Majibu ya hoja za wadau – oktoba, 2012 -tume ya ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya hoja za wadau – oktoba, 2012 -tume ya ajira

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Penguin-1, Oct 10, 2012.

 1. Penguin-1

  Penguin-1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [h=3][​IMG]1. Mimi ni Mtanzania, nimekuwa nikiisikia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Je, naweza kufahamishwa majukumu ya Sekretarieti ya Ajira kwa ujumla ni yapi?[/h][h=3]JIBU
  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ina majukumu yafuatayo:-
  a) Kutafuta wataalam wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuhifadhi taarifa za wataalam;
  b) Kutangaza nafasi wazi za kazi zinazojitokeza katika Utumishi wa Umma;
  c) Kuhusisha wataalam maalum ili kushirikiana nao kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji;
  d) Kuwashauri waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira;
  e) Kuandaa orodha ya wahitimu wa Vyuo na wataalam weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea za ujazaji wa nafasi za ajira katika Utumishi wa Umma; na
  f) Kutekeleza majukumu mengine kadri itakavyoelekezwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma

  SWALI

  2. Je, mmeshawahi kukutana na Waombaji wa fursa za ajira ambao wamegushi vyeti? Kama ni ndio je, mnawachukulia hatua gani waombaji kama hao?

  JIBU
  Moja ya changamoto kubwa inayoikabili Sekretarieti ya Ajira kwa sasa ni udanganyifu wa sifa kwa baadhi ya Waombaji. Hatua zinazochukuliwa ili kutatua changamoto hiyo ni hizi zifuatazo:-
  a) Kuimarisha mifumo ya kiutendaji ili kupunguza na kuondoa udanganyifu unaofanywa na baadhi ya waombaji.
  b) Pili, Sekretarieti ya Ajira imekuwa ikivichukua vyeti hivyo vya kughushi na kuviwasilisha katika mamlaka husika ambako waombaji walidai kuvipata mfano Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Vyuo vya mafunzo ya ufundi (VETA) au Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na taasisi nyinginezo ili kuvishikilia kwa ushahidi kwa ajili ya hatua za kisheria vitakapohitajika.
  c) Tatu, ni kuwaondoa katika orodha ya wasailiwa pale tunapojiridhisha kuwa vyeti walivyotumia kuomba fursa ya ajira si halali;
  d) Nne, tunaendelea na mchakato wa kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwapeleka mahakamani kwa kushirikiana na mamlaka husika ili kukabiliana na tatizo hili katika utumishi wa umma.
  e) Tano, tunaendelea kutoa elimu kwa umma ili waelewe kuwa kudanganya au kutumia vyeti ambavyo si vyako ama vya kughushi ni kosa la jinai linaloweza kumfikishwa mwombaji katika vyombo vya sheria na itakapothibitika ametenda kosa hilo mtuhumiwa anaweza kufungwa jela, kulipa faini, kupoteza kazi kama alishaipata. Kwa mfano kulingana na Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mtu akibainika ameghushi cheti cha baraza hilo kwa lengo la kupata ajira anaweza kupelekwa jela kw kifungo kisichozidi miaka ishirini (20) au kutozwa faini isiyozidi shilingi mlioni moja (1,000,000) au adhabu zote mbili kwa pamoja.

  SWALI
  3. Nimesikia Sekretarieti ya Ajira imeanzisha “Database” yaani kanzidata je, naweza kujua namna inavyotumika hivi sasa hiyo kanzidata yenu?

