Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Mangula kumbuka ulikotoka,Mdee kachaguliwa na wananchi wewe umeteuliwa na kazi uliyopangiwa umeishindwa hivyo 2015 inakula kwako,kucha vya mwisho na kama ulikuwa haujajenga Dar ujenge isije kufika 2015 ukarudi tena kijijini.changamka
 
Kwa sasa kijana yeyote ambaye hataki kuitikia wito anaweza kusingizia kuumwa na ku "Mang'ula" wito huo.
 
Mzee asituhamishe kwenye ajenda kwa kutuletea siasa nyepesi. Kiongozi makini ni yule anayetimiza ahadi zake na ikishindiiana anaachia ngazi. Mzee mara baada ya kuteuliwa aliahidi kwamba ndani ya miezi sita atahakikisha wale wote waliopata uongozi kwa kutumia rushwa anawaondoa. Kwamba viongozi wengi wa CCM waliwahonga wapiga kura ili kupata madaraka siyo issue kwa sababu hata mwenyekiti wa chama kitaifa alilalamikia tatizo la rushwa kukithiri kwenye chaguzi za chama. Mpaka leo mzee kimya. Chezea fisadi weye, taanngamia mwenyewe. Mzee kula hela yako pole pole, Tanzania ya leo huiwezi imekamatwa na MAFISADI.
 
anaona aibu maendeleo anayofanya mama mdee afu sisem walikuwa makopo tu
 
Mzee mangula siulikuwa mkulima wew njombe hapo!?kweli madaraka matamu hadi nyanya umesahau kulima,komaa na mdee huyo mzee wng
 
Mwacheni Halima wetu kama yeye hatakuja kwenye kikao cha wazee wa Kawe sisi wengine tutamwakilisha. Kijana mchapa kazi kawaumbua vigogo wanapora ardhi sehemu zisizoruhusiwa!
 
Siyo Mangula tu, Hadi Mzee Mwinyi, Mzee Warioba, JK akistaafu, Majaji na Mawaziri karibu wote wako jimbo la Kawe kwa hiyo asione tatizo na amheshimu mbunge wake.
 
Nadhani point yake ipo kwenye jinsia zaidi kuliko upinzani.

Anasumbuliwa na uzee na ubongo umekuwa senile. Poor guy. Huyu ana chuki na wapinzani. Hata way back 2005 alikuwa anashabikia ule wimbo wa msinziaji bungeni wa kuwachinja wapinzani lakini rais mteule akamkataza na kumwambia siyo CCM peke yake waliokuwa wamempa ushindi wa 80%.
 
Ungefanya utafiti kidogo ungejua kuwa jimbo la kawe halitakuwa chini ya chadema tena kwa sasa mdee kachuja sana hana uwezo wa kuutisha hata mkutano wa hadhara akapata watu.
Sidhani kama itawezekana CCM kuirudisha Kawe kutoka CHADEMA.

Swali kuu ni kwamba, Nini Halima Mdee na CHADEMA waliwafanyia wananchi wa Kawe kabla ya uchaguzi wa 2010 mpaka wakalichukua jimbo la Kawe kirahisi na Nini CCM tunawafanyia wananchi wa Kawe sasa mpaka 2015 watuamini na kurudisha jimbo la Kawe CCM?
 
Kumbe kuna wazee wengine wakizeeka badala ya busara kuzidi wao 'zinarudi' nyuma kwa kasi hivyo? Ama kweli CCM kazi ipo!
 
Ni dhahiri MaCCM wengi wanadanganyana sana kwa ripoti za uwongo wanazopeana huko Lumumba kwamba watamtoa Mdee pale Kawe!Jimbo la Kawe ni miongoni mwa Majimbo yanayokaliwa na Wasomi,Watu wenye kipato cha juu na waliotembea sana Duniani.Ufahamu wao ni mkubwa sana na kuwaingia hawa watu unapaswa kuwa na hoja nzito zenye ushawishi wa hali ya juu.Wengi wa watu hawa wanamkubali sana Mdee.Uncle wangu ni miongoni mwa watu hao,Yeye ni msomi mzuri sana,Amezunguka Nchi nyingi sana,Ameishi nje ya Nchi kwa zaidi ya miaka 16,Amefanya kazi na Serikali za Nchi za Nje ka muda mrefu kama Mshauri wa mambo ya Afya na sasa anafanya kazi katika Shirika moja hapa Jijini Dar lililo chini ya Tajiri Mkubwa kabisa Nchini Marekani Bw Bill Gates kama Boss wa hilo Shirika,Huyu ni mwanaCCM damu lakini anamkubali sana Mdee.Tabia za hawa Wasomi ni kwamba hawapendi kujishirikisha sana katika mambo ya siasa lakini wakati wa kupiga kura huwa hawakosekani na wanamjua ni nani wa kumpa kura kwasababu hawa maamuzi yao hutokana na utafiti wanaofanya
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,” alisema.

Maswali yangu kwake ni haya:
-WanaCCM pekee wa jimbo la Kawe wanatosha kulirudisha jimbo CCM ktk sanduku la kura?
-Kwanini awe mwongo asisngizie kuumwa,kwani hana demokrasia ya kukataa kwenda kwenye kikao?

-Kinachomsababisha ajute ni kipi?

Alisema "NITAKISAFISHA....NDANI YA MIEZI SITA KUANZIA SASA" Kumbe ni biti ya santuli kama kawa..?
 
Anaangaika na Halima wa nn? yeye ange base zaidi ktk maendeleo ya jimbo la kawe halafu alinganishe na majimbo mengine, lkn kumchukia mtu kwa sababu ya jinsia yake au chama chake bado ni mambo ya kizamani sana,
 
masikini mzee wa watu ! Sasa 2015 atakaa wapi ? Maana cdm inakwenda kuteketeza dar yote !
 
Kumbe kuna wazee wengine wakizeeka badala ya busara kuzidi wao 'zinarudi' nyuma kwa kasi hivyo? Ama kweli CCM kazi ipo!

Huwaoni akina Wasira ambO wakati watu wanawaza katiba mpya yeye anawaza chai na juice? Siyo kila mzee amejaliwa busara.
 
kwani alilazimishwa kuishi jimbo la Mh. huyo wa Chama pinzani.

hili ni janga yaani hatashindwa kuudhulia vikao vya maendeleo ya jimbo la KAWE, kisa lipo chini ya mbunge wa upinzani.
mi nilidhani angeweza kuwa ni mmoja ya waleta changamoto kama mkazi, au mmoja wa wakubwa wa kuendelea kuinua maendeleo ya jimbo hilo.
shida ya itikadi ya chama kimaoja....
 
Mangula anajivunga tu anajua ccm jinsi alivyo ya kinyang'au alivyomfanyia chini ya JK
 
Back
Top Bottom