Maoni ya wananchi: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

Najua huko saudi arabia unakoishi kuna restriction sana ya watu wa aina fulani kutoa maoni yao. Karibu sana kwenye free world ya JF!
Ingependeza kutumia siku ya leo kwa kutoa au kuchangia vitu vya maana ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo hapo bongo badala ya kuwa Hadija Kopa... kumbuka kesho huna jeuri ya kuwepo hapa na mipasho yako...
 
Fly-overs ni wazo zuri. Lakini nina mashaka kama zitawezekana Tz kutokana na magari mengi kuwa vimeo.

Fly-overs system inabidi iende sambamba na ukaguaji wa magari mara kwa mara. Asilimia kubwa ya magari bongo hayako kwenye hali mzuri kutokana na ukosefu wa regular check-up. Kwa hiyo nina wasiwasi tutakuwa tunapata ajali nyingi zinazotokana na magari yanayoshindwa ku-accelerate kwenye slope ya hizo fly-overs. Hebu imagine jinsi vipanya na malori yatakavyokuwa yanapoteza maisha ya watu kwa ku-flip baada ya kukwama kupanda kwenye hizo fly-overs? I mean, ikiwa tunashuhudia malori kadhaa kupinduka baada ya kushindwa kupanda kale kamlima ka pale junction ya Kawe, tuweza kuhimili fly-overs kweli?

Kwa mtazamo wangu, njia mbili sambamba tunaweza kuzitumia kupunguza msongamano wa magari:

1)Kutanua barabara - tuongeze idadi ya lanes kwenye major roads kutoka mbili mpaka nne kila upande. Then, tuzigawe hizo lanes mara 2. Lane 2 za kulia zinakuwa za high speed lanes kwa magari madogo. Na 2 za kushoto zinakuwa za dala dala na malori. Tusisahau kuwa foleni bongo zinasababishwa na madaladala. Kwa hiyo tu kizitengea lanes zake, tutaweza kutibu suala la foleni kwa kiasi kikubwa.

2) Tuongeze idadi ya barabara - Tuna barabara chache sana Bongo. Tukitumia mfano uliouweka wa maeneo ya Mbezi Beach, Tegeta na kuendelea, utaona kuwa kuna njia mbili tu za kutoka na kuingia Mebzi Beach -Ali Hassan Mwinyi na ile inayoanzia Avocado Kawe mpaka barabara ya White Sand Hotel (bado inajengwa). Hii idadi ni ndogo ukizingitia idadi ya watu wanaoishi maeneo haya. Tegeta peke yake ina idadi ya watu wanaotesheleza kuitwa wilaya. Anyway, mkazi wa Mbezi Beach akitaka kwenda airport inabidi aje mpaka mwenge kupata access ya kwenda airport. Inabidi tujenge barabara kama mbili au tatu zinazounganisha Mabezi Beach na Mbezi Kimara? Tena wala zisiishie hapo, at least moja au mbili ziendelee all the way mpaka Pugu Road or something. Kuna ile barabara ya kupanga kule Goba, mpaka leo ujenzi wake bado wanaupiga danadana. Au vipi ile barabara ya Wazo Hill, kwa nini wasiendeleze zaidi. Yaani imeishia pale kwende kile kiwanda tu....kuendelea mbele ni mbonde tu.

Kwenye fly-over hiyo, iwapo gari ingetaka kwenda Msasani kutokea Mwenge, kungekuwa na sehemu (mstari) maalum ya kuliwezesha gari hilo kuingia pole pole kwa kutumia utaratibu wa kisheria unaojulikana kama "yielding". Utaratibu huo ungetumika pia kwa wale ambao wangetaka kwenda Kinondoni kutokea Mwenge, hivyo kuwezesha magari kutembea kwa kasi zaidi bila kusimama, na hivyo kufanikiwa kuondoa kabisa tatizo la msongamano wa magari.

Tukiondoa suala la fly-overs, nakubaliana na wewe kuhusu kuweka filters kwenye junctions. Tukiongeza lanes, ninaamini hizo filters zitafanya kazi vizuri sana.

