SoC01 Maonesho ya vyakula vya asili fursa mpya ya Utalii Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

G-empire-FP

Member
Feb 24, 2017
19
16
Utalii ni shughuli ya kibinadamu inayohusisha watu kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa shughuli mahsusi ikiwemo, mapumziko na starehe, biashara, mikutano au matukio mengine yeyote kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Sekta ya utalii inachangia kiasi kikubwa katika maendeleo ya uchumi hapa nchini. Utalii umegawanyika katika aina tofauti tofauti, hapa Tanzania utalii wa kutembelea mbuga za wanyama, kupanda milima na uwindaji wa wanyama pori ndio utalii ulioshika hatamu zaidi.

Ipo aina nyingine ya utalii ambayo bado haijapata nafasi na mafanikio makubwa hapa nchini licha ya jitihada nyingi za kuitangaza aina hii ya utalii nayo ni utalii wa utamaduni (Cultura Tourism). Utalii wa utamaduni ni moja ya aina ya utalii ya kitambo zaidi ambayo kwa Africa na Tanzania ingali bado ni changa.

Utalii wa utamaduni unahusisha mifumo ya maisha ya watu, historia ya maisha ya watu na maeneo yao, shehere za kitamaduni, vyakula, mali kale, maeneo ya kihistoria, dini za watu na mambo yote mengine yanayojaza maisha ya watu wa eneo flani. Aina hii ya utalii ndio inayowezesha jamii kuweza kunufaika moja kwa moja kupitia utalii.

Utalii huu wa utamaduni sio tu unahusisha kutembelea maeneo ya mali kale, miji ya kale mfano Kilwa, Bagamoyo, lakini pia inahusisha kutembelea maeneo ya vijijini na kushiriki katika shughuli za kitamaduni ikiwemo matambiko, sherehe za kitamaduni, vyakula vya asili na vinywaji vya asili, kutengeneza na kununua bidhaa za asili na kazi za sanaa za asili kama vinyago na michoro mbalimbali.

Aina hii ya utalii inasaidia sana katika kukuza na kuendeleza utamaduni wetu wa asili, kutunza na kuendeleza historia ya watu na maeneo yao na inachangia sana maendeleo ya watu moja kwa moja. Aina hii ya utalii imesaidia sana katika maeneo mengi duniani kuwezesha makundi ambayo hayakuwa na kazi za vipato kupata shughuli za kuweza kuwaingizia vipato hasa wanawake na vijana kwa kujiajiri kupitia utalii.

Kutokana na shughuli za kitalii Tanzania kushika hatamu zaidi katika mtandao wa maeneo ya utalii ya kaskazini (northern tourism circuit) aina hii ya utalii pia imeanza kupata nafasi kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Hata hivyo bado kama nchi hatujatengeneza mfumo rasmi wa namna ya kuvutia watalii wengi katika utalii wa aina hii kama vile ambavyo tunapata watalii wa mbuga za wanyama.

KUWEPO NA MSIMU WA MAONYESHO YA VYAKULA VYA ASILI
Tanzania bado hatujanufaika na utalii wa matukio na maonesha (Event Tourism) kwa namna ya kutosha na kuridhisha. Itakumbukwa Tanzania tuna maonesho mbalimbali ya kibiashara na maonyesho makubwa zaidi ni maonesho ya saba saba. Hatahivyo hatujaweza bado kuandaa maonesho ya makubwa ya kitamaduni ambayo yangeweza kuvutia watu mbalimbali kuja hapa nchini kushiriki maonesho hayo ili kukuza sekta ya utalii na kuongezea nchi mapato kupitia sekata ya Utalii.

Taarifa mbalimbali zinaonesha nchi nyingi dunia zinanufaika na utalii wa aina hii. Mfano Brazil huvutia maelfu ya watu kushiriki katika ngoma yao ya samba. Tanzania tunaweza kuanzisha maonyesho ya vyakula vyetu vya asili na kuandaa msimu wa maonyesho hayo ambayo ungepambwa na matukio mbalimbali ya kuonesha na kutangaza utamaduni wetu. Matukio hayo yangejumuisha ngoma zetu za asili, shughuli mbalimbali za kitamaduni na kuonesha mapishi yetu ya asili, kuonesha mavazi ya asili ya makabila mbalimbali Tanzania n.k.