  JIBU
  i. Ni kweli Sekretarieti ya Ajira imeanzisha mfumo wa kuhifadhi taarifa kanzidata (data base) za wataalam wenye ujuzi maalum kulingana na vigezo na sifa zinazotakiwa kwa kada mbalimbali Serikalini.
  ii. Sekretarieti ya Ajira kwa mfano, kwa mwaka wa fedha 2011 hadi Septemba, 2012 imeweza kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji 783 waliofaulu saili mbalimbali kutoka katika kanzidata (data base) kwa Waajiri wapatao 134 wa Taasisi za umma nchini.
  iii. Mbali na hilo kanzidata ya Sekretarieti ya Ajira imekuwa ikihifadhi pia orodha ya Wahitimu kutoka Vyuo mbalimbali hapa nchini, ambapo mpaka sasa imeweza kuhifadhi jumla ya wahitimu elfu ishirini na moja, mia sita, tisini na moja (21,691) kutoka Vyuo Vikuu kumi na moja (11) kwa lengo la kurahisisha rejea na ujazaji wa nafasi wazi za ajira katika Utumishi wa Umma. Aidha, inaendelea kukusanya takwimu hizi ili kuboresha taarifa zake siku hadi siku kadri zinavyopatikana.[/h][TABLE="width: 671"]
  [TR]
  [TD][h=4]NA.[/h][/TD]
  [TD][h=4]JINA LA CHUO[/h][/TD]
  [TD][h=4]2008[/h][/TD]
  [TD][h=4]2009[/h][/TD]
  [TD][h=4]2010[/h][/TD]
  [TD][h=4]2011[/h][/TD]
  [TD][h=4]JUMLA[/h][h=4]KWA[/h][h=4]CHUO[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]1.[/h][/TD]
  [TD][h=4]MZUMBE UNIVERSITY (MU)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]1605[/h][/TD]
  [TD][h=4]1887[/h][/TD]
  [TD][h=4]2595[/h][/TD]
  [TD][h=4]6087[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]2.[/h][/TD]
  [TD][h=4]MOSHI UNIVERSITY COLLEGE FOR COOPERATIVE AND BUSINESS STUDIES(MUCCOBS)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]578[/h][/TD]
  [TD][h=4]900[/h][/TD]
  [TD][h=4]1454[/h][/TD]
  [TD][h=4]2932[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]3.[/h][/TD]
  [TD][h=4]INSTITUTE OF ACCOUNTANCY ARUSHA (IAA)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]933[/h][/TD]
  [TD][h=4]1209[/h][/TD]
  [TD][h=4]1237[/h][/TD]
  [TD][h=4]3379[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]4.[/h][/TD]
  [TD][h=4]HUBERT KIRUKI MEMORIAL UNIVERSITY (HKMU)[/h][/TD]
  [TD][h=4]107[/h][/TD]
  [TD][h=4]120[/h][/TD]
  [TD][h=4]139[/h][/TD]
  [TD][h=4]188[/h][/TD]
  [TD][h=4]554[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]5.[/h][/TD]
  [TD][h=4]KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY (KIU)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]4[/h][/TD]
  [TD][h=4]82[/h][/TD]
  [TD][h=4]86[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]6.[/h][/TD]
  [TD][h=4]MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO (MUM)[/h][/TD]
  [TD][h=4]158[/h][/TD]
  [TD][h=4]155[/h][/TD]
  [TD][h=4]310[/h][/TD]
  [TD][h=4]277[/h][/TD]
  [TD][h=4]900[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]7.[/h][/TD]
  [TD][h=4]THE AGA KHAN UNIVERSITY (AKU)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]162[/h][/TD]
  [TD][h=4]117[/h][/TD]
  [TD][h=4]149[/h][/TD]
  [TD][h=4]428[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]8.[/h][/TD]
  [TD][h=4]UNIVERSITY OF ARUSHA (UOA)[/h][/TD]
  [TD][h=4]108[/h][/TD]
  [TD][h=4]336[/h][/TD]
  [TD][h=4]428[/h][/TD]
  [TD][h=4]308[/h][/TD]
  [TD][h=4]1180[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]9.[/h][/TD]
  [TD][h=4]INTERNATIONAL MEDICAL AND TECHNOLOGICAL UNIVERSITY (IMTU)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]109[/h][/TD]
  [TD][h=4]138[/h][/TD]
  [TD][h=4]168[/h][/TD]
  [TD][h=4]415[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]10.[/h][/TD]
  [TD][h=4]OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA (OUT)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]468[/h][/TD]
  [TD][h=4]1020[/h][/TD]
  [TD][h=4]2670[/h][/TD]
  [TD][h=4]4158[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][h=2]11.[/h][/TD]
  [TD][h=4]TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU)[/h][/TD]
  [TD][/TD]
  [TD][h=4]149[/h][/TD]
  [TD][h=4]611[/h][/TD]
  [TD][h=4]812[/h][/TD]
  [TD][h=4]1572[/h][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 2"][h=4]JUMLA YA WAHITIMU KWA MWAKA[/h][/TD]
  [TD][h=4]373[/h][/TD]
  [TD][h=4]4615[/h][/TD]
  [TD][h=4]6763[/h][/TD]
  [TD][h=4]9940[/h][/TD]
  [TD][h=4]21691[/h][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [h=3]SWALI
  4. Je, mnaweza kuelezea umma njia mnayotumia kuchuja waombaji wa nafasi za kazi na kubaki na waombaji wenye vigezo kulingana na nafasi za kazi zilizotangazwa?
  JIBU
  Vigezo ama njia zinazotumika na Sekretarieti ya Ajira katika kuchuja waombaji wa nafasi za kazi kulingana na kada husika viko vingi ila naweza kuviweka katika makundi manne (4) ya msingi kama ifuatavyo;-
  a) Ni kupitia maombi ya waombaji wote wa fursa za ajira kama yalivyopokelewa na kuchambuliwa kulingana na kada na baadae kuandika orodha ndefu (longlisting) ya kila kada na kuanza kuangalia sifa za mhusika kulingana na kada aliyoomba kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za taaluma kuthibitisha uhalali wa nakala ya vyeti vilivyowasilishwa na waombaji kama vile;-
  · Tume ya Vyuo Vikuu (Tanzania Commission for Universities – (TCU) ili kuthibitisha uhalali wa Cheti na Chuo husika alichosoma mwombaji hasa kwa waombaji waliosoma nje ya nchi.
  · Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ili kuhakiki uhalali wa cheti husika.
  · Kuwasiliana na mamlaka nyingine kwa ajili ya uchunguzi ikiwemo wadhamini (referee) waliowasilishwa na mwombaji katika wasifu (CV) wake ili kuona kama anakidhi vigezo hitajika kama alivyoonesha.
  b) Baada ya kukidhi vigezo vya msingi vinavyotakiwa mwombaji ataingia katika orodha fupi (shortlisting) na kuitwa kwa ajili ya usaili wa mtihani wa kuandika kulingana na nafasi aliyoomba.
  c) Baada ya hapo mwombaji atafanya pia mtihani wa vitendo (practical) mfano ameomba kazi ya udereva atapelekwa VETA au TEMESA atafanya majaribio ya kuendesha gari au mwombaji wa nafasi ya IT atapewa Kompyuta na kuambiwa mambo ya kufanya au Mpigapicha atapewa Kamera na kuelekezwa cha kufanya nk.
  d) Baada ya hatua hiyo ndipo mhusika atamalizia kwa kufanya mtihani wa mahojiano ya ana kwa ana, hii ikiwa ni hatua ya mwisho ya kumpata mwombaji mwenye sifa zinazotakiwa katika nafasi/kada husika.
  e) Mwisho mwombaji akitimiza vigezo na kupitia michujo yote hiyo na kufaulu usaili husika basi atapangiwa kituo cha kazi kulingana na fursa za ajira zilizopo na endapo nafasi ni chache basi anaweza kubakia kwenye kanzidata mpaka pale nafasi itakapopatikana na kupangiwa.