Kwa kifupi, mimi naona barabara zetu zibaki tu chini. Tunachotakiwa ni kuongeza barabara na lanes. Pia tuzitenganishe hizo lanes baina ya magari na daladala. Tukifanya hivi tutaweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa.
 
Mmi naona tatizo ni kuwa mji wetu huduma muhimu zote zimerundikana sehemu moja,kila kitu posta,sasa inafanya kuwe na msongamano kuelekea sehemu moja..so tuangalie kugawa huduma ili tuweze angalau badala ya watu kila aibihu kudamkia posta kununua samaki wabichi basi wawe wananunuliwa tazara(mfano),na baadhi ya huduma nyingine..
 
Tatizo ni msongamano! Je wanaJF wanaushauri gani juu ya hilo.. sasa mdada tayali umekibilia kwenye kuhukumu... hapana shaka una uwalakini kuwepo hapa JF

Kibunango, be real bana hapa tunajadili serious issue. Hivi wewe unaijua foleni ya Dar? alichokiandika MM ndo ukweli wenyewe. Watawala wetu hawajui kwamba wamepewa dhamana ya kulinda the general good ya wote.

Kama wanavyosema wenzangu foleni Dar siyo kero tena limekuwa ni Jambo la kitaifa! Jiulize kama kuna mgonjwa TMJ anahitaji kukimbizwa Muhimbili..si atafia njiani? Ushauri, inabidi tuboreshe PUBLIC TRANSPORT, ukifanya hivi hata wanaonunua magari watapungua (wengi wananunua si kwa kupenda bali kuepuka adha za kusimama kwenye dala dala, ambazo hata kuzipanda mpaka uwe na nguvu!).

Tanzania we cant afford shortcut, hata fly overs sina uhakika kama zinaweza kusaidia, kwa bara bara zipi?..mnaonaje tukikarabati hizo bara bara harafu tukaongea na serious investors tukajenga trams (treni) from my experience Europe wana vibara bara vidogo lakini trams zimerahisisha usafiri. Well hatuwezi kuwa Europe leo au kesho, but hey..we have to dare tufanye kitu ambacho kitatusaidia na generations nyingine zijazo!

At times I wonder serikali inafaidika vipi na wasomi wake..kwa nini isiwatumie maprofesa kibao wa uhandisi...wakafikiria namna ya kutatua hili tatizo? mpaka Lowassa mwenye degree ya sanaa ndo anakuja kutupa ideas za kutumia bara bara efficiently? some body somewhere must not be doing his homework.. and you all know who!
 
Ogah you are right, lakini ukiangalia kwa layman analysis utaona kuwa ajali ndogondogo zimeongezeka, congestion haijapungua, imeanza hata kuleta confusion vichwani mwa madereva, na enforcement yake ni very mechanical. Inaonekana kama ni decision iliyofanyika ili kujitafutia political gains lakini haikutafitiwa kama inaweza kuendana na mazingira ya sasa.

1.Congestion haijapungua - this can be evaluated and report should be made public.....moja ya main issue itakayoangaliwa ni "travel times" on different sections in relation to its respective Level of Service

2.Confusion Vichwani mwa Madereva - Hapa ni Enforcement na hasa katika utoaji wa leseni za kuendesha magari.......Dar es salaam kuna "madreva" sio madereva. katika hili serikali inahitaji mabadiliko ya HALI YA JUU na hasa ukizingatia SAFETY ni kitu cha kwanza barabarani.

3.Enforcement yake ni mechanical - nakubaliana na wewe zote soft and mechanical ni muhimu ziende pamoja........mind you the technology is very simple and not expensive either.

4. Decision na political gains - you may assume that........but to me technical officers always ndio wa kuwapa policy makers idea ili kufanikisha malengo ya technicalities walizokubuhu nazo....sasa kama ilikuwa ni political gains.........mmmhhh interesting!!
 
