Maoni ya wananchi: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

Huu uhuni na viini macho jijini mbona ni mambo ya miaka yote? Kuna jipya gani hapa? Hizo fedha wanazolipia consultancy wapewe ripoti ya msongamano wa magari ni matumizi mabaya ya kodi zetu. Huhitaji kufanya survey yoyote kubaini kuwa hizi barabara zina msongamano. Labda uniambie inahitajika ripoti ya kwenda kuombea mkopo wa fedha mahali (IMF fulani au world bank) vinginevyo ni wizi mtupu.

Kabla ya uchaguzi uliopita tulipigiwa stori hiyo hiyo na ilienda mbali zaidi kiasi cha watu kuvunjiwa vijumba vyao vilivyokuwa ndani ya eneo la barabara. Baada ya uchaguzi tunaona kimya na hadi sasa majengo mapya lukuki yameoteshwa usawa wa yale yaliyovujwa. Unataka kuniambia wanafikiri kuna uwezekano magari yamepungua ndani ya miaka 3-4 iliyopita? Maana wakati huo walikuwa rede kabisa kuipanua (the false impression given then).

Wasitufanye watoto kiasi hicho bwana tunajua wanachofanya... danganya toto.
 
Mbona zitajengwa nyingi tu kuelekea mwakani! Nyingine zitawekwa matuta while ni highways (moro Rd), fidder roads zitajengwa bila ya mitaro ya maji taka(Kigogo-maziwa), taa zitawekwa na kuungua baada ya kitambo kidogo(Manzese-Tandale), pembuzi yakinifu nyingi zitafanywa ili mradi kuwepo na linaloendelea kuelekea mwakani( Magari yaendayo kasi), uhakiki wa mapato (Ubungo stand na Soko la Kariakoo), wanafunzi elimu ya juu watapewa mikopo kwa viwango vya kuridhisha.
 
Ule usemi wa wahenga usemao SUBIRA YAVUTA HERI umedhihirika kwa wakazi wa Dar,baada ya Kampuni ya ujenzi ya MAC Construction kuanza mchakato wa kutathimini idadi ya magari yanayotumia barabara ya Ally Hassan Mwinyi na ile ya New Bagamoyo kwa kipindi cha asubuhi hadi jioni kuanzia jana tarehe 14/04/2009 hadi kesho 16/04/2009.Kwa wakazi wa Dar wanaotumia barabara hizo mbili wameshuhudia kwenye makutano ya Sam Nujoma Mwenge,Shekilango Bamaga,Kajenge Sayansi na Kawawa Morocco kuna vijana waliovaa visibau vinavyong'aa (Reflectors). Akihojiwa na Bonge wa Power Breakfast kiongozi wao alisema kuwa wapo katika mchakato wa kuongeza barabara hiyo kutoka Morocco hadi Tegeta kuwa ya njia nne. Hakika hii itakuwa faraja kwa wakazi wa Dar ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi barabarani.

Mkuu,

Yaani hata greda la kusawazisha kifusi halijapita wewe umeshaanza kushangilia...!!?? Ndio kwanza wanahesabu idadi ya magari yanayopita njia hiyo....maana yake hata kuchora plan bado...ukishakuwa na plan ndio hela ianze kutafutwa...then mkandarasi atafutwe...ujenzi uanze..duh...hiyo itakuwa tayari 2015..!!
 
hizo chai tu
huu msemo wa vijana wa udsm......karibu sana..
attachment.php

iangalieni kilwa road....
 
Attachments

  • kilwaroad.jpg
    kilwaroad.jpg
    20.4 KB · Views: 202
...Akihojiwa na Bonge wa Power Breakfast kiongozi wao alisema kuwa wapo katika mchakato wa kuongeza barabara hiyo kutoka Morocco hadi Tegeta kuwa ya njia nne. Hakika hii itakuwa faraja kwa wakazi wa Dar ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi barabarani.

...Hawafikirii ile gridlock katikati ya jiji!

wajaribu Congestion Charges kuingia katikati ya jiji, Jumatatu mpaka Ijumaa; kuanzia pale RAILWAYS GEREZANI, KAMATA, MSIMBAZI, FAYA, SALANDER BRIDGE nk, halafu iwe marufuku magari zaidi ya tani 3.25 kuingia mjini kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni.
 
Tusker,
Mie kidogo nina mwanga wa hiyo iitwayo traffic Engineering na roads designing. Ninachoweza kukuambia kuwa hiyo ni ndoto. Ni sawa na wazimbabwe walikuwa wanasema wazi kabisa kuwa '... hizo ziro wanazozikata, zitarudi tena sasa hivi..' Watu wakishajua kuwa mjini tambarale, basi ndiyo kila mtu nyumbani atanunuliwa gari.

