Manispaa ya Moshi ni takataka kabisa 🚮

Baada ya kuishi Moshi kwa miaka kadhaa nimegundua wachagga wanapenda sifa kama wahaya
 
Kahawa ilijenga mahosipitali, shule za kata, vyuo vikuu, barabara za lami, majengo ya kibiashara, ajira kwa karibia kila mtu aliyeweza kufanya kazi, na kuongeza mzunguko kwenye biashara nyingine. Lakini Mkapa kwa kisasi cha upinzani alioupata kaskazini akafanya aliyoyafanya.
 
kuna wanaosema walaumiwe wachaga wameutekeleza mji wao.

Sogea Moshi pazuri bwashee tupige mbili tatu
 

Siasa zimedidimiza mkoa wa Kilimanjaro kuanzia mwaka 2000 mkoa uliduma sana mpaka sasa.
 
Hakuna JIJI la watu Laki na NUSU na Viamba.

Hakuna jiji lenye ukubwa kama shamba la Msukuma.

Huwezi kuwa jiji kwa mapato ya kuunga unga.

Mwisho wa siku, likiwa Jiji unapata nini, kum-massage ego yako, ukiwa umelewa Kiwingu au???
 
Sasa kwanini matajiri wa kichaga wasiwekeze nguvu kwenye kukuza shughuli za kiuchumi kwenye mkoa wao badala ya kuwekeza fedha nyingi ugenini?
 
Siasa zimedidimiza mkoa wa Kilimanjaro kuanzia mwaka 2000 mkoa uliduma sana mpaka sasa.
Hayo ni mapito ya ukuwaji wa Moshi ambao tangu miaka ya 1700 umekuwa ukipanda na kushuka kama roller coaster. Kuna vitu/watu wanaopandisha na kushusha maendeleo ya kaskazini na hiyo cycle hujirudia tangu zamani hata baadae.
 

Hii nchi ni ya kifala sana, unaua ushirika na viwanda, unabinafsisha! Shule karibu zote za Kilimanjaro zimejengwa na Ushirika (Cooperative unions), hakuna asiejua kuhusu mchango wa Kilimanjaro Native Cooperative Unions (KNCU) na Kilimajaro Native Planters Association, katika kujenga mashule, kutoa udhamini wa masomo, vituo vua afya na ustawi wa biashara na jamii.

Akina Reginald Mengi walisomeshwa nje na huu ushirika. Baadae Mkapa aka adopt sera ya kubinafsisha viwanda, kuua ushirika na kuleta soko huria. Leo tunalalamika ajira hakuna wakati waliua viwanda na ushirika kwa sera ya ubinafsishaji mashirika na viwanda.
 
Hayo ni mapito ya ukuwaji wa Moshi ambao tangu miaka ya 1700 umekuwa ukipanda na kushuka kama roller coaster. Kuna vitu/watu wanaopandisha na kushusha maendeleo ya kaskazini na hiyo cycle hujirudia tangu zamani hata baadae.
Hili nakataa...

Ila ukisema kuna watu wanajitahidi mikoa ya bara isiizidi au kuikaribia Dar takuelewa...

Kwanza angalau nyinyi Arusha inajengwa, umewahi kufika Mbeya?
 
Vyuo vikuu vipi?
Unaweza kuvitaja kwa majina?
 
Umekumbusha kuuwawa kwa viwanda vya umma zoezi lililofanywa kikamilifu nchi nzima. Maelfu ya watu wanahangaika kwa kukoseshwa ajira viwandani lakini viongozi hawajali sababu wao na uzao wao wejimilikisha ajira serikalini na wanazilinda hata kwa damu za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…