Kibunango, be real bana hapa tunajadili serious issue. Hivi wewe unaijua foleni ya Dar? alichokiandika MM ndo ukweli wenyewe. Watawala wetu hawajui kwamba wamepewa dhamana ya kulinda the general good ya wote.

Kama wanavyosema wenzangu foleni Dar siyo kero tena limekuwa ni Jambo la kitaifa! Jiulize kama kuna mgonjwa TMJ anahitaji kukimbizwa Muhimbili..si atafia njiani? Ushauri, inabidi tuboreshe PUBLIC TRANSPORT, ukifanya hivi hata wanaonunua magari watapungua (wengi wananunua si kwa kupenda bali kuepuka adha za kusimama kwenye dala dala, ambazo hata kuzipanda mpaka uwe na nguvu!).

Tanzania we cant afford shortcut, hata fly overs sina uhakika kama zinaweza kusaidia, kwa bara bara zipi?..mnaonaje tukikarabati hizo bara bara harafu tukaongea na serious investors tukajenga trams (treni) from my experience Europe wana vibara bara vidogo lakini trams zimerahisisha usafiri. Well hatuwezi kuwa Europe leo au kesho, but hey..we have to dare tufanye kitu ambacho kitatusaidia na generations nyingine zijazo!

At times I wonder serikali inafaidika vipi na wasomi wake..kwa nini isiwatumie maprofesa kibao wa uhandisi...wakafikiria namna ya kutatua hili tatizo? mpaka Lowassa mwenye degree ya sanaa ndo anakuja kutupa ideas za kutumia bara bara efficiently? some body somewhere must not be doing his homework.. and you all know who!

Kamanda Masanja, kama una ushabiki na MWK ni juu yako lakini penye ukweli lazima aambiwe....

Nikirudi kwenye mada umezungumzia waandisi na wasomi wengine katika kero hii ya msongamano. Lakini umeshindwa kijua ni nini tatizo la msongamano jijini.

Ni vema kwanza kujua tatizo ambalo limeleta kadhia hii, baada ya hapo ni rahisi kujadili namna ya kuondokana na tatizo hilo.

Kwa maoni yangu tatizo hili linachangiwa na mambo yafuayo
  • Mipango Miji kwa ujumla
  • Ongezeko la waakazi wa jiji
  • uchumi

Katika suala la Mipango Miji, Jiji la DSM leo lina Halmashauri tatu, lakini huduma muhimu zinapatikana katika halmashauri moja tu. Hii inasababisha waakazi karibia wote kwenda katika halmashuri moja kila siku hivyo kusababisha msongamano.

Ni vema kutawanya huduma muhimu katka halmashauri zote, hii itapunguza msongamano kwa asilimia kubwa.
 
Mimi ktk utafiti wangu kwa suala la msongamano dar ni kuwa hatujafikia hatua hiyo ya kujenga fly-over. Dar kuna barabara nyingi mno za mitaani zimesaulika, hazifanyiwi ukarabati. Chukua mfano wewe ulikuwa unatoka Mbezi luguluni unaenda mbezi beach kitu gani kingekupeleka Ubungo kama kungekuwa na barabara inayounganisha mbezi luguluni na mbezi beach?

Haya chukulia mtu yuko Manzese anataka kwenda kinondoni kuna barabara nyingi sana pembeni mwa morogoro road ambazo unaweza kuzitumia ili ufike kinondoni lakini itakubidi uende mpaka mapipa maana hizo barabara ni mbovu kupita maelezo. why kila mtu anataka atumie morogoro road? Au Alhasani mwinyi? believe me hizi barabara zikitengenezwa kwa kiwango cha lami hakuna mtu atakayeng'ang'ania kupita haya mabarabara makubwa. Fikiri mtu anaenda airport kutoka kibamba lazima apite ubungo unategemea usiwepo msongamano? Ukitengeneza hizi barabara hatutakuwa na msongamano kamwe.