Kuonesha na kuuza bidhaa mbalimbali za asili na kitamaduni, silaa zetu za jadi n.k. Licha ya kuvutia utalii maonesho haya yatachochea sana kukua kwa biashara na lingine kubwa yatasaidia kukuza fani ya upishi nchini. Mbali na hivyo maonesho haya yatakuwa chanzo kingine kipya na kikubwa cha mapato serikalini. Kushiriki Utalii wa maonesho ndio utalii rahisi zaidi kwa watu kuufanya kwani gharama za kushiriki ni nafuu na hivyo kuvutia watu wengi zaidi duniani.

Utalii huu unawavutia watu wengi kutokana na gharama za kushiriki kuwa nafuu kwani tozo nyingi zinazohusika katika utalii mfano wa mbuga za wanyama na kupanda Milima hazihusika katika utalii huu na hivyo kwa watu wote wanaopenda safari huvutiwa sana na utalii huu wa maonesho kwani huwapa fursa za kutembelea maeneo mbalimbali duniani.

UANDAAJI NA USIMAMIZI WA MAONESHO YA VYAKULA VYA ASILI
Tanzania ni nchi ya makabila mengi na tamaduni nyingi iliyojaliwa utajiri wa mapishi mengi ya asili na vyakula vya asili kuanzia Tanzania bara mpaka Zanzibar. Vyakula hivi hutofautiana maandalizi yake, sifa zake, mapishi yake, na hata ladha yake, hivyo kupitia Msimu wa Maonyesho y vyakula vya asili itakuwa ni fursa ya kipekee kuweza kupata sehemu moja ambayo mtu ataweza kuonja ladha ya vyakula vyote vya asili kutokea Tanzania, kuanzia LOSHORO YA KIMASAI, KIBULU NA KITALOLO CHA KICHAGA MPAKA UROJO WA ZANZIBAR.

Maandalizi ya sherehe hizi za kuonesha mapishi na vyakula vyetu vya asili itahusisha pia mjumuiko wa makabila mbalimbali na tamaduni mbalimbali. Katika kutoa nafasi ya jamii kushiriki kikamilifu sherehe hizi zaweza kuratibiwa kuanzia ngazi ya Mikoa. Kupitia maonesho ya mikoa ambayo pia yatakuwa sehemu ya msimu wa maonesho ya vyakua vyetu, tungeweza kuratibu zoezi la kupata washindi ambao wangeshiriki katika maonesho ya kitaifa. Maonesho haya yanaweza kuandaliwa na kuratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania chini ya Wizara ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana na ofisi za ya Mkuu wa mkoa.

Katika kuleta mvuto zaidi wa maonesho haya, mialiko ya wapishi vya vyakula mbalimbali vya asili kutoka mataifa mbalimbali dunia inaweza kutolewa kimkakati kuweza kuvutia watu kutoka katika mataifa hayo kushawishika kuja kushiriki katika maonesho yetu wakijua sio tu watapata ladha ya vyakula vyetu ila hata vyao vitakuwepo.

Vile vile tunaweza kuwaalika wapishi maarufu duniani kuweza kunogesha zaidi maonesho yetu na zaidi sana pia kushawishi na kuaalika watu maarufu na mashuhuri duniani kuja kushiriki katika msimu wetu wa maonyesho ya vyakula vyetu vya asili kama njia ya kuyatangaza maonesho yetu na kuyapa hadhi na upekee.

