Manji ajaribu kujisafisha Kashfa ya Kagoda; ajichongea!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Wakuu,

Yusufu Manji katoa taarifa yake kama inavyoonekana chini hapa... Huenda vyombo vya habari nyumbani vikatumia taarifa hii lakini ieleweke kuwa haijasainiwa, tarehe za usajili Kagoda, tarehe za usajili Quality Finance na tarehe za mikopo zimejichanganya mno... You need to be smart when playing such games!

Maneno hayasaidii, go thru the docs:

tamko-manji.jpg

tamko-manji2.jpg


Sasa angalia nyaraka hizi chini:

loan-agreement.jpg

loan-agreement2.jpg


kagoda-registration.jpg


Sasa ndugu yangu Manji, hivi Kagoda na loan kipi kilitangulia? Mkopo kabla ya kampuni au kampuni kabla ya mkopo?

Hapa umejichanganya mkuu wangu, mnaweza kuangalia namna ya kuiweka sawa hii?
 
Surah As shu`araa’ (26), Aayat 181-184, Prophet Shu`aib tells his people:

Give just measure, and cause no loss (to others by fraud). And weigh with scales true and upright. And withhold not things justly due to men, nor do evil in the land, working mischief. And fear Him Who created you and (Who created) the generations before (you).
 
To be honest ya manji na kagoda naona ni old news kwangu.

Mpya ni hili la Manji kuwaweka madiwani wake na meya wake jijini Dar na yanayojiri now....

Halafu si Manji ndie mmilikiwa wa SasaTel?

Kodi wanazolipa SasaTel zikoje? Kodi za Quality Group?

tukiendelea kujadili wizi wa 2005 wakati kuna wizi mwingine unaendelea ni busara kweli?

Si juzi jiji wamempa ufukwe wote wa Oysterbay?
 
It's so easy to catch these mumianis... just sprinkle a bit of sea salt on one of their tentacles and they start writhing about, exposing all other hidden appendages.

Si mnakumbuka ya Kinana na receipt za ndege kwa ajili ya safari za First Lady?!!!
 
Ukienda ikulu kuna makanjanja, ukienda kwenye redio zao kuna makanjanja, hadi kwa huyu che-manji naye pamoja na wasaidizi wake wote makanjanja!
 
Chonde chonde Invisible, ungeangalia namna ya kuwasiliana naye haya ni matatizo ya kiufundi katika kufoji, duu kwanini wasitulie kidogo? yanajirudia makosa yale yale ya kufungua akaunt ya benki siku ya Jumapili. Pole sana Tanzania!!!
mkuu Ezan alijua wa bongo wengi tuna ugonjwa wa kusoma vitu..
 
Ukisoma katikati ya mistari utagundua kwamba ni walewale waliomtuma Msemakweli kuleta humu upuuzi wake na ni hao hao wamejifanya Manji.

Naanza hivi: Hiyo press release ni ya kihuni, ni upuuzi na nahisi imeandikwa bar yaani na mlevi. Kwanza sio official kwa maana ya unsigned, sio headed na imefanya personality attack badala ya kujibu hoja zao za kipuuzi.

Pili hivi huyu Manji, kama na yeye kakubaliana na 'press release' yake, anatufanya mafalz sie? Hata kama brela walimcheleweshea registration japo alikuwa tayari on business sasa ni kwa nini hasemi hayo? Lakini pia kwa nini yeye na serikali wasiungane kuwashitaki Kagoda?

Na nani hasa alikuwa Kagoda ambaye serikali ilimtuhumu kuiba pesa na kumkopesha manji moja kwa moja? Na kwa nini yeye manji alikuwa mdhamini wa wezi kule bank, na mwisho hizo debits huko bank mbona zilikuwa nyingi bila sababu maalum? Wezi watupu?

Najua Nape rafiki yangu anahangaika na haya, baba nikwambie tu ushashindwa hata kabla hujaanza, nawasilisha.
 
To be honest ya manji na kagoda naona ni old news kwangu.

Mpya ni hili la Manji kuwaweka madiwani wake na meya wake jijini Dar na yanayojiri now....

Halafu si Manji ndie mmilikiwa wa SasaTel?

Kodi wanazolipa SasaTel zikoje? Kodi za Quality Group?

tukiendelea kujadili wizi wa 2005 wakati kuna wizi mwingine unaendelea ni busara kweli?

Si juzi jiji wamempa ufukwe wote wa Oysterbay?

Aaaah Bossi, vipi tena mkuu??? Active members zaidi ya 15,000 kati ya members 47,000 tushindwe kuzipelekesha hizi thread sambamba??!!

Unaogopa sauti za "man on, man on" uwanjani, utaweza kweli kubutua mpira walau nje ya goli??!! lol
 
Kwani Manji yupo humu?

Itajulikana tu kama yumo au hayumo, anyway sio lazima yeye awepo anawatumwa wake wanamjulisha.

Huu mchezo wa kukanusha vitu bora kukanusha na kuweka personal attack ndani yake bila ushahidi kutawamaliza wengi.

Again kwa huu utumbo ni wazi kabisa Manji ni fisadi, ina maana anataka kusema ana ugomvi na KAGODA, kwa sababu alirudisha hiyo hela serikalini?

Ni nani huyo Kagoda anayemzungumzia Manji maana kaweka kama mzimu flani tu kwa sababu yeye anawajua awaweke hadharani anaogopa nini?

Manji hawezi kukana tuhuma za Msemakweli kirahisi hivyo; kwanza kama Msemakweli anakutishia kukulipua kisha ukampa hela ina maana alichokutishia ni cha kweli, hii ina kuhusu wewe wala usiseme ni watu.

Mwisho, uhusiano wake na KAGODA uko wazi na ameukiri sasa Msemakweli kakosea wapi? Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Manji alikuwa ni mdhamini wa KAGODA yaani mafisadi, na kwa kutumia mwanya huo alifungua kesi kumshitaki Mengi, sasa hapa hatajibu vipi hizo tuhuma kwamba yeye sio part ya mafisadi.

Ni kwa biashara zipi za mabilioni KAGODA walimwambia wanafanya hapa nchi na yeye kuingia nao mkataba na kupokea hela bila kujua zinatoka wapi?
 
Lakini mkuu, hii kitu haijawa - signed, sio umeingizwa chaka?
Well,

Barua haiko signed basi ni CHAKA... Umeangalia tarehe za registration ya Kagoda na ukaangalia makubaliano ya mkopo toka Kagoda kwenda Quality Finance? Do you see my concern? Wala mi sina shida na yeye kupinga, ana haki na si vema kuchafuliwa kama anajua yeye ni msafi. Tatizo langu ni ninapoangalia hizi TAREHE mkuu wangu
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom