Manumba alazwa ICU Aga Khan

Manumba alazwa ICU Aga Khan

Awaambie Tiss wakamtibu apone! Kilichowafanya wamkimbizie agha khan ni nini? Wangempeleka Muhimbili!!! R.I.P
 
Kwa vyovyote vile yafaa sisi wanadamu tuwatendee wema wanadamu wenzetu ili siku tutakapokuwa tunuaga ulimwengu huu tuuage kwa amani, tukumbuke kilichofungwa duniani na mbiguni kimefungwa.
 
..eeeh Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na upendo...uwasamehe woote waliotoa comment humu JF za kumuombea kifo Manumba. maana Wewe ndiye Mhukumu wa Haki! wote tuseme Amen...
 
hakuna atakayekwepa kifo. kila mtu atakwenda kwa ahadi yake. kama hawa mapolisi ni wakosaji tofauti yao na sisi ni ipi? wao kwa ukaidi wetu tunaona wanatenda mabaya dhidi yetu kwa vitendo. sisi kwa nia zetu mioyo yetu inawawazia mabaya kiasi cha kuwaombea kifo .tofauti yetu na wao nini? kumbe sote tu wabaya ktk dunia hii, tumekosa nafasi tu vinginevyo tungekuwa nafasi zao nadhani ubaya wetu ungekuwa juu saana. maana kumuombea mtu kifo ni nafasi ya shetani.
 
Breaking News: Manumba alazwa ICU Aga Khan
HALI ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwenye wodi ya wgonjwa Mahututi (ICU) jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com hivi punde ni kwamba Manumba amelazwa katika Hospitali hiyo tangu juzi.
Hata hivyo vyanzo vya kuaminika ndani ya Jeshi la Polisi nchini zinadai kwamba hali ya Mkurugenzi huyo wa makosa ya jinai nchini ni mbaya.......

MY TAKE:
Eah Mwenyezi Mungu Msaidie Kiumbe wako huyu apone haraka aje atutumikie watanzania kama alivyotutumikia Jana na juzi na kesho afanye hivyo,
Umzidishie maisha marefu aishi ili aine kesho na kesho kutwa.
Amin!

Rest In Peace Manumba tupate mbadala wa kuwashughulikia mafisadi
 
Breaking News: Manumba alazwa ICU Aga Khan
HALI ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwenye wodi ya wgonjwa Mahututi (ICU) jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com hivi punde ni kwamba Manumba amelazwa katika Hospitali hiyo tangu juzi.
Hata hivyo vyanzo vya kuaminika ndani ya Jeshi la Polisi nchini zinadai kwamba hali ya Mkurugenzi huyo wa makosa ya jinai nchini ni mbaya.......

MY TAKE:
Eah Mwenyezi Mungu Msaidie Kiumbe wako huyu apone haraka aje atutumikie watanzania kama alivyotutumikia Jana na juzi na kesho afanye hivyo,
Umzidishie maisha marefu aishi ili aine kesho na kesho kutwa.
Amin!
Last edited by Kibanga Ampiga Mkoloni; Yesterday at 21:01.​

Nikisikia shida za viongozi huwa ninajiuliza kwanini walitutendea uovu kwani hawakujua sote hapa duniani ni wapangaji tu?

Psalms 37: 13-14

"The wicked plots against the just, and gnashes at him with his teeth.

The LORD laughs at the wicked because He knows his days are numbered........"
 
si wengine huwa wanawapeleka India, huyu ndo kusema serikali haina hela? Aishi ili aone mengi

emergency haina india ndugu. Huwa wanawadharau tu madoctor wetu. Muulize Miraji, alijikuta tu yuko mikononi mwa madoctor waliowatukana na baba yake.
 
Manumba mahututi, alazwa Aga Khan HALI ya Mkurugenzi wa Upeleleziwa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbayana amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan,Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapobaada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.

Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumbaalikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha piafigo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.

"Alitakiwa kupelekwa nje ya nchikwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua,ikashindikana," kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alithibitisha kamishna huyo kulazwaICU Aga Khan lakini akasema kuwa hadi jana jioni, hali yake ilikuwa ikiendeleavizuri.

"Ni kweli amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendeleavizuri," alisema Senso.
Mtu wa karibu na Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vyamalaria, tatizo ambalo lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo figokushindwa kufanya kazi.

"Kutokana na hali aliyonayo tumeshindwa kumsafirisha kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu zaidi kwa sababu baadhi ya viungo havifanyi kazi," alisemamtu huyo.
Hata hivyo, alisema hali ya Manumba inaendelea vyema baada ya kuanza kupatamatibabu.

JK amjulia hali
Viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwamo Rais Jakaya Kikwete jana walifika hospitalini hapo kumjulia halikamishna huyo wa polisi.
Habari zilizopatikana zilieleza kuwa Rais Kikwete alifika hospitalini hapo janamchana baada ya kumsindikiza mgeni wake, Rais wa Benin ambaye pia ni Mwenyekitiwa Umoja wa Afrika (AU), Boni Yayi.
Daktari
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema jana kwambaManumba alifikishwa katika hospitali hiyo tangu juzi akisumbuliwa na malaria naalikuwa hajitambui.

Dk Dharsee alisema kuwa uchunguzi wa awali ulionyesha kwamba alikuwa na malariakali iliyosababisha alazwe ICU. Hata hivyo, alisema baada ya matibabu, haliyake ilianza kubadilika na kuleta matumaini.

"Nimepigiwa simu nyingi leo (jana), nikiulizwa na watu mbalimbali wakitakakufahamu kama Manumba amefariki dunia, ninachotaka kuwaambia ni kwamba ni mzimalakini yuko ICU," alisema.


Hata malaria mtu inabidi aende kutibiwa nje ya nchi kweli??
 
Mungu siku zote ni mwema sana, atamponya KAMANDA ili apate muda wa kutubu kwa yale aliowatendea WATANZANIA... Dhambi haiui bali inatesa ili umrudie MUUMBA wako.... Manumbu Mungu akuponye haraka ili nawe umurudie yeye HARAKA. Amin
 
ARV kwa huyo mzee zimedunda safari hii mana long time anauugua hako kaugonjwa ka kukosa kinga za mwili
 
Back
Top Bottom