FAIDA ZA MAONESHO HAYA
Zipo faida nyingi za kuanzishwa kwa maonesho hapa nchini ikiwemo;
  • Kutangaza na kuendeleza utamaduni wetu wa chakula
  • Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wetu wa chakula
  • Kuvutia uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali
  • Serikali kupata chanzo kipya na kikubwa cha mapato
  • Kutangaza zaidi utalii wetu na nchi yetu kimataifa
  • Kuinua fani ya mapishi na fahari yake nchini
  • Kuzalisha ajira mpya nchini na hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira
 
Nyama choma festival ilikuwa inafanya hicho unachozungumzia ...figisu za makonda na serikali ya ccm vikamuondoa kwenye reli dada wa watu
nakubaliana na wewe nyama choma festival ilikuwa idea nzuri, ila ni tofauti na hii idea nayozungumzia hapa in term of Approach na management, tunayo fursa kubwa sana hapa kama nchi kitalii.

naomba kura yako mkuu
 
Wazo zuri sana inatakiwa kufika mpaka kwa waziri wa utalii tunahitaji vijana kama hawa 1000 tu tutakua mbaaaaali sana 2025 🤝🏾🇹🇿🤔
 
Lets share Andiko hili kwa wingi sana wadau, kura yako pia ni ya muhimu sana and much appreciated 🙏
 
Kura zinapigwa wapi
Angalia kiambatanisho hiki kaka kujua namna ya kupiga kura

Screenshot_20210810-230316.jpg
 
Utalii ni shughuli ya kibinadamu inayohusisha watu kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa shughuli mahsusi ikiwemo, mapumziko na starehe, biashara, mikutano au matukio mengine yeyote kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Sekta ya utalii inachangia kiasi kikubwa katika maendeleo ya uchumi hapa nchini. Utalii umegawanyika katika aina tofauti tofauti, hapa Tanzania utalii wa kutembelea mbuga za wanyama, kupanda milima na uwindaji wa wanyama pori ndio utalii ulioshika hatamu zaidi.

Ipo aina nyingine ya utalii ambayo bado haijapata nafasi na mafanikio makubwa hapa nchini licha ya jitihada nyingi za kuitangaza aina hii ya utalii nayo ni utalii wa utamaduni (Cultura Tourism). Utalii wa utamaduni ni moja ya aina ya utalii ya kitambo zaidi ambayo kwa Africa na Tanzania ingali bado ni changa. Utalii wa utamaduni unahusisha mifumo ya maisha ya watu, historia ya maisha ya watu na maeneo yao, shehere za kitamaduni, vyakula, mali kale, maeneo ya kihistoria, dini za watu na mambo yote mengine yanayojaza maisha ya watu wa eneo flani. Aina hii ya utalii ndio inayowezesha jamii kuweza kunufaika moja kwa moja kupitia utalii. Utalii huu wa utamaduni sio tu unahusisha kutembelea maeneo ya mali kale, miji ya kale mfano Kilwa, Bagamoyo, lakini pia inahusisha kutembelea maeneo ya vijijini na kushiriki katika shughuli za kitamaduni ikiwemo matambiko, sherehe za kitamaduni, vyakula vya asili na vinywaji vya asili, kutengeneza na kununua bidhaa za asili na kazi za sanaa za asili kama vinyago na michoro mbalimbali.

Aina hii ya utalii inasaidia sana katika kukuza na kuendeleza utamaduni wetu wa asili, kutunza na kuendeleza historia ya watu na maeneo yao na inachangia sana maendeleo ya watu moja kwa moja. Aina hii ya utalii imesaidia sana katika maeneo mengi duniani kuwezesha makundi ambayo hayakuwa na kazi za vipato kupata shughuli za kuweza kuwaingizia vipato hasa wanawake na vijana kwa kujiajiri kupitia utalii. Kutokana na shughuli za kitalii Tanzania kushika hatamu zaidi katika mtandao wa maeneo ya utalii ya kaskazini (northern tourism circuit) aina hii ya utalii pia imeanza kupata nafasi kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Hata hivyo bado kama nchi hatujatengeneza mfumo rasmi wa namna ya kuvutia watalii wengi katika utalii wa aina hii kama vile ambavyo tunapata watalii wa mbuga za wanyama.

