwe na kipaji. Sasa inapotokea MSANII na mwana siasa aanze kutoa maamuzi juu ya hicho kitu, matokea yake ni kuwa anatengeneza MACHINJIONI ....
 
ON a more serious note: hii njia tatu itakuwa imeua watu wengi sana! Sijui kama kuna statistics kuhusu hilo? Lakini naamini si wapita njia, au madereva au abiria, ni wengi tu kwani ilikuwa ni hatari sana.
Sasa tunachohitaji ni tamko rasmi la serikali ikitangaza kufutwa kwa njia tatu na kutangaza utaratibu mpya wa kuboresha barabara na kupunguza foleni
 
Inasemekana zaidi ya watu (pedestrians) wapatao 15 walikufa hapa Dar kutokana na kugongwa na gari au magari kugongana katika kipindi mpango huo ukitumika. Mbunifu EL ndiyo anabeba roho za marehemu hao kwa ubunifu wake ambao haukuwa na uchunguzi wa kina!
 
I hope there is a special hell for people like huyu msanii! Yaani alikuwa anataka sifa akaleta maagizo ya kijinga hata mtoto wa darasa la 1 angemwambia it won't work! Lakini alitaka sifa tu na kuonyesha that he is soo powerful!
 
Unajua watanzania tunatakiwa kubadilika na kuoji haya maamuzi ya kutatanisha. Mtu anaamka na kuweka mpango fulani hata bila ya kufanya utafiti wa kina na kuelimisha watu. Enough is enough...Mr. Politician maamuzi yenu yaendane na masuala ya 'rule of law'.
 
Shadow,
Mkuu, kwani mpango wa njia tatu bado unatumika? mbona nasikia uliondolewa kama alivyoondolewa mbunifu wake au?..

Njia tatu anayoiongelea shadow ni ile ya bagamoyo road ambayo imeongezwa upande mmoja kwa hiyo zimekuwa njia tatu, njia mbili mishale inaonyesha kuelekea mjini na moja mshale kuelekea mwenge,
sasa ngoma ni pale madereva wa bongo tusivojua sheria ya barabarani wanaoenda mjini wanatumia njia mbili na wanaoenda mwenge wanatumia njia mbili
 
Hao TANROADS ni sababu kubwa ya ajali za barabarani maana huwezi kuweka tuta kwenye kupandisha kilima lakini wao wameweka kama matuta matatu ,karibu njia zote tena si kupandisha hata katika kushusha kilima utaona wameweka hiyo dizaini sijui waliiona wapi nafikiri kuna mshamba mmoja ndani yao alisafiri na kuona hayo matuta bila ya shaka yeye aliyaona mitaani kwa ujuaji wake akaona yanaweza kutumika katika highway na zaidi gari zinapopandisha vilima au kushusha ,maana kama basi au track limezidiwa pumzi kwenye kilima basi moja kwa moja litashindwa kuvuka mtihani wa tuta na hapo ndio msalie mtume maana litaanza kurudi kinyumenyume aidha ikiwa ni katika kushusha trailler ya six wheel inaweza kuvuka na kukiacha kichwa kikiendeleza safari wakati trailler ikisebureka mabondeni.
 
Mimi nafikiri kamati ya bunge (Miundo mbinu) inabidi iwe inawafanyia perfomarnce appraisal.

Bunge lina haja ya kupitisha kanuni za kitaalmu kuhusiana na utendaji wa TANROADS mfano Daraja linatakiwa lijengwe katika kiwango na mfumo hupi? kuwepo na uniformity, pili kuwepo na appraisal perfomance za hizi kanda za TANROADS.

Mfano kama ajali nyingi zinatokea eneo fulani basi ukiacha kutupa lawama kwa madereva , pia huyo mtalaamu wa eneo hilo naye awekwe kitimoto.

Mimi nafikiri hawa TANROADS wamekuwa fungate kwa muda mrefu na wengi wetu huwa tunachelea kuwastukia.
 
Njia tatu ni ovyo kabisa na hii inachangiwa na mipango mibovu na madereva wasiojali sheria. Ni jambo la kawaida tu kwa madereva wengi kupita kwenye taa nyekundu.

Hapo awali ilikuwa ni madereva wa daladala na sasa imekuwa kama ugonjwa kwa wengi wenye magari. Je unapoteza kitu gani kufuata kwa usahihi alama za barabarani? Sawa barabara tatu ni makosa tu lakini kuna alama zinazoonyesha magari yaende vipi. Cha kushangaza utakuta magari yamebanana kwenye barabara ambayo inaonyesha kuwa magari kutoka mwenge ndiyo yanapaswa kuitumia barabara hiyo!