Pili office zetu tuangalie namna ya kuzi-alocate isiwe kila kitu Posta na kariakoo. yafaa kuanza kubuni maeneo mengine ya kujenga maofisi na sehemu za biashara kama supermakets pembeni mwa mji.Kwa sababu sasa hivi kila mtu akiamuka asubuhi ni posta, kariakoo, mjini na jioni nyumbani hii lazima kuwe na msongamano.
 
Zote points ila kwa ukweli ivi jamani hata daraja la feri limetushinda miaka nenda rudi sasa huku mitaani si ndio kabisa, barabara ya uhuru ndio usiseme
ivi na hii ya bagamoyo rd morocco mwenge sasa kuna lane 3,mbili zimewekwa alama ya kwenda town sasa kwaio ni watu wa kutoka mwenge tuu ndio watumie au na ndio kuchanganyana tu!!!!!
 
MwanaH na wakuu wengine mliotangulia..... Hili swala la msongamano wa magari jijini kwa kweli limeongelewa sana humu jamvini......
1. Tulianzia kwenye issue ya project iliyofanywa na wale wakuu wa pale Chuo cha Ardhi, siku hizi panaitwa UCLAS, they did a marvelous job.

Kwanza ndugu Morani75 nikusahihishe kidogo tu. UCLAS kwa sasa inaitwa Chuo Kikuu cha Ardhi (Ardhi University).

Nikirejea kwenye mjadala, tatizo kubwa la msongamano jijini Dar es salaam linatokana na mipango duni ya miundo mbinu ya barabara. Ni bahati mbaya kwamba waliosanifu barabara za jiji nadhani hawakutilia maanani ukuaji wa jiji na ongezeko la magari.

Sasa nini kifanyike ili kuondoa tatizo japo inahitaji uwekezaji mkubwa
1. Barabara zote zinazoingia na kutoka jijini zote zipanuliwe na ziwe dual carriage-way, hili lina athali zake kwamba bomoaboma itakuwa nyingi.
2. Maeneo ya makutano ya barabara kuu zijengwe multi-level roads, nina maana kusiwe na traffic light. Wahandisi watanisaidia kuweka kiswahili sawa.
3. Barabara zaidi ziimarishwe ili kuondoa tatizo la wasafiri kutumia barabara kuu tu wanapotaka kwenda mjini, kwa mfano, kupitia Makongo juu au changanyikeni kwenda maeneo ya mbezi hadi Tegeta.
4. Katikati ya jiji barabara zipamgwe za kuingia tu na za kutoka, nin maana (one way traffic roads)

...Mengine nitaendelea baadaye.
 
  • Magari mengi yaingiayo ndani ya jiji ni machakavu
  • Barabara zote ndani ya Jiji zinatosha na nzuri
  • Ufungaji wa barabara za mitaa maarufu Jijini

Iwapo kweli tunakata kuondokana na msongamano wa magari Jijini, ni vema kuangalia ubora wa magari ambayo yanaingia Tz. Kwa wengi hii ni lawama.

Upo umuhimu wa kufunga kabisa barabara maarufu ndani ya jiji. Barabara hizo zitumike kwa waendao kwa miguu na wapanda baiskeli tu. Hii itasaidia watu kuacha magari yao majumbani na kutumia public transport kwenda ndani ya Jiji, Kimazingira ni wazo zuri huku kiafya ni jambo la msingi.

Barabara zote za mjini na nzuri na wala hazihitaji kupanuliwa. kinachotakiwa hapa ni kuwepo kwa kodi ya matumizi ya barabara za mijini. Hii ni zaidi na kodi ya kuegesha gari.
 
ukiangalia kiwango cha uchumi wa Tanzania na infrastructure ilivyo primitive tutakuwa tunajidanganya kufikiri serikali itaweza kujenga highway interchanges dar-es-salaam wameshindwa kumaintain barabara walizojenga kwa misaada na mikopo hawana uwezo wa kutatua tatizo hilo.