KUWEPO NA MSIMU WA MAONYESHO YA VYAKULA VYA ASILI
Tanzania bado hatujanufaika na utalii wa matukio na maonesha (Event Tourism) kwa namna ya kutosha na kuridhisha. Itakumbukwa Tanzania tuna maonesho mbalimbali ya kibiashara na maonyesho makubwa zaidi ni maonesho ya saba saba. Hatahivyo hatujaweza bado kuandaa maonesho ya makubwa ya kitamaduni ambayo yangeweza kuvutia watu mbalimbali kuja hapa nchini kushiriki maonesho hayo ili kukuza sekta ya utalii na kuongezea nchi mapato kupitia sekata ya Utalii. Taarifa mbalimbali zinaonesha nchi nyingi dunia zinanufaika na utalii wa aina hii. Mfano Brazil huvutia maelfu ya watu kushiriki katika ngoma yao ya samba. Tanzania tunaweza kuanzisha maonyesho ya vyakula vyetu vya asili na kuandaa msimu wa maonyesho hayo ambayo ungepambwa na matukio mbalimbali ya kuonesha na kutangaza utamaduni wetu. Matukio hayo yangejumuisha ngoma zetu za asili, shughuli mbalimbali za kitamaduni na kuonesha mapishi yetu ya asili, kuonesha mavazi ya asili ya makabila mbalimbali Tanzania n.k. Kuonesha na kuuza bidhaa mbalimbali za asili na kitamaduni, silaa zetu za jadi n.k. Licha ya kuvutia utalii maonesho haya yatachochea sana kukua kwa biashara na lingine kubwa yatasaidia kukuza fani ya upishi nchini. Mbali na hivyo maonesho haya yatakuwa chanzo kingine kipya na kikubwa cha mapato serikalini. Kushiriki Utalii wa maonesho ndio utalii rahisi zaidi kwa watu kuufanya kwani gharama za kushiriki ni nafuu na hivyo kuvutia watu wengi zaidi duniani. Utalii huu unawavutia watu wengi kutokana na gharama za kushiriki kuwa nafuu kwani tozo nyingi zinazohusika katika utalii mfano wa mbuga za wanyama na kupanda Milima hazihusika katika utalii huu na hivyo kwa watu wote wanaopenda safari huvutiwa sana na utalii huu wa maonesho kwani huwapa fursa za kutembelea maeneo mbalimbali duniani.

UANDAAJI NA USIMAMIZI WA MAONESHO YA VYAKULA VYA ASILI
Tanzania ni nchi ya makabila mengi na tamaduni nyingi iliyojaliwa utajiri wa mapishi mengi ya asili na vyakula vya asili kuanzia Tanzania bara mpaka Zanzibar. Vyakula hivi hutofautiana maandalizi yake, sifa zake, mapishi yake, na hata ladha yake, hivyo kupitia Msimu wa Maonyesho y vyakula vya asili itakuwa ni fursa ya kipekee kuweza kupata sehemu moja ambayo mtu ataweza kuonja ladha ya vyakula vyote vya asili kutokea Tanzania, kuanzia LOSHORO YA KIMASAI, KIBULU NA KITALOLO CHA KICHAGA MPAKA UROJO WA ZANZIBAR. Maandalizi ya sherehe hizi za kuonesha mapishi na vyakula vyetu vya asili itahusisha pia mjumuiko wa makabila mbalimbali na tamaduni mbalimbali. Katika kutoa nafasi ya jamii kushiriki kikamilifu sherehe hizi zaweza kuratibiwa kuanzia ngazi ya Mikoa. Kupitia maonesho ya mikoa ambayo pia yatakuwa sehemu ya msimu wa maonesho ya vyakua vyetu, tungeweza kuratibu zoezi la kupata washindi ambao wangeshiriki katika maonesho ya kitaifa. Maonesho haya yanaweza kuandaliwa na kuratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania chini ya Wizara ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana na ofisi za ya Mkuu wa mkoa.