Wakati mwingine tuache kulalama kila mtu awajibike kwa nafasi aliyo nayo. kama una gari basi fuata sheria (maana vitu vingine ni 'sunk costs') wakati mipango mingine ikifanywa kuboresha miundo mbinu.
 
Wana ndugu zangu,

Kile chuo cha DIT? kinatengeneza kwa sasa taa za barabarani. Kama wangelipata tenda ya kuzitengeneza hizo taa za Dar tu basi ingelikuwa safi sana. Kuweka alama za barabarani za chini tu (kuweka mistari) ni makosa kwani watu hawaoni hizo alama. kuweka taa za barabarani zikionyesha ni mistari ipi wana taa za kijani na wapi wana nyekundu. Hizi ndiyo zilitakiwa kuwekwa pale kwenye makutano. Faida yake ni kuwa asubuhi zinawaka tatu zinazoenda mjini na jioni zinawaka tatu zinazokwenda Mwenge. Kabla ya kuanza, inabidi kufanya majaribio na kupeleka shule.

Kwanza unatangaza mji mzima sheria mpya. Pia kwa siku kadhaa mnafanya shule kwa madriver. Traffic na watu wa TANROADS walitakiwa kushinda barabarani na kumpa shule kila driver atakayevunja sheria kwa muda tuseme wa wiki mbili. Baada ya hapo zinaanza faini za papo kwa papo. Mwanzo ndogo na muda unavyokwenda zinakuwa kubwa zaidi. Hawa driver wangeliona traffic kibao, tanroads kibao, jamaa wa DIT na hata UDSM wako pale kuwachangamkia, nafikiri kwa mwezi mmoja somo lingelikuwa limeeleweka.

Kamera pia zingelisaidia sana kwani mkosaji angelitafutwa bila kujali kakimbia au lahh. Hiyo wala haina kupokea kitu kidogo. Hili linawezekana ila ni kazi ya muda mrefu na kufanya utafiti mkubwa kabla ya kulifanya.

Kawaida inatakiwa kila kukitokea ajali, wanaweka kwenye ramani ni wapi na lini hiyo ajali imetokea. Ikionekana zimetokea nyingi basi inabidi hapo kitu fulani kifanyike.
 
Kawaida inatakiwa kila kukitokea ajali, wanaweka kwenye ramani ni wapi na lini hiyo ajali imetokea. Ikionekana zimetokea nyingi basi inabidi hapo kitu fulani kifanyike.

kweli kabisa Sikonge.............Traffic Police wanaweza kujifunza mambo ya GIS na kutumia a simple GPS...........kwa kutumia GPS wanaweza kuingiza information zao zote za kipolisi wanazohitaji na za kihandisi pia (Uingizaji wa fomu za accident inabidi kuandaliwa kwa pamoja i.e Traffic Engineers and Traffic Police) na kwa hiyo kurahisisha kazi yao na katika kutengeneza Accident appreciation Map...........of which nafikri itakuwa msaada mkubwa sana both kwa akina Fundi Mchundo na Morani75 kwenye design zao........na police kwa ujumla........

sina hakika sana kama hizi barabara zetu zinafanyiwa safety Audits ......ziwe mpya...au ......pindi tunapobadilisha aina ya matumizi............
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hapa ni wizara ya transport na government at large. Mimi sielewi Tanzania kuna Tanroad, NIT nab ado tupo so behind in transport planning.

Ni vizuri wananchi tukauliza is there any model to prove and predict whatever the strategies wanazokuja nazo zinafanya kazi?

Transport planning/ traffic engineering is a large area na it needs skilled people. It incorporate socio-economic studies, land use na mambo mengi. Before you make final decision on any traffic/transport strategies approach or highway improvement a model should be built to replicate and predict what will happen once that idea is implemented. This helps to set mitigations against any possible impacts such as congestion, accidents, environmental, economic and social impacts.

Sasa watu wetu hapa Tanzania wanaamua vitu bila even a simple model. Na sasa hivi there are advanced transport modelling tools available sijui hiyo wizara ya transport, NIT and TANROAD wanafanya nini? Wanalipwa for what purposes?
 
Tatizo tulishalisema zamani.
Traffic Engineering ni somo gumu sana. Mhandisi wa kawaida wa barabara hawezi kulifanya hili somo. Linataka pia uwe na kipaji. Sasa inapotokea MSANII na mwana siasa aanze kutoa maamuzi juu ya hicho kitu, matokea yake ni kuwa anatengeneza MACHINJIONI ....

