Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Watu wanaunda vikundi ili waweze kusaidia wakati wa matatizo yeye bado analeta ukabila!! Mtu akifiwa yeye kama kiongozi wa serikali ameshawachangia nini ili angalau kama ni kusafirisha maiti au watu tu wa kukodi gari ili wafike msibani!

Watu wanaanzisha makundi mazuri ili tu waweze kujiendeleza! Namshngaa sana huyu jamaa kwa sababu hata serikali sasa hivi inavikundi mbalimbali
 
Yaani Moshi wandhani kila wakati wanaonewa sana! Mbona alipiga marufuku vikundi vya Mara na hatukusikia kelele kama ninyi? Au ndo munatafuta ushujaa kuliko wengine!
 
RC yupo sahihi ni kuleta ukabila tu na ubaguzi , futa kabisa huo upuuzi
Kwa mpumbavu kama wewe tena watu wasiojitambua lazima utasema hivyo kwani hujui maana ya vyama hivi. Kwa faida ya wajinga kama wewe vyama hivi vina manafaa makubwa kwa wahusika kma ifuatavyo;
  1. Kusaidiana ktk mambo ya shida na raha ie misiba au sherehe
  2. Kusaidiana ktk biashara kwa kukopeshana nk
  3. Kuratibu mambo ya maendeleo ktk maeneo yao
  4. Ieleweke pia kuwa vikundi hivi vingi husajaliwa km utaratibu unavyotaka
 
Yaani Moshi wandhani kila wakati wanaonewa sana! Mbona alipiga marufuku vikundi vya Mara na hatukusikia kelele kama ninyi? Au ndo munatafuta ushujaa kuliko wengine!
Ni ile majigambo kwamba wameendelea sana! Kumbe Mwamposa akipita, anawakusanya!
 
Mnapoelekea mtawakataza ata watu kuongea lugha ya mama.Hivi mtajisikiaje ndugu zenu wakikatazwa kukutana huku kama Diaspora.
 
RC wa Manyara, Alexander Mnyeti amefuta kikundi cha watu wa Kilimanjaro waishio Manyara. Wiki chache zilizopita alikifuta kikundi cha watu wa mkoa wa Mara waishio Manyara. Amesema ataendelea kuvifuta vikundi/vyama vyote vya watu kutoka mikoa mingine waishio Manyara kwa sababu havina faida kwa mkoa huo na vinaendekeza ukabila. Ameshauri viundwe vikundi vya jamii za watu wa Manyara kama Wairaq, Wafyomi, Wamassai etc.


Swali : Kwa kadri ya kumbukumbu ya mwanaJF unayesoma uzi huu , vikundi kama hivi vya kuzikana viliwahi kuleta madhara yoyote mahali popote ?

MAONI YA WADAU








View attachment 1283640
Kama athali zimeanza leo lazima wapigwe!
 
Hata mimi sivipendi vikundi hivyo,vifutwe tu,kama kukitokea tatizo wote tusaidiana kama jamii.Ila anaji-contradict kwa kuruhusu uanzishwaji wa vikudi vya makabila ya mkoa wa Manyara,mbona navyo ni vya kikabila?Asiruhusu vyote.Mimi huwa sipendi pia vikundi vya kufa na kuzikana,napenda tatizo likitokea tusaidiene wote kama jamii.
Ukipata tatizo ndio utajua umuhimu wa hivi vikundi , Ndio watu wasaidiane kama jamii, jiulize nan atakusaidia tu halafu likitokea kwake wewe hauonekani? Kwa dunia ya kileo hakuna mtu anaetoa kitu bila kufikiri mara mbili mbili.
 
Ukipata tatizo ndio utajua umuhimu wa hivi vikundi , Ndio watu wasaidiane kama jamii, jiulize nan atakusaidia tu halafu likitokea kwake wewe hauonekani? Kwa dunia ya kileo hakuna mtu anaetoa kitu bila kufikiri mara mbili mbili.
Unajua mkuu,unachokiri ndicho kinachotokea.Faith makes the unreal real.Hii ina maana kwamba unakula matunda ya maneno,mdomo,ukiri wako au imani yako,so you are a product of what you believe in.Sasa ukishajiunga na vikundi hivyo,you are infact admitting that problems will happen,and so you are creating problems.

Vikundi hivi ni vibaya zaidi kwa kuwa they make you shift your faith from God to the group! Unajua unachowaza:nikipata tatizo kikundi changu kitanisaidia,not knowing that in so doing,the group then becomes your idol or God.How stupid.

Lakini kumbuka kwamba Mungu amesema Yeye ni Mungu mwenye wivu, so our faith must be centred in God only.Sasa kama umemuacha Mungu,kwa nini usipate mapigo kutoka kwa Shetani?

Labda nimalizie kwa kusema vikundi hivi is a new phenomenon, zamani havikuwepo kabisa and we were comfortable, tatizo likitokea wote kama jamii tunasaidiana kulitatua.

Nini kimetokea?The bitter truth is,people have fallen away from God.Watu wanatumia akili zao katika kila jambo,hawamtegemei Mungu,kwa hiyo Mungu naye amewaacha.It is an extremely sad situation.
 
Kimsingi huyu jamaa Ni mkorofi.Hivi vyama vimetapakaa nchi nzima na lengo nikusaidiana katika shida mbali mbali .Uanachama upo wazi kwa yoyote anayetaka kujiunga.Ndio maana wachaga wengi wakifariki maiti zinasafirishwa.Harusi za wachaga kawaida zinakuwa well organized kutokana na vikundi Kama hivi
 
Mimi naona kuna namna nyingi za kutafuta umoja wa kijamii ukiachilia mbali ukabila na ukanda, hivyo yupo sahihih havina msingi mzuri kwa afya ya umoja wa kitaia. Umo ndani kuna majigambo na ubaguzi dhidi ya wTu wasio wa kundi hilo.
 
Back
Top Bottom