Maombi yamepokelewa Secretariat ya Ajira, kwanini hadi sasa hakuna mrejesho mwingine?

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,985
2,770
Kwenu Secretariat ya Ajira. Mliweka Nafasi za kazi za MDA na LGA hapo July 2022. Wasaka Ajira tukajitosa kuomba Tena Kwa Gharama kubwa na Sifa mlizotaka zipo. Mrejesho toka kwenu ikawa Received.

Mpaka Leo hakuna jibu lingine la maybe not shortlisted au shortlisted au nafasi hii imechukuliwa Watu wa akiba. Tunasubiri majibu toka kwenu hakuna. Kinachotokea ni kuona tuu wahitimu wa 2021 na 2020 wakiitwa Kazini.

Naomba Muwe Wazi Ili tusihangaike kusubiria majibu ambayo hayatakaa yaje. Laiti mngalijua Mtaani miaka 8 bila formal Ajira kulivyo kugumu.
 
Kwenu Secretariat ya Ajira. Mliweka Nafasi za kazi za MDA na LGA hapo July 2022. Wasaka Ajira tukajitosa kuomba Tena Kwa Gharama kubwa na Sifa mlizotaka zipo...
Secretariat ya ajira ni jipu huwa wanatangaza nafasi sijui hawakuwa tayari, kwanini wanatangaza nafasi kama hawako tayari mtu anaomba nafasi toka mwezi wa nne mpaka leo hata hawajaita kwenda kwenye usaili
 
Kwa kweli mambo za PSRS Sasa ni ushuzi tu.. just imagine unaomba kazi siku unaitwa Usaili miezi 10 ago Hadi unasahau kazi ilihusu nn
 
Wanatoa ajira kwa wote mimi kuna watu nawafahamu wamekaa kitaa muda na wame pata ajira so kuwa mvumilv


Ni kweli mkuu. Ila subira ina mwisho wake. Njaa haiezi kusubiri.

Mi nadhani wangekua wanawasiliana na wateja wao (wasaka ajira)
Kwa maana ya kutoa public taratibu za ufanyaji kazi wao

Mfano waseme kabisa kuwa ukiapply basi tegemea kuitwa usaili baada ya mwezi mmoja

Ukifanya usaili tegemea kuitwa kazini baada ya mwezi mmoja

Na kisha kweli huo muda uzingatiwe.

Na kama kuna shida bas waseme kuna shida imetokea muda wa majibu umesogezwa mbele


Changamoto unakuta mtu hujui siku ya kuitwa usaili ni lini au placement ya kazi ni lini. Unakaa kwa mashaka mashaka na mambo mengine huwezi kufanya

Mfano unakuta inabid mtu ahame mkoa kutafuta riziki lakin anafikiria hivi akihama au akianzisha ishu flan alafu muda mdogo kaitwa usaili au placement unaacha hiki unashika hiki.


Mawasiliano muhimu sana


Mfano ukifika ofisi flani au hospitali kisha mnapanga foleni masaa yanaenda kama mfanyakaz wa ofis asipotoa taarifa watu wataanza kupanik hasira na kuchoka

Ila akija mwakilishi akasema labda daktar kapata dharura anakuja baada ya masaa mawili au network ya benk imezingua itarud baada ya masaa matatu bas angalau wa kwenda kula ataenda wa kusubiri atasubiri na hakutakuwa na sintofahamu ya kinachoondelea


Yote ya yote ndo nchi yetu ilivo inabd watu wavumilie...wakiamua mda wanaona unafaa basi watatoa hayo majina.
 
Watu walioomba tra Deadline ya mwezi wa nne wakaanza kutia misuli kujiandaaa mpk Sasa hv kmyaa
 
Tumeshawazoea Hawa jamaa hwana jipya so. Jiandae tu na madesa yao maana siku wakiyaachia majina hawakupi hata wiki ya kujiandaa
 
Back
Top Bottom