Maofisa watano wa TMDA waliokuwa na tuhuma ya kuhujumu uchumi waachiwa huru

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi ya Uhujumu Uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA) akiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Raymond Wigenge, waliokuwa wanakabiliwa na shtaka moja la kuisababishia hasara Mamlaka hiyo ya Sh58 milioni.

Hiyo ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi ya washtakiwa hao.

Uamuzi wa kuifuta kesi hiyo umetolewa leo Jumanne Mei 17, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo, wakati shauri hilo lilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka

CHANZO: Mwananchi
 
Hii kesi ninaifahamu vizuri. Hakuna uwizi wowote uliofanyika hapo ila iliwekwa kwenye kundi la uhujumu uchumi tu kumfurahisha Magufuli.
.
Hao watuhumiwa walikuwa ni viongozi wakuu wa Idara mbalimbali za TFDA. Wao waliidhinisha safari za kikazi kwa ma junior wao. Inaonekana hao majunior wao walipata kazi zingine za kufanya kutoka vitengo vingine Serikalini. Kwa hiyo wakaamua kufanya kazi zingine badala ya zile walizotumwa na mabosi wao. Halafu wangeenda kwenye kazi hizo baada ya zile zingine.

Basically hii ilikuwa ni administrative issue ambayo hata Board of Trustees haifiki.

Magufuli ameipitisha Nchi kwenye ujinga mwingi
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi ya Uhujumu Uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA) akiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula...
Hivi ni lini serekali itakujaga kushida kesi watu wanaiba weee wanaachiwa
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi ya Uhujumu Uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania (TMDA) akiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula...
Ni mwendo wa mchongo tu sasa hv,
 
Hii kesi ninaifahamu vizuri. Hakuna uwizi wowote uliofanyika hapo ila iliwekwa kwenye kundi la uhujumu uchumi tu kumfurahisha Magufuli.
.
Hao watuhumiwa walikuwa ni viongozi wakuu wa Idara mbalimbali za TFDA. Wao waliidhinisha safari za kikazi kwa ma junior wao. Inaonekana hao majunior wao walipata kazi zingine za kufanya kutoka vitengo vingine Serikalini. Kwa hiyo wakaamua kufanya kazi zingine badala ya zile walizotumwa na mabosi wao. Halafu wangeenda kwenye kazi hizo baada ya zile zingine.

Basically hii ilikuwa ni administrative issue ambayo hata Board of Trustees haifiki.

Magufuli ameiputisha Nchi kwenye ujinga mwingi
Unaifahamu wapi kulikua na double payments , mtu anapata malipo mara mbili kwa kazi moja alofanya ndio msingi wa hio kesi
 
Utakuta walibambikiwa ili kiwakomesha Utawala wa Jiwe ulikuwa wa laana.
 
Unaifahamu wapi kulikua na double payments , mtu anapata malipo mara mbili kwa kazi moja alofanya ndio msingi wa hio kesi
Uhujumu uchumi wa sh 58m! Upumbavu mkubwa. Kweli nchi iiongozwa na washamba, watu wenye chuki.

Makosa mengine yalikuwa ya kodi, mengine ya kimaadili, na mengine ya kukosa uaminifu, lakini yote yakafanywa ni uhujumu uchumi.

Niliwahi kwenda huko Iringa, nikasikia wachoma mkaa waliokuwa na magunia 10 ya mkaa wamekamatwa na kiongozi akaagiza wafunguliwe shtaka la uhujumu chumi kwa sababu wameikosesha halmashauri mapato. Ushuru wenyewe kwa kila gunia ilikuwa shilingi 3,000. Kwa magunia 10, ina maana wamehujumu uchumi kwa kukwepa kulipa sh 30,000.
 
Hapo Kuna mtu wa Chato alikuwa anatafutiwa ajira, Chato dynasty wakasuka zengwe kuwatoa
 
Unaifahamu wapi kulikua na double payments , mtu anapata malipo mara mbili kwa kazi moja alofanya ndio msingi wa hio kesi
Sikatai hilo bali nasema ilikuwa ni issue ya internal disciplinary mechanism na siyo issue ya Kimahakama. Tunapoteza muda mwingi kutumia muda wa Mahakama ambao ungeelekezwa kwenye makesi sugu yaliyokaa mahakamani
 
Back
Top Bottom