Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,792
Habari za J2 wapendwa,
Huyu shost mtakuwa mnamfahamu ni yule tulipata pamoja Ki-paimara katika lile kanisa. Shost huyu kwao wamezaliwa mabinti 6 hawana kaka na mabinti wote sita wametoka mashallah. Shost alipomaliza IV matokeo yalikuwa ya kawaida, alifanikiwa kusoma secretarial course na kupata kazi pia alibahatika kupata ndoa ya kanisani, mwenzangu alipata bahati ya kukaa madhabahuni tena na gauni leupe, kwangu mimi vilikoma baada ya ki-paimara.
Basi bwana shost alipata mume ambae alisaidia sana kwao, alisaidia ada za wadogo zake, alisaidia matengenezo ya nyumba wa wakwe na pia kuongeza mtaji kwenye biashara ya baba. Shost anaendelea na ajira yake, watoto watatu na msaidizi wa kazi za ndani ni mdada.
Shost amekuja kugundua kuwa msaidizi wa kazi za ndani ana uja uzito, uliza maswali dada amegoma kabisa kumtaja mhusika, shost anamsubiri mume wake amfahamishe kuwa dada ajira imekoma, mume amekuja juu ajira imekoma kwa sababu gani, kwani anashindwa kufanya kazi, hapana ana mimba, sasa mimba ni ugonjwa?
Baada ya mahojiano marefu, shost anagundua kuwa mimba ni ya mume wake, na pia hayuko tayari kumrudisha kijijini kwao anadai kwa usalama wa afya yake, Dar ndiyo kuna hospitali nzuri akae mpaka ajifungue.
Kwa kweli shost ana hali mbaya sana, ana hasira na anataka kuondoka, wazazi wanamshauri akae tu kwani huyu mwanaume ni kama mkombozi wa familia. Nikiangalia hali hii kwakweli wanaume haya sasa ni manyanyaso kisa unasaidia ukoo wa mke ndiyo umfanyie haya? Matokeo yake mtu anaamua kujiua.