Inabidi ukumbuke milele kuwa siku utakayosikia wanajenga barabara za chuma/reli ili kuhudumia usafiri wa city center (Metro, trams, bus train za juu na ardhini nk - hata kama zinatumia mafuta) basi siku hiyo ndiyo unaweza ukaanza kushangilia.

Tatizo ni kuwa City Center ni kama mdomo wa chupa. Hata kama huko kwenye kitako utakufumua na kukupanua sanaa tu, kumbuka idadi ya maji yanayoingia au kutoka inatokana na shingo ya chupa. Shingo ya chupa kwa Dar es salaam ni hizo barabara chache sana na nyembamba sana kama Uhuru road, Ali H.Mwinyi Road, Morogoro Roads, Kilwa Roads na Pugu road??(nimeisahau) na hapo zinakuwa ndiyo zimeisha. Sasa hata ushindilie vipi, inavika sehemu Posta inasema "I can't take no more......" na hapo unaona magari yamesimama na wengine hadi kuzima injini za magari.

Dawa na kuijenga haraka Dodoma yenye barabara pana na kuhamishia huko makao makuu. Hii walau itafanya mji wa Dar upumue kidogo kabla ya kujaa tena huku tukianza kushuhudia Dodoma ikifurika watu kama mvua + wale wanafunzi 40,000 wa Dodoma University na hapo ongeza wafanyakazi na vitengo vyote vitakavyokuwa vikihudumia wanafunzi hao na wageni wote waliohamia makao makuu Dodoma.
 
Ule usemi wa wahenga usemao SUBIRA YAVUTA HERI umedhihirika kwa wakazi wa Dar,baada ya Kampuni ya ujenzi ya MAC Construction kuanza mchakato wa kutathimini idadi ya magari yanayotumia barabara ya Ally Hassan Mwinyi na ile ya New Bagamoyo kwa kipindi cha asubuhi hadi jioni kuanzia jana tarehe 14/04/2009 hadi kesho 16/04/2009.Kwa wakazi wa Dar wanaotumia barabara hizo mbili wameshuhudia kwenye makutano ya Sam Nujoma Mwenge,Shekilango Bamaga,Kajenge Sayansi na Kawawa Morocco kuna vijana waliovaa visibau vinavyong'aa (Reflectors). Akihojiwa na Bonge wa Power Breakfast kiongozi wao alisema kuwa wapo katika mchakato wa kuongeza barabara hiyo kutoka Morocco hadi Tegeta kuwa ya njia nne. Hakika hii itakuwa faraja kwa wakazi wa Dar ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi barabarani.

SIR,

we have been doing this for years, the solution is right there in their shelves!
 
Salaam, Tatizo la congestion Dsm linahitaji 'strategies' mbali mbali kutoka kwa stakeholders mbali mbali. Mfano watu wa mipango miji wanaweza kuanzisha satellite towns. Watu wa usafiri majini wanaweza kuanzisha usafiri wa boti/ferry kati ya city centre na outskirts kama Kunduchi n.k. Watu wa reli wanaweza kuanzisha huduma hapa mjini kwa reli zilizopo. Kupanua barabara peke yake kutasaidia kidogo bali jawabu haswa ni kama nilivyoeleza. Mambo kama congestion pricing pia inaweza kusaidia kwani imefanikiwa sana katika jiji la London. Lakini ukiweka congestion pricing lazima uwapitie watu njia nzuri mbadala yaani kuwepo usafiri wa mabasi ya kuaminika. Watu wanaweza pia kuwa encouraged kutumia baiskeli kama wanavyotumia wengi kule Ulaya. Nilikutana na professor mmoja wa kule Denmark anayetumia baiskeli kwenda chuoni kufundisha. Mimi naamini joint efforts ya professionals and stakeholders inaweza kupata ufumbuzi japo solutions nzuri zaidi zinahitaji muda mrefu kuona mafanikio.
 
Siku zote tumekuwa tunatabika na foleni si asubuhi wala jioni wakati huo huo vihice vimepungua sana katika ya jiji lakini foleni hipo pale pale tatizo vihice au bala bala ndogo?
Mfano:
1.Bala bala ya morogoro asubihi foleni inaanzia
manzese, jioni foleni inaanzia kona ya akiba saa 11
kufika Kimara saa 1 usiku au saa 2 usiku
anaekwenda moro amefika wa Mbezi usiseme je
Kibamba. TATIZO NINI?
 
Tatizos
-Mfumo mbovu wa barabara vs wingi wa magari.ilitakiwa tuwe na lane atleast 4 ways
-feeder roads nyingi ziko ktk hali mbaya
-fly overs zingesaidia kupunguza foleni
-city plani ni mbovu kuliko maelezo.watu woote wanatoka upande mmoja asubuhi kwenda mjini na jioni tunarudi woote toka mjini.tunahitaji remote cities zenye kila kitu
 
Siku zote tumekuwa tunatabika na foleni si asubuhi wala jioni wakati huo huo vihice vimepungua sana katika ya jiji lakini foleni hipo pale pale tatizo vihice au bala bala ndogo?
Mfano:
1.Bala bala ya morogoro asubihi foleni inaanzia
manzese, jioni foleni inaanzia kona ya akiba saa 11
kufika Kimara saa 1 usiku au saa 2 usiku
anaekwenda moro amefika wa Mbezi usiseme je
Kibamba. TATIZO NINI?