Katika kuleta mvuto zaidi wa maonesho haya, mialiko ya wapishi vya vyakula mbalimbali vya asili kutoka mataifa mbalimbali dunia inaweza kutolewa kimkakati kuweza kuvutia watu kutoka katika mataifa hayo kushawishika kuja kushiriki katika maonesho yetu wakijua sio tu watapata ladha ya vyakula vyetu ila hata vyao vitakuwepo. Vile vile tunaweza kuwaalika wapishi maarufu duniani kuweza kunogesha zaidi maonesho yetu na zaidi sana pia kushawishi na kuaalika watu maarufu na mashuhuri duniani kuja kushiriki katika msimu wetu wa maonyesho ya vyakula vyetu vya asili kama njia ya kuyatangaza maonesho yetu na kuyapa hadhi na upekee.

FAIDA ZA MAONESHO HAYA
Zipo faida nyingi za kuanzishwa kwa maonesho hapa nchini ikiwemo;
  • Kutangaza na kuendeleza utamaduni wetu wa chakula
  • Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wetu wa chakula
  • Kuvutia uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali
  • Serikali kupata chanzo kipya na kikubwa cha mapato
  • Kutangaza zaidi utalii wetu na nchi yetu kimataifa
  • Kuinua fani ya mapishi na fahari yake nchini
  • Kuzalisha ajira mpya nchini na hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira
Jambo lolote huanzia katika mawazo, na mawazo bora ndio huleta mabadiliko chanya katika jamii. Karibu katika kutafakari na mimi wazo hii kwa mazingir yetu, Usisahau kunipigia kura. Kura yako ni muhimu kwangu na naithamini sana🙏💯
 
Mpango wa Serikali na shabaha ya serikali ni kufikia mwaka 2025, kama nchi tuwe tunapokea watalii Million Tano kwa mwaka kuja kutembelea nchi yetu. Ikiwa hatutaongeza vivutio na tukabaki tukitegemea utalii wa mbuga na milima peke yake hatutaweza kufikia shabaha hii iliyo na manufaa mengi kwa taifa letu. Ndio maana ni muhimu kuja na mawazo mapya ya namna ya kuhakikisha tunaipa sekta ya utalii uhai zaidi na shughuli zaidi za kuvutia watu wengi dunia kuja Tanzania. Wazo la kuwa msimu wa maonesho ya utalii ni wazo sahihi katika muda sahihi.

Karibuni tujadiliane na kusukuma wazo hili mbele wadau, usisahau kupigia kura wazo hili.

Natanguliza shukrani kwa kura yako 🙏
 
Nawashukuru Wote mnaoendelea kuunga mkopo wazo hili na kulipigia kura, naomba wale ambao bado hawajslipigia kura walipigie kura wazo hili, kwani ushindi wa wazo hili ni kulisukuma mbele na kulipa nguvu katika vyombo vya maamuzi vya kiserikali ili liweze kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu.

Kwa pamoja tunaweza.
 
Utalii ni shughuli ya kibinadamu inayohusisha watu kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa shughuli mahsusi ikiwemo, mapumziko na starehe, biashara, mikutano au matukio mengine yeyote kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Sekta ya utalii inachangia kiasi kikubwa katika maendeleo ya uchumi hapa nchini. Utalii umegawanyika katika aina tofauti tofauti, hapa Tanzania utalii wa kutembelea mbuga za wanyama, kupanda milima na uwindaji wa wanyama pori ndio utalii ulioshika hatamu zaidi.

Ipo aina nyingine ya utalii ambayo bado haijapata nafasi na mafanikio makubwa hapa nchini licha ya jitihada nyingi za kuitangaza aina hii ya utalii nayo ni utalii wa utamaduni (Cultura Tourism). Utalii wa utamaduni ni moja ya aina ya utalii ya kitambo zaidi ambayo kwa Africa na Tanzania ingali bado ni changa. Utalii wa utamaduni unahusisha mifumo ya maisha ya watu, historia ya maisha ya watu na maeneo yao, shehere za kitamaduni, vyakula, mali kale, maeneo ya kihistoria, dini za watu na mambo yote mengine yanayojaza maisha ya watu wa eneo flani. Aina hii ya utalii ndio inayowezesha jamii kuweza kunufaika moja kwa moja kupitia utalii. Utalii huu wa utamaduni sio tu unahusisha kutembelea maeneo ya mali kale, miji ya kale mfano Kilwa, Bagamoyo, lakini pia inahusisha kutembelea maeneo ya vijijini na kushiriki katika shughuli za kitamaduni ikiwemo matambiko, sherehe za kitamaduni, vyakula vya asili na vinywaji vya asili, kutengeneza na kununua bidhaa za asili na kazi za sanaa za asili kama vinyago na michoro mbalimbali.

