Hii nchi ni ya kifala sana, unaua ushirika na viwanda, unabinafsisha! Shule karibu zote za Kilimanjaro zimejengwa na Ushirika (Cooperative unions), hakuna asiejua kuhusu mchango wa Kilimanjaro Native Cooperative Unions (KNCU) na Kilimajaro Native Planters Association, katika kujenga mashule, kutoa udhamini wa masomo, vituo vua afya na ustawi wa biashara na jamii.
Akina Reginald Mengi walisomeshwa nje na huu ushirika. Baadae Mkapa aka adopt sera ya kubinafsisha viwanda, kuua ushirika na kuleta soko huria. Leo tunalalamika ajira hakuna wakati waliua viwanda na ushirika kwa sera ya ubinafsishaji mashirika na viwanda.