Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,077
- 136,505
Inasemekana amekutwa na muhuri wa jeshi isivyo halali. Na pia vitambaa vya sare za jeshi. Mashtaka aliyofunguliwa ni uhujumu uchumi. Nadhani ana mengi ya kusema kama atabahatika kuendelea kuwepo. Je alikuwa na utaratibu wa kufanya hivyo kila mara? Vitambaa hivyo vilikuwa vikipelekwa wapi? Kazi haswa ya huo muhuri ni nini?
Maana sasa kuna shtaka la uhujumu uchumi na usalama wa taifa. Sasa kwenye usalama wa taifa sijui tatizo liko wapi, kwani hizo sare zilitakiwa kupelekwa kwa wanajeshi waasi ama kikundi chochote cha uasi?
Wafanye wafanyacho ila cha muhimu haki itendeke, msumeno wa sheria ukate kotekote. Yani hata kama kuna walioshirikiana naye na wako kwenye vyombo vya madaraka wabanwe. Unless rais aliyepo ana mpango wa kukaa madarakani maisha yake yote. Kwasababu huwezi kumkuta na makosa na kumuhukumu kama ameshirikiana na vigogo halafu ukawafumbia macho vigogo hao na hukumu ikawa ya haki.
Kwa upande mwingine pia, asiwe amebambikiwa. Lakini kama vinahusiana na ugaidi ama jitihada za uasi, basi hilo ni suala jingine kabisa.
Duh!
Kama ni kweli basi atakuwa ni bonge la zumbukuku.
Hajui kuwa sasa kuna sheriff mpya hapa mjini?