Aina hii ya utalii inasaidia sana katika kukuza na kuendeleza utamaduni wetu wa asili, kutunza na kuendeleza historia ya watu na maeneo yao na inachangia sana maendeleo ya watu moja kwa moja. Aina hii ya utalii imesaidia sana katika maeneo mengi duniani kuwezesha makundi ambayo hayakuwa na kazi za vipato kupata shughuli za kuweza kuwaingizia vipato hasa wanawake na vijana kwa kujiajiri kupitia utalii. Kutokana na shughuli za kitalii Tanzania kushika hatamu zaidi katika mtandao wa maeneo ya utalii ya kaskazini (northern tourism circuit) aina hii ya utalii pia imeanza kupata nafasi kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Hata hivyo bado kama nchi hatujatengeneza mfumo rasmi wa namna ya kuvutia watalii wengi katika utalii wa aina hii kama vile ambavyo tunapata watalii wa mbuga za wanyama.

KUWEPO NA MSIMU WA MAONYESHO YA VYAKULA VYA ASILI
Tanzania bado hatujanufaika na utalii wa matukio na maonesha (Event Tourism) kwa namna ya kutosha na kuridhisha. Itakumbukwa Tanzania tuna maonesho mbalimbali ya kibiashara na maonyesho makubwa zaidi ni maonesho ya saba saba. Hatahivyo hatujaweza bado kuandaa maonesho ya makubwa ya kitamaduni ambayo yangeweza kuvutia watu mbalimbali kuja hapa nchini kushiriki maonesho hayo ili kukuza sekta ya utalii na kuongezea nchi mapato kupitia sekata ya Utalii. Taarifa mbalimbali zinaonesha nchi nyingi dunia zinanufaika na utalii wa aina hii. Mfano Brazil huvutia maelfu ya watu kushiriki katika ngoma yao ya samba. Tanzania tunaweza kuanzisha maonyesho ya vyakula vyetu vya asili na kuandaa msimu wa maonyesho hayo ambayo ungepambwa na matukio mbalimbali ya kuonesha na kutangaza utamaduni wetu. Matukio hayo yangejumuisha ngoma zetu za asili, shughuli mbalimbali za kitamaduni na kuonesha mapishi yetu ya asili, kuonesha mavazi ya asili ya makabila mbalimbali Tanzania n.k. Kuonesha na kuuza bidhaa mbalimbali za asili na kitamaduni, silaa zetu za jadi n.k. Licha ya kuvutia utalii maonesho haya yatachochea sana kukua kwa biashara na lingine kubwa yatasaidia kukuza fani ya upishi nchini. Mbali na hivyo maonesho haya yatakuwa chanzo kingine kipya na kikubwa cha mapato serikalini. Kushiriki Utalii wa maonesho ndio utalii rahisi zaidi kwa watu kuufanya kwani gharama za kushiriki ni nafuu na hivyo kuvutia watu wengi zaidi duniani. Utalii huu unawavutia watu wengi kutokana na gharama za kushiriki kuwa nafuu kwani tozo nyingi zinazohusika katika utalii mfano wa mbuga za wanyama na kupanda Milima hazihusika katika utalii huu na hivyo kwa watu wote wanaopenda safari huvutiwa sana na utalii huu wa maonesho kwani huwapa fursa za kutembelea maeneo mbalimbali duniani.

