Maombi ni upotevu wa muda

Maombi ni upotevu wa muda

Maombi yako hayajibiwi labda una imani dhaifu au huongezi juhudi kupata unachoomba au muda wake wa kujibiwa bado
 
MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....
 
Ukitaka kujua kitu kina ukweli angalia historia yake. Maombi yamekuwepo tangu na tangu. Kabla hata ya kuletewa dini za mashariki ya kati.

Maombi yanafanya kazi. Maana kwenye ulimwengu huu kuna vinavyoonekana na visivyoonekana. Ukikaza shingo itavunjika.

Bila nguvu ya maombi wengi tungeshakata tamaa. Naamini asilimia 100 kwenye maombi.
 
Mimi BushDokta kwa sasa nikisikia tu hata sauti inayoambatana na mambo ya makanisa au misikiti nachukia Sana.

Nikimwona mtu anaomba moja Kwa moja namuona kama aliyerukwa na akili na hajielewi.

Maombi hayana effect yoyote na hayana kazi kwenye maisha ya Binadamu. Ni upo
Maombi si mabaya kiivo, kwani yanampa tumaini muombaji kuwa atafanikisha analolifanya (lazima uwe unafanya kitu na si kuomba na kukaa)
Maombi yasaidie muombaji kutokata tamaa hivyo aendelee na analofanya mpaka aone matokeo.
Ni saikolojia.....
 
Maombi si mabaya kiivo, kwani yanampa tumaini muombaji kuwa atafanikisha analolifanya (lazima uwe unafanya kitu na si kuomba na kukaa)
Maombi yasaidie muombaji kutokata tamaa hivyo aendelee na analofanya mpaka aone matokeo.
Ni saikolojia.....
Ni saikolojia Tu kumbe hakuna nguvu yoyote ya kiroho wala ya Kimungu
 
Kila mtu na imani yake, ukiona unapoteza muda sawa, lakini kwangu ni heri nipoteze muda kwa Mungu kuliko kupoteza muda kwenye vijiwe, kwenye mipira, kwenye Kubet huko sio muda tu unaopotea na nafsi ya mtu inapotea.

Aliyekuambia ukiomba usifanye kazi ni nani? Hivi unakuwa kipofu kuna wanaofanya kazi kwa bidii kabisaa na wewe bidii yao unaiona lakini hawajafanikiwa? Kwani wewe ni mgeni huko kwenye migodi ya madini watu wanatoa kafara na kuna ushuhuda hapa kwamba ukienda kizembe wewe ndio unakuwa kafara yenyewe, hapo ndipo imani inachukua nafasi yake ni either uamini kwa waganga au umuamini Mungu akusaidie.

Ukiona kuomba ni kupoteza muda ni sawa, lakini kwa anayeomba muache maana anajua anayemuomba
 
Maombi sio kitu naunga mkono
Kwanza tunayemuomba hatuna uhakika kama yupo

Unaomba afya unaumwa
YESU, ALLAH, YEHOVA, ELISHADAI, ELOHIM, BWANA WA MAJESHI, MUNGU, GOD, haya yote ni majina ya kutungwa ya kukipa uwezo kiumbe ambacho hakipo kwa madhumuni ya kuwadanganya watu.

Wanaokesha makanisani/misikitini wanapoteza muda wao bure maana maombi yao yanakwenda bure yaani wanaomba kitu ambacho hakipo, hakisikii, hakina uwezo wa kujibu.

Maombi yangekuwa na nguvu, majibu tungeyaona kwa hizi jamii za kiafrika zilizojishikamanisha na dini.

dunia ina MUUMBA lakini si Mungu, MUUMBA ni zaidi ya Mungu, Muumba haitajiz hizi dini na TAKATAKA zingine ili tumjue.

Tunamuomba asiyestahili ndiomaana hatupati majibu.
 
Maombi sio kitu naunga mkono
Kwanza tunayemuomba hatuna uhakika kama yupo

Unaomba afya unaumwa
Duh
Shida yetu asee tunaangalia neema tulizo nyimwa hatuangalii mengi tuliyopewa

Sometimes unaomba kitu hupewi coz kina athari hasi kwako kwa sababu anatujali hatupati kila tunachoomba
 
Back
Top Bottom