Ndio maana nakuambia mwanamke usipokua na akili hautaweza ndoa, kwakuwa mwanaume anaweza kukuambia au kufanya kitu kinaweza kisikupendeze ndio lakini unatakiwa u react in a way ambayo yeye mwenyewe akikaa akitafakari anakuja kuomba msamaha bila kutaka, sio unaanza kubishana nae na kupayukiana mpaka ajirani wanatoka milangoni kuchungulia, au usiku unamsusia haki ya ndoa. Kaa nae kiakili, nasikiaga watu wanasema ukishamjua mtu wala asikupe shida we nenda nae sawa tu mwisho wa siku atajirudi, vitu vingine ni majaribu na mitihani, uki panic yataendelea kuwa makubwa, bora utulie tu usikurupuke katika maamuzi