  SWALI
  5. Ninajua mmekuwa mkiendesha mchakato wa ajira ikiwemo kufanya usaili wa nafasi mbalimbali kama za;-
  a) Watendaji Wakuu wa Mashirika/Taasisi za umma;
  b) Watumishi wa kada za kawaida/kada ya kuingilia kazini
  c) Academic Staff/Professional Staff;
  Swali langu linakuja je, hawa wote mmekuwa mkiwafanyia usaili wa aina moja? Kama sio je, ofisi yenu ina Wataalam wa kutosha kufanya saili za aina zote?
  JIBU
  Kulingana na swali lako nitalijibu kwa A) na B) sehemu A) nitaelezea kuhusu aina za usaili kulingana na kada na B) nitaeleza kuhusiana na namna Sekretarieti ya Ajira inavyoweza kufanya aina zote za usaili kulingana na wataalam iliyo nao.
  A) Kuhusu suala la usaili nalo nitalielezea kulingana na kada kama ulivyoaziainisha;-
  i. Watendaji Wakuu wa Mashirika/Taasisi za umma; Watendaji hawa wanapoitwa kwenye usaili hupewa mada ambao wanatakiwa kuiandaa kwa muda wa saa moja kwa kutumia kompyuta na kisha baadae huingia kwenye jopo la usaili lenye wataalam wa kada husika na kuiwasilisha kwa kawaida muda huwa haupungui nusu saa na kuendelea na kisha jopo la wataalam huanza kumuuliza mhusika maswali kutokana na mada aliyowasilisha. Kimsingi msailiwa atatakiwa kupata alama kuanzia sitini (60) na kuendelea endapo atapata alama chini ya hapo basi mwombaji atakuwa ameshindwa usaili. Kwahiyo unaweza kuona kuwa msailiwa amepitia hatua tatu za usaili yaani mtihani wa Kuandika (Written examination), Kuwasilisha (Presantation) na Mwisho usaili wa ana kwa ana (Oral interview).
  ii. Watumishi wa kada za kawaida/kada ya kuingilia kazini;-
  Watumishi wa kada hii mara nyingi huwa na waombaji wengi sana kwa nafasi moja au mbili. Hivyo waombaji hawa wanapoitwa kwenye usaili kulingana na wingi wao na Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma toleo la 2 la mwaka 2008 kazi mojawapo ya Sekretarieti ya Ajira ni kufanya usaili na kuweka kumbukumbu za waombaji nafasi za kazi waliofaulu katika kanzidata. Kwahiyo Sekretarieti hufanya usaili wa kuandika pale tu inapotokea waombaji kazi ni wengi na wana sifa zinazolingana na kwa wale watakaofaulu kwa alama kuanzia hamsini (50) na kuendelea huitwa katika usaili wa pili ambao ni wa ana kwa ana (oral interview). Ambapo msailiwa yeyote atakayepata alama zaidi ya hamsini (50) na kuendelea hupangiwa vituo vya kazi kulingana na mahitaji ya waajiri na mshindi aliyeongoza kwa ufaulu na watakaobakia huingizwa kwenye kanzidata (Database) ya ofisi.
  iii. Academic Staff/Professional Staff;
  Usaili wa Wahadhiri una tofauti kwa kiasi fulani na zile mbili nilizozielezea awali. Kwanza, msailiwa anatakiwa kupata alama kuanzia sabini (70) na kuendelea. Aidha, utaratibu wa usaili kwa kada hii msailiwa hupewa fursa ya kuchagua mada moja katika eneo lake la kitaaluma/kufundishia na kutakiwa kuiandaa kwa muda wa dakika arobaini na tano (45) mara baada ya kuianda anatakiwa kuiwasilisha kwenye jopo la usaili lenye wataalam ambao hupima vitu vingi kutoka kwa mhusika ikiwemo mbinu za ufundishaji, uwezo/uelewa wa mhusika katika fani husika, kiwango cha elimu , haiba na wakati mwingine hufuatiwa na usaili wa ana kwa ana.

