sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 626
- 1,036
Salaam kwenu nyote.
Bima ya afya (NHIF) kwa watumishi wa umma inahudumia wategemezi watano mbali na mchangiaji mwenyewe. Wapo watu kadhaa ambao wameainishwa kuwa wanaweza kuwa wategemezi wa mwanachama mchangiaji endapo vigezo vitafikiwa.
Miongoni mwa wategemezi ni;mwenza, watoto na wazazi.
Jambo linalonitatiza kwa bima nikwamba,kwanini wasiruhusu mchangiaji kuweka wategemezi anaoona wanafaa muhimu tu wakidhi vigezo vya umri na idadi inayotakiwa?
Unakuta mimi, mwenza wangu pamoja na wazazi tupo kwenye utumishi hivyo hapo hakuna tegemezi wa bima.Kwanini nisipewe nafasi ya kumuweka mzazi au mtoto mwingine ambae ana uhitaji wa matibabu. Kumbuka pamoja namimi kutokuwa nawategemezi ila bado nachangia mfuko.
Maoni yangu nikwamba wachangiaji tupewe uhuru wakuweka watemezi muhimu tuzingatie vigezo vyote ikiwemo hivyo vya idadi ya wanufaika na umri wao(kama niwatoto)