Nimesoma maoni mengi, na naomba kuchangia bila ya nia ya kumkashifu Mtu au Dini hapa.
1. Nimesoma maoni ya ndoa baina ya mwislamu, mkristo na myahudi. Lakini, Mimi ni mwislamu na sijaoa katika Dini hizo Tatu.
2. Katika nchi Tajiri Hamna mume kuwa na Sauti au Nguvu kuliko mwamamme. Kila nchi inavyotajirika iwe ya kiislamu au kikristo , Ndio kina mama wanazidi kupata Haki sawa. Kwa hivyo, ni Vigumu kutegemea mwanamume awe na Sauti kubwa kuliko mwamamke nyumbani katika nchi Tajiri hasa Zenye demokrasia kamili.
3. Dini ni Imani yako, na Hamna binadamu anaweza kufuata masharti ya Dini hata asilimia 30 ya Sheria za Dini Yake. Dini ya kiislamu inakataza RIBA, pombe na inafuata sharia law. Kuna Mtu kakatwa mkono Tanzania baada ya kuiba? Basi Kama Tanzania haifuati waumini wao hawafuati Sheria za Quran. Pia kutumia dawa kuzuia Mimba na kondom ni marufuku kwa Sababu tunaingilia kazi ya Mungu. Katika maisha yakileo ni vigumu kuzaa bila ya kupanga, na mara nyingi wanawake wanafunga uzazi au wanatumia dawa, kinyume na sheria za dini yao.Kujiita mwislamu au mkristo peke Yake Haitoshi Kama hatuwezi Kuishi na Sheria Ngumu za Dini. Kwa Karne ya 21, kila nchi inavyotajirika, utakuta Imani za Dini zote zinapungua.
Nawakilisha.