RIP Mzee Hamis Akida!
 
Kuondoa foleni kazi ndogo : Waweke kituo cha kukusanya mapato Manzese/Morocco (10,000/- kwa kila gari linalovuka) - foleni itapungua tu!
 
Siku zote tumekuwa tunatabika na foleni si asubuhi wala jioni wakati huo huo vihice vimepungua sana katika ya jiji lakini foleni hipo pale pale tatizo vihice au bala bala ndogo?
Mfano:
1.Bala bala ya morogoro asubihi foleni inaanzia
manzese, jioni foleni inaanzia kona ya akiba saa 11
kufika Kimara saa 1 usiku au saa 2 usiku
anaekwenda moro amefika wa Mbezi usiseme je
Kibamba. TATIZO NINI?

BALA BALA??? Nafikiri ulimaanisha barabara!!?

Well kwa uelewa wangu mipango miji tuliyoirithi kutoka kwa wakoloni hatukuwahi kuifanyia update na hivyo kupelekea jiji/majiji yetu kukua bila mpangilio!!!

Kuzuia vihiace kuingia katikati ya jiji sio solution ya kuzuia msongamano wa barabara. Mfano mzuri upo kwa jirani zetu Wakenya ambao daladala/matatu wanavyoziita nyingi ni Hiace na ukiangalia kwa makini msongamano wa magari sio mkubwa kama ilivyo Bongo!. Jiji letu pamoja na kuwa na hali mbaya kwa feeder roads pia unahitaji kuwepo na Ring roads - hizi ni barabara ambazo zinaweza kutumika na watu kutoka sehemu moja iliyo nje ya jiji kwande upande mwingine wa jiji bila kupitia barabara kuu za ndani ya jiji!

Kuna umuhimu mkubwa wa kufanya maboresho ikiwa ni pamoja na kuongeza ukubwa wa barabara zetu haswa zile zinazoingia katikati ya Jiji.

Flyovers nafikiri igekuwa ni option nzuri sana iwapo tu barabara zetu pia zingekuwa kubwa kiasi cha kumudu traffic flow.

Ni ukweli usiopingika kwamba Serikali yetu pamoja na CITY PLANNERS walifulia na hii ndio itaendelea kuleta kero siku zote Tanzania.

Kwa wenye ufahamu hata India walipogundua wamefulia waliamua kujenga New Delhi ambako kumepangiliwa na kumepangika sio kama ilivyo Old Delhi...

Its high time pia serikali yetu ichukue maamuzi na ijenge mji uliopangika (prototype) na ndio uwe mji mkuu kibishara kwa nchi yetu...otherwise Traffic jams will always be the order of the day!!
 
Just kuuliza. Hivi ule mpango wa mabasi yaendayo kasi umeishia wapi????? Au mimi ndo nilielewa vibaya? Nasikia na hela watu walisha lipwa fidia katika kupisha ujenzi wa barabara. Naomba kufahamishwa.
 
Just kuuliza. Hivi ule mpango wa mabasi yaendayo kasi umeishia wapi????? Au mimi ndo nilielewa vibaya? Nasikia na hela watu walisha lipwa fidia katika kupisha ujenzi wa barabara. Naomba kufahamishwa.

Hii ilikuwa ni kati ya ile miradi isiyo na vision!! Ulaji ulaji ulaji..........

Kupanua barabara zipi watu walilipwa fidia? City center kumebanana hakuna hata barabara moja inaweza kupanuliwa hata kwa mita moja!! Maghorofa marefu ndo tunashindana kujenga ila kupangilia jiji wala hatuhusiki!!!!

Mabasi yaendayo kwa kasi... kwani yatakuwa yanakimbia huo mwendo kasi kwenye barabara gani au ndo tunataka kuanza kujena subways??

Hakuna jipya bongo...kila siku ni kero...leo afadhali ya jana!
 
Bongo maneno yamezidi, vitendo kwetu ni ndoto.Leo mabasi ya kasi, kesho treni za umeme,mwakani tunaondoa vipanya, ili mradi hatuna ukweli wa mwelekeo.Jamani tunakwenda wapi, hatuoni mifano ya miji ya wenzetu, viongozi wetu mnatembea hamuoni aibu jamani.Mtu mpaka unajiskia vibaya jamaa wakizungumza habari ya jiji letu.Aibu,aibu,aibu !!! tubadilike, lawama hizi viongozi wetu hawezi kuzikataa lazima wazibebe na warekebishe dira.
 
Back
Top Bottom