kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,428
- 7,216
Chama cha Mapinduzi hua wanajizimia taa na kuwa gizani mara kwa mara.
Utaratibu wao wa kumteua Rais akitoka chama chao kuwa mwenyekiti wa chama chao safari hii wameikosea Demokrasia kwa kumchagua Samia kuwa Mwenyekiti.
Kwa kawaida CCM wana utaratibu wa kidemokrasia kumchagua mgombea urais wa chama chao. Pia wana desturi na sio katiba ya CCM kumteua Rais wa Jamhuri ikiwa anatoka chama chao kua mwenyekiti wa chama chao kumrithi mwenyekiti aliyemaliza mihula yake ya urais wa Jamhuri.
Rais Samia hakuwahi kuwa mgombea, kuteuliwa kuwa mgombea urais wala hakuwahi kugombea urais ila ameupata urais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano baada ya Rais aliyekuepo madarakani kufariki dunia.
Kwa maoni yangu aliyekua makamu mwenyekiti wa CCM bara ndiye alistahili kurithi uenyekiti wa CCM hadi kufanyika uchaguzi mwingine.
Kitendo cha kumpa kofia ya uenyekiti CCM mtu asiyekua na ridhaa ya wanachama naona kimekua hatari kabisa kwa msimamo wa chama kiitikadi na chama kuyumba kusimamia serikali ya chama chake.
Tangu ameingia Rais Samia tumeona mwelekeo tofauti kisiasa na kiuchumi utafikiri kumetokea mapinduzi au chama kipya kimeingia madarakani.