..............ha ha haaaaaaaaaaa, mkuu hii imetulia. Anyway lakini mkubwa kazi ya ujenzi wa barabara kuanzia planning (feasibility stage) sikuzote inafanywa na consultants (mostly international consultants). Hawa wanajua how traffic lights should be designed, security lamps and installation of CCTV cameras along the road. Binafsi nadhani Tanzania swala la kuwa na CCTV barabarani, taa za barabarani, na traffic light zakisasa kwa ajili ya kuongozea magari pamoja na watembea kwa miguu si kipaumbele. Nasema hivi kwakuwa hakuna design inayofanyika ikazingatia mambo haya.
 
Tatizo hapa ni wizara ya transport na government at large. Mimi sielewi Tanzania kuna Tanroad, NIT nab ado tupo so behind in transport planning.

Ni vizuri wananchi tukauliza is there any model to prove and predict whatever the strategies wanazokuja nazo zinafanya kazi?

Transport planning/ traffic engineering is a large area na it needs skilled people. It incorporate socio-economic studies, land use na mambo mengi. Before you make final decision on any traffic/transport strategies approach or highway improvement a model should be built to replicate and predict what will happen once that idea is implemented. This helps to set mitigations against any possible impacts such as congestion, accidents, environmental, economic and social impacts.

Sasa watu wetu hapa Tanzania wanaamua vitu bila even a simple model. Na sasa hivi there are advanced transport modelling tools available sijui hiyo wizara ya transport, NIT and TANROAD wanafanya nini? Wanalipwa for what purposes?

ha ha ha mkuu umejitahidi kuchambua. Lakini mkuu umewaonea kusema hakuna models wanazotumia. Naomba utambue kuwa Tanzania inategemea wafadhili kujenga miundombinu kama barabara. Kwakigezo hicho tu ili mradi uweze kupata pesa nilazima upitie kwenye vigezo vya Worldbank. Kwakifupi miradi yote ya barabara Africa lazima iwe appraised kwa model iitwayo HDM-4 so is not true kuwa hawatumii models. zipo model nyingine kama RED model, etc

Tatizo ninaloliona mimi ni usimamizi na inefficiency za serikari at policy level juu ya namna gani miundombinu yetu tunataka iwe.
 
Kawaida inatakiwa kila kukitokea ajali, wanaweka kwenye ramani ni wapi na lini hiyo ajali imetokea. Ikionekana zimetokea nyingi basi inabidi hapo kitu fulani kifanyike.

Sikonge, tatizo la bongo system zake hazijawa centralised. Pia office nyingi hazikoconnected to one another kwa mtandao. Ukizingatia matatizo ya umeme na ufinyu wa matumizi ya ICT, bado si rahisi kutatua tatizo unalosema. Anyway is good watu wanatambua nini kifanyike and the same need to be communicated to policy makers ili mikakati ya kuboresha ianze. Take a simple example, watanzania hawana digitised physical address. Yaani kama unamtafuta mtu inabidi uende unaulizia hatakama garilako lina GPS mashine. Hizo ni baadhi ya challenge zinazotakiwa kutafutiwa ufumbuzi pia. Kitu kidogo kama hiki kingeweza rahisisha kazi ya polisi, na kuboresha mazingira ya biashara kwa ujumla.
 
Mimi nafikiri kamati ya bunge (Miundo mbinu) inabidi iwe inawafanyia perfomarnce appraisal. Bunge lina haja ya kupitisha kanuni za kitaalmu kuhusiana na utendaji wa TANROADS mfano Daraja linatakiwa lijengwe katika kiwango na mfumo hupi? kuwepo na uniformity, pili kuwepo na appraisal perfomance za hizi kanda za TANROADS. Mfano kama ajali nyingi zinatokea eneo fulani basi ukiacha kutupa lawama kwa madereva , pia huyo mtalaamu wa eneo hilo naye awekwe kitimoto. Mimi nafikiri hawa TANROADS wamekuwa fungate kwa muda mrefu na wengi wetu huwa tunachelea kuwastukia.

Mkubwa upo sahihi unajua thread hii imenifurahisha kwakuwa ninmabo ambayo yalinifanya nijiulize maswali mengi sana tatizo ni nini. Mkuu, swala la kiwango cha daraja au barabara vyote vipo wazi tena ni international standard kwakua zinatokana na model ambazo zipo approved kutumika Africa nzima. Tatizo ni usimamizi mkuuu pamoja na kale kamchezo kenu ka rushwa.
 
Back
Top Bottom