Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Siyo Mangula tu, Hadi Mzee Mwinyi, Mzee Warioba, JK akistaafu, Majaji na Mawaziri karibu wote wako jimbo la Kawe kwa hiyo asione tatizo na amheshimu mbunge wake.

hilo ndio la Msingi
na sio kutengeneza propaganda ambazo zinaweza kumwathiri hata yule raia wa kawaida kisa ni itikadi za vyama fulani, na kusahau maendeleo ya jimbo husika.
 
Aende aka kae Njombe. Kwanza mwongo alitudanganya kuwa ndani ya miezi 6 atakuwa amewatimua viongozi wote walioingia madarakani CCM kwa rushwa. Badala ya kufanya kazi aliyoahidi akaenda kuoa na kwenda fungate akajidai eti kuongeza miezi 6 mingine. Sasa new wife akijifungua ataongeza mwaka mbele. Kashindwa kazi. Hakuwaza vizuri. Utatoboaje mtumbwi uliokubeba majini hata kama ni mbaya?! Unaotaka kuwatoa ndio waliokupa kura asilimia mia bila kujua kuwa walikuwa wanakumaliza makali lakini wewe bila kujua ukachekelea ukifikiri wamekukomboa toka kilimo cha nyanya! Muulize JK alikoishia na watu wake wa EPA na orodha ya wauza unga atakwambia ugumu wa kuwashughulikia waliokubeba! Muulize Nape pia spidi yake ya kuwang'oa mapacha watatu ilikoishia. Alipoona mfupa mgumu akahamia kwenye mahubiri ya ukabila, ukanda na udini. Muulize Mukama alikoishia kutokana na kesi ya mapacha watatu. Mangula, Silence speaks louder than voice!
 
Ungefanya utafiti kidogo ungejua kuwa jimbo la kawe halitakuwa chini ya chadema tena kwa sasa mdee kachuja sana hana uwezo wa kuutisha hata mkutano wa hadhara akapata watu.

Ha ha ha ha....Unajisumbua mkuu....WAna- Kawe huwaambi kitu kwa Halima Mdeee.....
 
Huenda Nape alikuwa sahihi aliposema Wazee wa CCM wanasubiri kufa...Huyu mzeee kama kufikiri kwake ndo kumefikia hapa basi asubiri kufa tuu..
 
Anajuta kwa kuwa yupo katika jimbo lililo mikononi mwa upinzani au jimbo halitendewi haki kimaendeleo!!?
Kama jibu ni hilo la pili basi ajue wapo wengi wanajuta si katika jimbo hilo bali katika nchi hii!!
 
hilo ndio la Msingi
na sio kutengeneza propaganda ambazo zinaweza kumwathiri hata yule raia wa kawaida kisa ni itikadi za vyama fulani, na kusahau maendeleo ya jimbo husika.


Uko sahihi, kwa mantiki ya huyu mzee inamaana Mbowe, Lipumba na Mbatia wasingizie wanaumwa kisa Rais anataka kuonana nao?? Huyu mzee kapotea.
 
Ni aibu kwa mtu wa nafasi yake kutoa lugha kama hii, inaelekea mfumo dume umemkaa sana, kwa kuwa Halima ni very young lady kwa hiyo hafai kuwa mbunge wake? Yeye anadhani watu wote wale wa jimbo la Kawe walio mchagua hawana akili au hawana hadhi kama yeye? Au anamainisha kwa kuwa Halima ni mbunge wa upinzani CDM? Na kama ni kwakuwa Halima ni mbunge wa upinzani ndio maana maana anaona aibu kuishi Jimbo la Kawe, basi ataona pia aibu kuishi Tanzania iwapo TZ itachukuliwa na vyama vya upinza, kwa hiyo ajifanye anaumwa chama chake kimpleke huko nje akatibiwe mpaka afie huko huko. Aache unyanyapaa kwa viongizi akina dada, wawe wa upinzani au wa chama chake.
 
Hivi hawa MaCCM wana nini kichwani zaidi ya makam.a.s.i pekee? Kwanini hawaishi kuropoka kila uchao? Kama kibano cha mageuzi kimezidi ni bora wasalimishe linchi letu tulitibie mijeraha walotia. Pambaaaf!!!!
 
Ajiandae kisaikolojia make 2015 atatakiwa kuwa ndani ya Tz inayoongozwa na CDM ...huyu msee bwana ama sivyo ahamie China
 
Ni ufinyu wa fikra alionao, kama anakili ahame hilo jimbo arudi kwao

Na jana amedanganywa na mwenyekiti wa wilaya mambo mengi sana tunamshauri mangula kwa uzoefu wake kama kweli alikua kwenye study tour alitakiwa kuwasikiliza wanachama wake kama mbunge wao pekee alivyosema watu wamenyimwa nafasi za kusema kwaio mengi yamejificha yani wanazidi kujimaliza hiki chama bwana kinafurahisha kweli jinsi kinavyofanya wanachama wake mandondo
na jana kumetokea mpasuko mkubwa sana mangula rudi tena kinondoni la sivyo chama kinakufa pale mmemweka msemaji yule anaongea sana utendaji kidogo mnaliwa nyie
 
Huyu jamaa c ndiye nilikuwa namuona akilima kwenye shamba lake kule njombe!! ameshakuwa mwenyeji wa mjini hadi anaanza kusahau alipotoka?
 
Mangula kaa hapo uvute 'pension' yako ya mwisho mwisho achana na mengine watu tunakuheshimu Mzee. Hivi hajioni kuwa amekumbukwa kibahati tu katika hii duru ya pili. Labda tumkumbushe tu ile misheni yako baada ya kuteuliwa ya kuwa utachunguza na hatimaye kuwafukuza wote waliongia kwenye madaraka kwa rushwa imeishia wapi?

Hivi hajionei aibu na huruma yeye mwenyewe kwanza kwa kuwa kwenye chama ambacho kimesha mcheza shere baada ya kufanywa 'muhanga' wa ajali mbaya ya kisiasa? CCM imesha mchezea sana kisaikolojia na hatimaye kumrudisha tena kwa staili ya 'kejeli' baada ya kuona shida zimemjaa na hana ubavu wa kusema "No Sir". Yambidi ajionee aibu yeye mwenyewe kwanza kwa kupandikizwa kama 'Makamu Mwenyekiti' jina tu ndani ya Chama chake.
 
Ungefanya utafiti kidogo ungejua kuwa jimbo la kawe halitakuwa chini ya chadema tena kwa sasa mdee kachuja sana hana uwezo wa kuutisha hata mkutano wa hadhara akapata watu.

Kujaza watu kwenye mkutano ndo kupata wapiga kura?
 
Back
Top Bottom