Jambo pekee lililobakia ni ni kuwataka wananchi wenye pesa za kihalali na za mafisadi tuchange na mabepari wengine wa nje ya nchi tuanzishe tollroad authority na government ikaribishwe. Badala ya Lowassa na mafisadi wenzake kuchukua pesa Tanesco kwa capacity charges wangeweza kupata fedha kihalali kutoka kwa wenye magari,maisha yatakuwa bora haraka
 
  • Magari mengi yaingiayo ndani ya jiji ni machakavu
  • Barabara zote ndani ya Jiji zinatosha na nzuri
  • Ufungaji wa barabara za mitaa maarufu Jijini

Are you serious unaposema barabara zetu mzuri na zinatosha?

Ni uzuri upi huo unaoungelea?

Barabara bongo ni chache mno. Na isitoshe hizo chache ni mbaya na ndogo. Sasa sijui mzee unazumngumzia barabara zipi? Labda ungefafanua tafadhali..

Iwapo kweli tunakata kuondokana na msongamano wa magari Jijini, ni vema kuangalia ubora wa magari ambayo yanaingia Tz. Kwa wengi hii ni lawama.

Upo umuhimu wa kufunga kabisa barabara maarufu ndani ya jiji. Barabara hizo zitumike kwa waendao kwa miguu na wapanda baiskeli tu. Hii itasaidia watu kuacha magari yao majumbani na kutumia public transport kwenda ndani ya Jiji, Kimazingira ni wazo zuri huku kiafya ni jambo la msingi.

Nakubaliana na wewe. Kuna umuhimu wa ki-set kiwango cha ubora cha magari yanayoingia nchini. Lakini hiyo haitatosha peke yake. Bado tunahitaji kufuatilia kwa karibu ubora wa magari yaliyo tayari nchini. Magari mengi ni vimeo vya kutupwa. Kwa kweli tutajichimbia kaburi wenyewe kama hatutaweka sawa ubora wa magari kwanza kabla hatufikiria kujenga hizo fly-overs.

Suala la kufunga barabara downtown linawezekana, na litasaidia kupunguza foleni. Pale mjini tunaweza ku-implement shuttles (buses au trains) ambazo zita control mizunguko ndani ya downtown.

Barabara zote za mjini na nzuri na wala hazihitaji kupanuliwa. kinachotakiwa hapa ni kuwepo kwa kodi ya matumizi ya barabara za mijini. Hii ni zaidi na kodi ya kuegesha gari.

Again, are you serious? Kabisa una uhakika unaposema barbara zetu haziitaji upanuzi?

Unapozungumzia kuwepo kwa kodi ya matumizi ya barabara unamaanisha tuzigeuze barabara zetu kuwa toll-roads? Huoni kama kufanya hivyo tutajishindilia wenyewe msumari wa gharama za maisha

Binafsi, sidhani kama tunahitaji toll sytem kwenye major roads. Nitaunga mkono wazo la toll roads kama litahusishwa kwenye ujenzi wa private roads. Vinginevyo, bado hatujafikia hatua ya kutoza watanzania toll (directly)kwenye utumizi wa barabara. Nafikiri tunalipa kodi (inderectly) ya barabara. Si hivyo?
 
Are you serious unaposema barabara zetu mzuri na zinatosha?

Ni uzuri upi huo unaoungelea?

Barabara bongo ni chache mno. Na isitoshe hizo chache ni mbaya na ndogo. Sasa sijui mzee unazumngumzia barabara zipi? Labda ungefafanua tafadhali..

Nakubaliana na wewe. Kuna umuhimu wa ki-set kiwango cha ubora cha magari yanayoingia nchini. Lakini hiyo haitatosha peke yake. Bado tunahitaji kufuatilia kwa karibu ubora wa magari yaliyo tayari nchini. Magari mengi ni vimeo vya kutupwa. Kwa kweli tutajichimbia kaburi wenyewe kama hatutaweka sawa ubora wa magari kwanza kabla hatufikiria kujenga hizo fly-overs.