  B), Baada ya kufafanua taratibu na hatua za usaili kwa kila kada kama ulivyoainisha sasa nitaongelea namna Sekretarieti ya Ajira inavyoweza kuendesha saili zote hizo ulizozitaja. Aidha, Sekretarieti baada ya kufanya uchambuzi wa vibali vya ajira vilivyowasilishwa na Waajiri kulingana na mahitaji waliyonayo na kutoa matangazo, ambapo waombaji mbalimbali kuleta maombi yao. Baada ya hatua hiyo kukamilika, Sekretarieti ya Ajira ina utaratibu wa kushirikisha Wataalam mbalimbali kutoka katika sekta ama Taasisi husika inayohitaji watumishi kutoa Wataalam watakaoshirikiana na Watumishi waliopo katika Sekretarieti ya Ajira kufanya yafuatayo;-
  a) Uandaaji wa orodha ndefu na fupi pale inapobidi,
  b) Kuandaa maswali yatakayotumika kwenye usaili kulingana na kada inayotakiwa,
  c) Kuunda majopo ya usaili kwa ajili ya kuwafanyia usaili waombaji wa fursa za ajira.
  d) Kusahihisha mitihani husika au kuwafanyia mafunzo ya vitendo kulingana na aina ya kazi inayoombwa.

