Maombi ni upotevu wa muda

Maombi ni upotevu wa muda

Maombi sio kitu naunga mkono
Kwanza tunayemuomba hatuna uhakika kama yupo

Unaomba afya unaumwa
Pia bila ya kuwa na changamoto au shida tunazo pitia
Tusinge thamini neema tunazopewa just imagine kusingekuwa na magonjwa uzima ungekuwa hauna thamani
 
Kama maombi kweli kweli yatatatua matatizo, basi umaskini ungeisha, magonjwa yangeponywa, rushwa ingeisha, na majanga yangezuiliwa kwa kuomba tu kwa bidii.

Lakini uhalisia haupo hivyo.

Watu wanaomba kazi badala ya kujitengenezea fursa. Wanaomba uponyaji badala ya kutafuta matibabu. Wanaomba mabadiliko wakati hawafanyi chochote kuyaleta.

Maombi yanaweza kutoa faraja ya kiroho, lakini faraja si uthibitisho wa ufanisi.

Hatuhitaji kuomba suluhisho. Tunahitaji kufikiri kwa kina, sayansi, ushahidi, vitendo, na uwajibikaji.

Acha kusubiri msaada wa kimungu. Tatua matatizo ya kibinadamu kwa vitendo vya kibinadamu.

Taikuni la kuwastua wanaotapeliwa kiimani hasa wakristo Kubwa la Maadui
Una hoja , usikilizwe.
 
Mara tatu kwa wiki Kuhani Musa anauza mafuta ya kuondoa matatizo yote Sugu na watu wanaenda kununua kila wiji na matatizo hayaishi.
 
Kama ambavyo Galileo alitaka kuuwawa kwa kusema dunia ni duara, ndivyo ambavyo aliesema kitimoto haramu alivyowaingiza watu chaka.
Baada ya miaka mingi werevu wa galileo uliweza kuthibitishwa kisayansi maana watu zamani waliamini dunia ni tambarare, kitendo cha yeye kusema si tambarare ni duara ilionekana kama kosa, hasa kwa kuwa waliosema tambarare walikuwa na mamlaka.
Hii issue ndio inakula watu kwenye dini mpaka leo kuhusu kitimoto. Kabla sayansi haijasema kitimoto na wanyama wengine wameumbwa vipi, Mjinga wa zamani aliwahadaa watu wasile kitimoto kwa kuwa hacheui. Kama unavyojua uongo hauna ushahidi hivyo hata wanasayansi walipobaini kuwa tofauti na mbuzi na ng'ombe na wanyama wengine walao majani, wenye matumbo kadhaa, kitimoto ana tumbo moja kama binaadamu. Hivyo anapokula chakula hawezi kucheua sawa na ambavyo binaadamu hawezi kucheua. Mbuzi na wengeo hucheua kama kitendo cha kurudisha akiba ya chakula mdomoni na kuitafuna kisha kuimeza sasa hadi tumbo kuu. So kitimoto hacheui kwa sabaabu za kiuumbaji na wala sio laana.
 
●Maombi ya aina yeyote yale kuna kukubaliwa na kukataliwa.

●Wengine maombi ni sehemu ya ibada zaidi kuliko kutaraji majibu, hivyo wanaomba kwa sababu ni ibada kuomba.

●Wengine wakitaka kufanya lolote lile huomba kwanza.

●Lakini maombi pia wakati mwengine ni suala lenye kuhitaji ujuzi au uwezo wa ziada.

●Pia maombi si kwa ajiri ya watu dini au watu wenye imani fulani pekee, unaweza usiwe na muumini na bado ukafanya maombi.
 
Back
Top Bottom