Itajulikana tu kama yumo au hayumo, anyway sio lazima yeye awepo anawatumwa wake wanamjulisha.
Huu mchezo wa kukanusha vitu bora kukanusha na kuweka personal attack ndani yake bila ushahidi kutawamaliza wengi.
Again kwa huu utumbo ni wazi kabisa Manji ni fisadi, ina maana anataka kusema ana ugomvi na KAGODA, kwa sababu alirudisha hiyo hela serikalini?
Ni nani huyo Kagoda anayemzungumzia Manji maana kaweka kama mzimu flani tu kwa sababu yeye anawajua awaweke hadharani anaogopa nini?
Manji hawezi kukana tuhuma za Msemakweli kirahisi hivyo; kwanza kama Msemakweli anakutishia kukulipua kisha ukampa hela ina maana alichokutishia ni cha kweli, hii ina kuhusu wewe wala usiseme ni watu.
Mwisho, uhusiano wake na KAGODA uko wazi na ameukiri sasa Msemakweli kakosea wapi? Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Manji alikuwa ni mdhamini wa KAGODA yaani mafisadi, na kwa kutumia mwanya huo alifungua kesi kumshitaki Mengi, sasa hapa hatajibu vipi hizo tuhuma kwamba yeye sio part ya mafisadi.
Ni kwa biashara zipi za mabilioni KAGODA walimwambia wanafanya hapa nchi na yeye kuingia nao mkataba na kupokea hela bila kujua zinatoka wapi?