  SWALI
  6. Je, mna sababu zozote za msingi za kuamua kutumia njia ya posta tu katika kupokea maombi ya kazi na si njia zinginezo?

  JIBU
  Sekretarieti ya Ajira imeamua kwa hivi sasa kupokea maombi yote ya fursa za ajira kwa njia ya posta tu kwa sababu zifuatazo;-
  a) Kuweka usawa kwa waombaji wote wa fursa za ajira katika utumishi wa umma.
  b) Kuepuka mawasiliano ya moja kwa moja yaani ana kwa ana kati ya wateja wa Sekretarieti na Watendaji.
  c) Kuwapunguzia gharama na muda waombaji wa fursa za ajira kusafiri umbali kuleta barua za maombi ya kazi.

  SWALI
  7. Je, Sekretarieti ya Ajira ina ofisi kila mkoa kama Sheria inavyoelekeza? Maana mara nyingi nimekuwa nikisikia mkitoa matangazo ya kuita watu kwenye usaili katika Dar es Salaam.
  JIBU
  Ni kweli Sekretarieti ya Ajira inatakiwa kuwa na ofisi kwa kila mkoa kama Sheria inavyoelekeza, lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti, upya wa ofisi, uhaba wa watumishi na mabadiliko ya majukumu kwa baadhi ya kada bado hatujaweza kuwa na ofisi kwa kila mkoa ila tumeshaweza kupata ofisi katika mikoa ifuatayo ikiwemo mkoa wa Manyara, Mwanza, Tabora, Dodoma na Dar es Salaam.
  SWALI
  8. Nimekuwa mfuatiliaji wa Vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo mitandao ya kijamii na kuna wakati niliona baadhi ya wadau wenu wakilalamikia suala la kutumia transcript katika kutuma maombi ya kazi. Je, Sekretarieti ya Ajira mnalizungumziaje suala hilo?

  JIBU
  Kuhusu suala la matumizi ya “Transcript” katika kuwasilisha maombi ya kazi inakubalika ila kutegemeana na muda wa mhusika aliomaliza masomo/elimu yake. Kwa mfano mhusika amemaliza chuo miaka miwili iliyopita na chuo alichomaliza elimu/mafunzo yake bado hakijatoa vyeti kwa wahitimu wake, basi mwombaji anaweza kutumia transcript kuwasilisha maombi yake ya kazi. Ila endapo mwombaji atatumia transcript kuwasilisha maombi na chuo husika alichomaliza kilishatoa vyeti vya kuhitimu atatakiwa kuambatanisha na nakala ya cheti cha kuhitimu na siku ya usaili anapaswa kuja na nakala halisi zote za taaluma aliyonayo na si kuendelea kutumia transcript pekeyake. Aidha, ni muhimu waombaji wakafahamu kuwa endapo cheti cha kuhitimu hakijatoka chuoni na mhusika ameona tangazo na kutuma maombi kwa kuwasilisha transcripts zilizoandikwa “statement of results”, au “provisional results” hazitakubaliwa.