Suala la kufunga barabara downtown linawezekana, na litasaidia kupunguza foleni. Pale mjini tunaweza ku-implement shuttles (buses au trains) ambazo zita control mizunguko ndani ya downtown.

Again, are you serious? Kabisa una uhakika unaposema barbara zetu haziitaji upanuzi?

Unapozungumzia kuwepo kwa kodi ya matumizi ya barabara unamaanisha tuzigeuze barabara zetu kuwa toll-roads? Huoni kama kufanya hivyo tutajishindilia wenyewe msumari wa gharama za maisha

Binafsi, sidhani kama tunahitaji toll sytem kwenye major roads. Nitaunga mkono wazo la toll roads kama litahusishwa kwenye ujenzi wa private roads. Vinginevyo, bado hatujafikia hatua ya kutoza watanzania toll (directly)kwenye utumizi wa barabara. Nafikiri tunalipa kodi (inderectly) ya barabara. Si hivyo?
Kamanda hebu rudi nyuma na tizama tatizo la msongamano wa magari hapo DSM. Magari mengi huwa yanaelekea sehemu moja tu ya Jiji hilo ambalo lina Halmashauri tatu kubwa. Napozungumzia utawanyaji wa huduma nina maana hata zile ofisi kubwa kubwa ndani ya jiji, ambazo zina wateja lukuki.

Kufunga barabara za ndani ya jiji ni mojawapo ya hatua muhimu katika kuondoa tatizo la msongamano. Iwapo kutakuwepo na hatua za makusudi za kufunga barabara hizo, ina maana kuwa wengi wataacha magari yao majumbani na kutumia usafiri wa daladala.

Kama barabara za bongo zitahitaji upanauzi basi ni vema kupanua barabara kwa ajili ya daladala na teksi. Na sio kupanua barabara kwa magari ya kawaida. Iwapo upanuzi wa lane utakuwa kwa ajili ya public transport hii ina maana ya kujenga ufanisi kwa daladala hivyo kutoa ushawishi mkubwa kwa watumiao magari binafsi kupanda daladala hizo.

Kuna baadhi ya wajumbe wamezungumzia kuhusu "fly over" ujenzi wake iwapo utashirikisha kampuni binafsi hapana ujanja zaidi ya kulipia kodi katika matumizi ya hizo fly over. Na iwapo zitzjengwa ni vema zijengwe nje ya katikatika ya Jiji na zijengwe kwa lengo la kuunganisha Halmashauri hizo tatu pasipo kupitia katikati ya jiji.
 
Ni wazo zuri kabisa na linahitaji msaada wa kufikishwa kunakohusika.

Lakini mimi nadhani ni bora kuanza kutatua tatizo la mifereji ya maji machafu kwanza kabla ya kulaza barabara yoyote ile.

Sasa serikali inatumia vipi wasomi waliopo Tanzania kushiriki kujenga nchi ndio mjadala.

La sivyo kuna siku mvua itakuja kunyesha na mji mzima itajaa maji kwa miezi na kutokee mlipuko wa magonjwa.

Pesa zinazoibwa zingesomesha vijana wenzetu katika nchi zilizoendelea ambako ukiondoa mafuriko katika maeneo ya mabonde, sijawahi kuona maji yamekwama mahala fulani.

Mungu ibariki Tanzania siku moja ibadilike.
 
Kamanda hebu rudi nyuma na tizama tatizo la msongamano wa magari hapo DSM. Magari mengi huwa yanaelekea sehemu moja tu ya Jiji hilo ambalo lina Halmashauri tatu kubwa. Napozungumzia utawanyaji wa huduma nina maana hata zile ofisi kubwa kubwa ndani ya jiji, ambazo zina wateja lukuki.

Kibunango,
Mbona decentralization ya offisi imeanza siku nyingi tu! Mabenki mengi (ndio biggest employer) yanafungua matawi kila kona ya jiji. Tanesco, post office, na telecommunication companies, kama Vodacom and the like, wana watawi kila sehemu. Idadi ya watu waneolekea downtown imepungua kwa kiasi kikubwa. kuna baadhi ya watu inabidi wapitie downtown kwenda na kurudi makazi. Hii yote inasababishwa na uchache wa barabara.

