Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Kwanini wasisaidie hao maskini kwa pesa zao binafsi bila kusubiri kwenda ikulu? kama wao waliweza kuwa matajiri kwanini wengine wasiweze kuupata? hoja dhaifu kabisa kwa mtu anayejiita msomi kuwa na fikra duni kuwa kipimo cha ubora wa maisha ni utajiri! nani amewaambia kuwa watanzania wanataka kuwa matajiri? ina maana watu hao wasipotimiza ndoto zao za urais hawatawasaidia watanzania kuwa matajiri? Lwaitama atuambie, hadi sasa hao matajiri wamewasaidia maskini wangapi kuwa matajiri.
Utajiri ama tuseme ustawi kwa jamii nzima hautokani wa wananchi kugawiwa pesa (rejea milioni 50 kwa kila kijiji zinazo ahidiwa na Makufuli au mabilioni ya Kikwete ya sikumbuki mwaka gani lakini ni kati ya 2005-2015), bali jinsi ya ku-manage na ku-organize rasilimali zilizomo nchini ikiwa ni pamoja na raslimali watu kama wewe ziweze kunufaisha jamii nzima. Hapa hatuzungumzii ubilionea au umilionea, bali kupata huduma na mahitaji yote ya msingi kwa binadamu yaliyo bora. Kama ni elimu kwa wote, iwe elimu bora, kama ni maji safi yawe maji safi na salama na upatikanaji bora kwa wote, kama ni .. kila kitu kipatikane kwa wote na kiwe bora. Huo ndio utajiri wa jamii. Mwanafalsafa Lwaitama yuko sahihi kabisa. CHAGUA MABADILIKO, CHAGUA UKAWA, CHAGUA LOWASSA.
 
Wasaliti wakubwa wa taifa ndio hawa.
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1441217944.055329.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1441217944.055329.jpg
    11.6 KB · Views: 310
Naunga mkono hoja.Toka lini tajiri akawa na urafiki na maskini? Ni kama paka kuvaa tasbihi/rozali ya dagaa.

Tatizo umekariri na haukuwa ukitaka kujifunza ,unaamini tu bila ya kufikiri na upande wa pili na ni kama vile unaamini muuaji hawezi kuwa na huruma ataendelea kuua kila siku .
 
Tatizo umekariri na haukuwa ukitaka kujifunza ,unaamini tu bila ya kufikiri na upande wa pili na ni kama vile unaamini muuaji hawezi kuwa na huruma ataendelea kuua kila siku .

Sasa hapo hoja yako ni nini?
 
PhD holder anapimwa kwa uwezo wake wa kuchambua mambo siyo kwa ushabiki wa kipumbavu kama wa mwendawazimu Azaveli lwaitama. Mzee mzima anakosa busara anaongea pumba.shenzi sana.

Imekuwa ni kawaida sasa kwa wanachana wa CCM kuwatukana watu kwa sababu ya kuambiwa ukweli ,unalishushia heshima jukwaa jitahidi kujadili alichosema Dkt Azaver Lwaitama na acha kumshambulia yeye binafsi.

Ukichambua alichosema kwa hoja tutakuelewa ,sio kawaida kwa wananchi Watanzania kutukana namna hii...
 
Sio msomi tu, huyu ni mwanafalsafa!
Huu ndio mtazamo wa watanzania wote wanaotamani Tanzania mpya si kwa kungalia matumbo yetu leo hii tu, bali ustawi wa jamii nzima hususan kwa vizazi vya kesho na kesho kutwa.

Sifa namba moja ya kuwa mwanafalsafa ni kuwa na fikra na mitazamo isiyoegemea upande wowote, jiulize sifa hiyo anayo huyo unayesema ni mwanafalsafa? au wewe unaelewa mwanafalsafa ni nani?
 
Sasa hapo hoja yako ni nini?

Sio hoja yangu ni yako kwa sababu uliunga mkono hoja ya aliepingana na Dkt Lwaitama na ukasema na we we unaamini tajiri hawezi kumsaidia masikini...

Au umeshasahau mapema hii !!...
 
Sifa namba moja ya kuwa mwanafalsafa ni kuwa na fikra na mitazamo isiyoegemea upande wowote, jiulize sifa hiyo anayo huyo unayesema ni mwanafalsafa? au wewe unaelewa mwanafalsafa ni nani?

Ameegemea upande gani kwa mtazamo wako ?
 
Mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu Zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu Dr Slaa sasa...wote ni WASALITI wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha CCM madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa Chadema...kadi nilinunua Dar es Salaam makao makuu ya Chadema DSM na nilikabidhiwa na mwanangu Benson Kigaila Dodoma , mji mkuu wa Tanania , Jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Benson Kigaila ya kuwania Ubunge Doadoma Mjini... Benson Kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha Chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee Mtei na mwanagu Mbowe ambao, kama Ndg Lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia Watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha Prof Mohamed Babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....Tena Lowasa ndani ya UKAWA si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya CCM ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za Tanganyika na Zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na Friends of Slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji FRIENDS OF UKAWA NO more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na CCM ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa CCM madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya Rais wa Muungano na kuwepo Muungano wa serikali tatu...