  SWALI
  9. Je, mnachukua hatua gani pale ambapo mnakumbana na waombaji kazi wenye sifa za ziada katika nafasi moja ya tangazo kwa fani hiyo hiyo?
  JIBU
  Sekretarieti ya Ajira pale inapokumbana na waombaji wenye sifa za ziada katika kada/fani moja inachokifanya ni kuwaingiza wahusika wote katika orodha fupi (shortlisting) na kuwaacha wote wapitie mchujo wa kazi husika na endapo wanaohitajika ni wawili (2) na wenye sifa za ziada wako wako watano (5) na wote wamekidhi vigezo na kufaulu usaili basi watapangiwa vituo vya kazi kulingana na ufaulu wao yaani anaeongoza na watakaobakia watawekwa kwenye kanzidata ya ofisi wakisubiri fursa nyingine ya ajira itakapojitokeza ili waweze kupangiwa endapo vigezo vitakavyokuwa vikihitajika vinanalingana na walivyonavyo.

  SWALI
  10. Je, mnachukua hatua gani pale ambapo mnakumbana na waombaji kazi wenye sifa za ziada katika nafasi moja ya tangazo kwa fani tofauti? Kwa Mfano, mnahitaji mtu wa (Astashahada-Certificate) au (Stashahada-Diploma) au (Stashahada ya juu-au Advanced Diploma) na akaomba mtu mwenye (Shahada-Degree) au (Shahada ya Uzamili-Masters)

  JIBU
  Kinachoangaliwa na kuzingatiwa ni sifa ya msingi ya kuingilia katika nafasi husika kama zilivyoainishwa kwenye miundo ya kiutumishi (scheme of service). Aidha, sifa ya ziada inachukuliwa kama “added advantage” kwa mhusika. Endapo waombaji wa kada/nafasi husika wapo wa kutosheleza hizo sifa za ziada hazitazingatiwa. Ila angalizo kwa baadhi ya waombaji unaweza kukuta kada inayotakiwa ni mwanasheria, lakini mwombaji amesoma shahada ya uchumi alafu akachukua shahada ya uzamili katika fani ya sheria hapo ajue wazi hawezi kuchaguliwa katika kazi aliyoiomba. Ijapokuwa kuna kazi zinazoweza kuingiliana mfano endapo kazi inayotakiwa inahitaji Afisa Tawala na mwombaji amesoma sheria na kufanya mwaka mmoja wa mafunzo ya sheria (school of law) akamaliza, mwombaji huyo endapo ataomba kazi hiyo na kukuta walioomba wako wanne (4) na kuna fursa za kazi saba (7) mtu huyo anaweza kuchukuliwa kwa nafasi hiyo. Ingawaje tunahimiza watu kuomba kazi kuendana na fani uliyosomea na fursa ya ajira iliyotangazwa kwa kuzingatia vigezo vya tangazo husika ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata kazi hiyo.

  SWALI
  11. Je, mnachukua hatua gani pale ambapo mwombaji kazi alishapangiwa kazi na Sekretarieti ya Ajira na anaomba tena kwa nafasi ileile lakini Taasisi tofauti?
  JIBU
  Sekretarieti ya Ajira inachofanya kwa waombaji ambao walishawahi kufanya usaili wakafaulu na kupangiwa vituo vya kazi halafu hawakwenda au walikwenda kuripoti na kuamua kuacha kazi katika maeneo husika ni kutokuwapangia tena hata kama wataomba endapo kazi wanayoiyomba ni kwa nafasi ama kada ileile ili kutoa fursa kwa wale wenye kuhitaji kazi na sio kuendelea kupoteza rasilimali za serikali kuwafanyia baadhi ya watu mchakato wa ajira ambao bado hawajajua wanataka nini.
  Hatua nyingine tunayoaichukua kwa watu kama hao ni kuwaelimisha madhara ya kupangiwa kazi sehemu fulani na kukataa kwenda kwa kutaka kuchagua maeneo au ofisi fulanifulani tu za kufanya kazi. Baadhi wameweza kutuelewa na sasa hawachagui maeneo ya kwenda kufanya kazi kwani wanaelewa changamoto ya ajira iliyopo nchini na wasomi ni wengi lakini hawana ajira sasa ni vyema kwa wale wanoipata kuitumia fursa hiyo vyema kuliko kuendelea kujidanganya na kujikuta amepoteza fursa nzuri ya kujikwamua kiuchumi na kimaisha na kubakia mtaani akilalamika na akitangatanga na kuwa tegemezi kwa ndugu na jamii kwa ujumla.