Kama barabara za bongo zitahitaji upanauzi basi ni vema kupanua barabara kwa ajili ya daladala na teksi. Na sio kupanua barabara kwa magari ya kawaida. Iwapo upanuzi wa lane utakuwa kwa ajili ya public transport hii ina maana ya kujenga ufanisi kwa daladala hivyo kutoa ushawishi mkubwa kwa watumiao magari binafsi kupanda daladala hizo.

Hii ndio mimi nazungumzia. Mawazo yangu ni kwamba tuongeze lanes ili baadhi ya hizo lanes ziwe kwa ajili ya daladala na malori tu. Tena kwa ishu ya malori, inabidi yakatazwe kutumia baadhi ya barabara.

Unajua, Bongo magari sio mengi kama tunavyodhania. Kinachofanya yaonekane mengi ni uchache wa barabara. Pindi tukiziongeza na kuzitanua, hapo ndio tutakapoweza kuona ni kiasi gani tuna magari.

Of course, watu wanaendelea kungiza magari kwa wingi. Kwa hiyo, haitachukua muda kabla idadi ya magari haija-tripple.
 
Tatizo la msongamano ndani ya jiji linaweza kupungua kwa kuongeza au kweka kodi ya kuingia jijini. Sioni ulazima wa kila mwenye gari kuingia mjini wakati anaweza kupanda daladala..

Apande daladala zipi? Hivyo vipanya vya kina Afande Kula Kula?
 
Mimi ktk utafiti wangu kwa suala la msongamano dar ni kuwa hatujafikia hatua hiyo ya kujenga fly-over. Dar kuna barabara nyingi mno za mitaani zimesaulika, hazifanyiwi ukarabati. Chukua mfano wewe ulikuwa unatoka Mbezi luguluni unaenda mbezi beach kitu gani kingekupeleka Ubungo kama kungekuwa na barabara inayounganisha mbezi luguluni na mbezi beach?

Haya chukulia mtu yuko Manzese anataka kwenda kinondoni kuna barabara nyingi sana pembeni mwa morogoro road ambazo unaweza kuzitumia ili ufike kinondoni lakini itakubidi uende mpaka mapipa maana hizo barabara ni mbovu kupita maelezo. why kila mtu anataka atumie morogoro road? Au Alhasani mwinyi? believe me hizi barabara zikitengenezwa kwa kiwango cha lami hakuna mtu atakayeng'ang'ania kupita haya mabarabara makubwa. Fikiri mtu anaenda airport kutoka kibamba lazima apite ubungo unategemea usiwepo msongamano? Ukitengeneza hizi barabara hatutakuwa na msongamano kamwe.

Pili office zetu tuangalie namna ya kuzi-alocate isiwe kila kitu Posta na kariakoo. yafaa kuanza kubuni maeneo mengine ya kujenga maofisi na sehemu za biashara kama supermakets pembeni mwa mji.Kwa sababu sasa hivi kila mtu akiamuka asubuhi ni posta, kariakoo, mjini na jioni nyumbani hii lazima kuwe na msongamano.

Barabara inayotoka Mbezi Beach hadi Mbezi Luguruni [sic] ipo, lakini tatizo ni kwamba haiko kwenye hali nzuri. Kipindi kifupi kilichopita barabara hiyo, ambayo inapitia Goba hadi Mbezi Luis, iliweza kupitika kwa muda wa dakika 25 hadi 30, ingawa ni kwa uangalifu mkubwa kutokana na kuwapo kwa milima na mabonde na kona kali MNO! Lakini baada ya mvua zilizonyesha na zinazoendelea kunyesha, barabara hiyo imeharibika kiasi cha kupitika kwa shida sana au kutopitika kabisa kwenye sehemu nyingi.

Nayapenda mawazo yako... nayapenda sana!
 
Back
Top Bottom