Dr Slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu Zito na Prof Mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha CCM another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama

Ni kweli tumechoka na Ccm, pia tukubaliane kwamba makamanda tumevamiwa. Ukweli lazima uume na ukate. Tusishabikie kiulimwengu bali tukae chini tuone wapi tumekosea hadi wapiganaji wetu wanatutoka. Leo chadema unadhani itadumu na Lowasa na Sumaye. Koma hamna hata babako akifa akiwa ameanzisha kitu alieanzisha anajua zaidi. Tusiwe wayahudi wa kupindisha ukweli,nature reserves it's own path.
 
Hivi unafahamu maana ya uchaguzi kweli?.Ni lini katiba za vyama vya siasa vikaweka vifungu vya viongozi kutawala milele?.Alieanzisha Chadema anaweza asinufaike nayo kabisa ,hata haki hupiganiwa na wachache kwa maslahi ya wengi.Alikuja Dkt Slaa akaondoka na sasa amekuja Lowasa nae muda ukifika ataondoka watakuja wengine na wengine nao wataondoka ndio namna ya uongozi inavyotakiwa kuwa.
 
Niliwahi kusema,ACT ili iweje? For sure ni kuchelewesha mabadiliko.....Zitto na Dr Slaa wanajua wanachokifanya. Wanajidai kuwa na uchungu na Tanzania but in reality wameshapoteza mwelekeo. Dr Slaa alisema alihoji ujio wa Lowasa as an asset or libility,alitakiwa ajihoji kwanza yy wakati anaingia alikuja as an asset or libility? Aliingia tu na kupewa nafasi ya kugombea ubunge, mbona anapenda kusema uongo mzee huyu!!! Naweza kukubaliana na Lisu kuw athe issue here ni uraisi.
 
Yaani tajiri amsaidie masikini awe tajiri kama yeye.?

Kuna mahali ktk historian ya dunia maskini akamsaidia maskini mwenzie? Ndio Yale ya kwenda kwa MTU analalia ngozi anakaa kwenye tembe anakudanganya kukupa utajiri!!!!
 
Bukanga

Dr Gani Hajui Hata Kuvaa Na Hajipendi? Huyo Lwaitama Alichobakiza Tu Ni Kuokota Makopo Kwani Ana Kila Vimelea Vya Mtu Aliyechanganyikiwa. Labda Sasa Amehamia CHADEMA + UKAWA Ataacha Kunywa Gongo Na Kuunguza Ule Mdomo Wake Ambao Muda Wote Lips Zake Ni Nyekundu Tu. Hivi Ni Kwanini CHADEMA + UKAWA Mnapenda Sana Kukumbatia Mizinga Ya Nyuki Namna Hii?

Kumbe unajua mipasho
 
Last edited by a moderator:
bukanga

dr gani hajui hata kuvaa na hajipendi? Huyo lwaitama alichobakiza tu ni kuokota makopo kwani ana kila vimelea vya mtu aliyechanganyikiwa. Labda sasa amehamia chadema + ukawa ataacha kunywa gongo na kuunguza ule mdomo wake ambao muda wote lips zake ni nyekundu tu. Hivi ni kwanini chadema + ukawa mnapenda sana kukumbatia mizinga ya nyuki namna hii?

huo unaitwa wivu wa kike mkuu, toa mawazo yako bila matusi.
 
Na walaaniwe wote wanaosaliti harakati hizi
Mungu sio wa mchezo kiasi hicho. Laana hiyo itakugeukia wewe na wenzako ambao mmefanya matendo maovu kama Dr Slaa aluvyosema.sikutegemea chadema kuna uhuni kiasi hiki. Kweli kabisa chama hiki kinataka kushika dola kwa maisha ya usanii namna hii. Haiwezekani watanzania wameshaamka. Yaani Dr Slaa nahisi ametumwa na Mungu, Mungu anamtumia kuleta ujumbe kwetu.ili Tuzinduke.
Na nasema baada tu ya uchaguzi mkuu, tutamwomba Mbowe, na team yake yote ituachie chama tukiendeshe wenyewe na ikiwezekana Dr Slaa na Prof Lipumba warudi
 
Hivi unafahamu maana ya uchaguzi kweli?.Ni lini katiba za vyama vya siasa vikaweka vifungu vya viongozi kutawala milele?.Alieanzisha Chadema anaweza asinufaike nayo kabisa ,hata haki hupiganiwa na wachache kwa maslahi ya wengi.Alikuja Dkt Slaa akaondoka na sasa amekuja Lowasa nae muda ukifika ataondoka watakuja wengine na wengine nao wataondoka ndio namna ya uongozi inavyotakiwa kuwa.

Wewe nae kuwa na upana wa mawazo, chama lazima kiwe na mtu imara. Sasa kuna nani imara Chadema. Wote wachumia tumbo. Tafadhari maneno ya msingi Usilete kwenye ushabiki. La sivyo nipe miaka kadhaa kama chadema hakitakuwa kama NCCR ya mrema na hasa mamvi alishindwa.
 
Mtu imara bila taasisi imara ni ujinga pia ,kaungane na Mh Wasira katika utabiri maana inaonekana bado unayo ilimu ya mkoloni kichwani mwako.Unafikiri unavyofikiri ndio mwisho wa upeo wa watu wote.
 
Back
Top Bottom