  SWALI
  12. Mimi ni mmoja wa wadau ninaefuatilia kwa karibu masuala ya ajira nchini hususani katika sekta ya umma ambae ningependa kujua changamoto za jumla zinazoikabili Sekretarieti ya Ajira katika utendaji wake.
  JIBU
  Kimsingi changamoto zipo nyingi, kwa leo nitazitaja baadhi tu ambazo ni;-
  i. Mapungufu ya Miundo ya Utumishi
  Baadhi ya miundo ya utumishi wa umma kutokukidhi mahitaji ya sasa ina mapungufu ikiwemo migongano ya miundo ya utumishi hasa upande wa sifa/vigezo. Ambapo unaweza kukuta sifa za kada moja zinatofautiana toka Taasisi moja ya Umma na nyingine hususan Miundo ya Wakala wa Serikali na Taasisi zingine za Umma. Jambo ambalo linachangia kuleta malalamiko kwa Waombaji kwani kazi moja (kada moja) inatangazwa kwa sifa tofauti tofauti. Miundo ya Taasisi hizi wakati mwingine inatofautiana na Miundo Mikuu ya Utumishi ya kada husika. Mapungufu haya yameshawasilishwa kwenye mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

  ii. Ufinyu wa Bajeti
  Mchakato wa ajira unahpita au unahitaji hatua mbalimbli mfano matangazo kwa njia mbalimbali, mawasiliano na mambo mengine ambayo yote kwa pamoja ili kuyafanikisha yanahitaji fedha. Hivyo ufinyu wa bajeti isiyokidhi mahitaji ya Sekretarieti ya Ajira unachangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa wakati na nyakati nyingine kujikuta ikiwa na madeni makubwa. Aidha, imechangia pia kushindwa kuzifungua ofisi zake za mikoani ambazo zingerahisisha kusogeza huduma ya ajira karibu na wananchi hivyo kukuta majukumu yake takribani yote yakiendelea kufanyika makao makuu ya ofisi zake na mara chache mikoani au kupitia kwenye kanda zilizoainishwa.

  iii. Udanganyifu/ kughushi vyeti kwa baadhi ya waombaji
  Sekretarieti ya Ajira imejikuta ikikumbana na changamoto ya udanganyifu wa sifa kwa baadhi ya waombaji, hususan kughushi vyeti vya kidato cha nne na sita vinavyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa na Vyuo vya mafunzo. Vilevile, baadhi yao hutoa taarifa za uongo kuhusu uzoefu walionao katika fani husika kwa lengo la kujipatia fursa za ajira serikalini.

  iv. Kutofahamika vya kutosha na wadau
  Sekretarieti ya Ajira kutofahamika vya kutosha na wadau wake kutokana na upya wake. Aidha, hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na ofisi hii ili iweze kutambulika zaidi kwa wadau wake.

  MWISHO.
  “Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawahimiza waombaji wote wa fursa za ajira Serikalini kuzingatia masharti ya tangazo wanapotuma maombi yao ya kazi na kujiandaa vyema pindi wanapopata fursa ya kuitwa kwenye usaili ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata kazi wanayoomba”.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Kwa maelezo zaidi tembelea PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT - PSRS au tuma maoni:[​IMG]1. Mimi ni Mtanzania, nimekuwa nikiisikia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Je, naweza kufahamishwa majukumu ya Sekretarieti ya Ajira kwa ujumla ni yapi?[/h][h=3]JIBU

  Kwa maelezo zaidi tembelea PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT - PSRS au tuma maoni:[/h]
   
Loading...