UANDAAJI NA USIMAMIZI WA MAONESHO YA VYAKULA VYA ASILI
Tanzania ni nchi ya makabila mengi na tamaduni nyingi iliyojaliwa utajiri wa mapishi mengi ya asili na vyakula vya asili kuanzia Tanzania bara mpaka Zanzibar. Vyakula hivi hutofautiana maandalizi yake, sifa zake, mapishi yake, na hata ladha yake, hivyo kupitia Msimu wa Maonyesho y vyakula vya asili itakuwa ni fursa ya kipekee kuweza kupata sehemu moja ambayo mtu ataweza kuonja ladha ya vyakula vyote vya asili kutokea Tanzania, kuanzia LOSHORO YA KIMASAI, KIBULU NA KITALOLO CHA KICHAGA MPAKA UROJO WA ZANZIBAR. Maandalizi ya sherehe hizi za kuonesha mapishi na vyakula vyetu vya asili itahusisha pia mjumuiko wa makabila mbalimbali na tamaduni mbalimbali. Katika kutoa nafasi ya jamii kushiriki kikamilifu sherehe hizi zaweza kuratibiwa kuanzia ngazi ya Mikoa. Kupitia maonesho ya mikoa ambayo pia yatakuwa sehemu ya msimu wa maonesho ya vyakua vyetu, tungeweza kuratibu zoezi la kupata washindi ambao wangeshiriki katika maonesho ya kitaifa. Maonesho haya yanaweza kuandaliwa na kuratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania chini ya Wizara ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana na ofisi za ya Mkuu wa mkoa.

Katika kuleta mvuto zaidi wa maonesho haya, mialiko ya wapishi vya vyakula mbalimbali vya asili kutoka mataifa mbalimbali dunia inaweza kutolewa kimkakati kuweza kuvutia watu kutoka katika mataifa hayo kushawishika kuja kushiriki katika maonesho yetu wakijua sio tu watapata ladha ya vyakula vyetu ila hata vyao vitakuwepo. Vile vile tunaweza kuwaalika wapishi maarufu duniani kuweza kunogesha zaidi maonesho yetu na zaidi sana pia kushawishi na kuaalika watu maarufu na mashuhuri duniani kuja kushiriki katika msimu wetu wa maonyesho ya vyakula vyetu vya asili kama njia ya kuyatangaza maonesho yetu na kuyapa hadhi na upekee.

FAIDA ZA MAONESHO HAYA
Zipo faida nyingi za kuanzishwa kwa maonesho hapa nchini ikiwemo;
  • Kutangaza na kuendeleza utamaduni wetu wa chakula
  • Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wetu wa chakula
  • Kuvutia uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali
  • Serikali kupata chanzo kipya na kikubwa cha mapato
  • Kutangaza zaidi utalii wetu na nchi yetu kimataifa
  • Kuinua fani ya mapishi na fahari yake nchini
  • Kuzalisha ajira mpya nchini na hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira
Chakula ni fahari ya jamii yeyote na nchi yeyote dunia. Ni moja ya utambulisho muhimu wa Tamaduni ya Jamii flani na nchi kwa ujumla. Hivi karibuni nchini kwetu tumeshuhudia Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akishiriki kutengeneza Filamu maalumu na mahsusi kabisa kwa ajili ya kuonesha fahari za Tanzania duniani kwa Lengo mahsusi la kuiuza Tanzania Kitalii na kuwavutia wawekezaji mbalimbali kujakuwekeza katika fursa za kibiashara hapa Tanzania. jambo la bahati mbaya, katika Filamu hii muhimu sana, na itakayorushwa katika kipindi maalumu cha "ROYAL TOUR" hakuna sehemu Mhe. Rais ataonekana akila chakula chenye asili ya Tanzania. Hakuna sehemu itaonekana maandalizi ya vyakula vyetu, asili yake, historia ya vyakula hivyo na faida ya vyakula vyetu. Hii ingekuwa Segment muhimu mno katika filamu ya aina hii, ndio maana naamini kuanzishwa kwa maonesho ya vyakula vya asili vya Tanzania ni urithi mwingine ambao sio tu utavutia watalii wengi duniani kuja Tanzania kujifunza mapishi yetu, vyakula vyetu na historia yetu bali pia itachangia mabadiliko makubwa ya sekta ya Utalii na kuongeza Pato kwa Serikali.

Nakukaribisha kusoma andiko Hili, na pia naomba kura yako kwa Andiko Hili.
 
Back
Top Bottom