Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Too late, Mzee Mangula. Tena afadhali mara 100 Edo akawa ndani ya chama kuliko awe nje.
 
Lakini kwanini nyinyi wanaCDM mnafurahia sana migogoro ndani ya chama chetu tawala? Hamjui CCM si CDM? Na CCM ikiyumba na nchi lazima itayumba! Mkionaga simba wanararuana kaeni mbali kama hamtafuti kuchafuka damu!

Kwahiyo CCM ikiondoka madarakani hakutakuwa na serikali ya TZ? Div five zimeshajaa Mulugo anzisha six
 
ccm banah,, shabikieni na hili sasa ukoo wa panya nyie kazi yenu kugombnia mali zetu

Mkuu hawa jamaa na lichama lao lote kwa Lowasa wanafyata mkia na kumwachia nape ndo apambane.
Ni hivi unamchukua kaumbwa chako alafu unasakisia akamate Tembo!
Hayo mbona ni Sunura jamaniiiii
 
Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

-------------------------

Mangula hayupo serious, maana angekuwa serious angejua namna Lowasa alivyokivuruga chama na serikali so far. Kama hajui pa kuanzia kuhusu Lowasa amuulize Mzee Fredrick Sumaye
 
Acha ccm waendelee kupangaranyika wakati sisi tukiendelea ku scan virus.!!
 
Ndudu wana Jf,

Matamko mawili ya vioungozi wa juu wa CCM Nape na Mangula, yameenda kinyume na campaign ambazo wanaCCM hapa Jf wamekuwa wakipiga kuhusu Democrasia ndani ya vyama huku wakiinanga Chadema kuwa inamnyima Zitto Kabwe Demicrasia ndani ya Chama. Je anachokifanya Lowassa sicho ambacho Zitto amekemewa na kuchukuliwa hatua ndani ya Chama chake Chadema? Kama ni jambo la Kidemocrasia kwanini Nape na Mangula wamemjia juu Lowassa? Vijana wa CCM acheni unafiki, vyama lazima viendeshwe kwa kanuni na taratibu, otherwise itakuwa ni vurungu za kilabu cha pombe za kienyeji.

CC:
Ritz, MSALANI, Lizaboni etc

Hakuna mahali lowasa anafanana na zitto. Tumia kichwa kufikiri
 
Wazee wengine sijui vip.. yaani bila aibu eti anatoka mbele za watu kukemea harambee na michango mbalimbali ya viongozi wa chama eti ni rushwa na watachukuliwa hatua... Lowassa anasaidia sana chama kujijenga na kujitangaza mana bila harambee zake sijui ccm wangekuwa wapi??? na wakina Nape Nnauye umaarufu wangeutoa wapi.. Lowassa anasaidia sana hata Mangula kuonekana channel ten ni kwa ajili yake, isingekuwa Lowassa angeongea nini sasa!!!

Lowassa anafanya kazi za viongozi wa chama ila kwa chuki watu wanapiga majungu, kama nao wanaweza wafanye nao harambee basi tuone kama watapata watu, in short ndo kichwa ndani ya ccm kwa sasa, waondoke wote ccm itabaki ila akiondoka yeye ndo mwisho wa chama..

CCM wawe na shukrani, Lowassa anawasaidia sana kina Mangula..

Kweli mkuu mtu anaitwa kwenye harambee ambazo zinasaidia miradi ambayo ilibidi afanywe na serikali ya CCM,bado anaonekana mbaya,kaza buti Lowasa tutokomeze umasikini kama Mungu anataka uwe rais utakuwa tu,kila mtu ana dhambi dawa yake ni kutubu tu.
 
Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

-------------------------
Jamani Huyu Mangula si ndiye aliyepeleka File Kubwa Eti lenye Madhambi na KUMUUA Kikwete 2005, ILI Kikwete asipitishwe kugombea Urais. Mzee Huyu mlima nyanya Kweli ni mtu aw Chuki. HAKOMI. NAPE naye Huyu ni CCJ yupo pale kwa Hisani ya Marehemu baba yake. HATA na Akina CCJ wakiongozwa na mzee SIX nao Wana ROPOKENI hovyo.
 
Jamani Lowasa ana haki ya kutangaza nia na isitoshe si mpaka apitie ccm kwan ccm nan? ndiye anayegawa urais? MIUNGU-WATU
 
Huyu mzee anamdanganya nani? Miezi sita alotoaga kwa watoa rushwa bado? ATULIZANE TU
 
Tukiachilia mbali ushabiki, Huyu Lowasa afai ata kupangisha mitaa karibu na magongoni.

Huyu jamaa kwa anayeishi Arusha atakubaliana na mimi kuwa amewateka matajiri karibu wote wa Arusha na kuzitumia pesa zao katika harakati zake za kuusaka uraisi.

Mathias Manga mmiliki wa jengo la gorofa 13 lililopo sakina darajani ni mmoja wa matajiri ambae Lowasa anatumia pesa zake katika kuusaka uraisi, na kwasasa huyu tajiri amesimamisha ujenzi wa gorofa lake ambalo lilikuwa likamilike january 2014 na kuzielekeza mabilioni yake katika kuipa nguvu harakati za Lowasa.

Sasa cha kujiuliza ni nani atakae walipa hao mabilionea pesa zao?
 
mimi napata shida sana kufaham kwanini hawa watu (CCM) wanamuogopa huyu jamaa (Lowassa) kiasi cha kujipanga kujibu mapigo kwa nguvu zote wakati mmoja? nachelea kusema "mti upigwao mawe ndio wenye matunda", maana haiwezekani wawe "upset" nae kiasi hicho as if he is the only one doing those sort of stuffs. hiki chama kimechafuka almost every one is dirty.
 
Waache kutuchanganya kwani mpaka leo mzee hajui kuwa ukitaka kugombea ccm nafasi yoyote kigezo kikubwa ni UGAWAJI FEDHA YANI RUSHWA
 
Tukiachilia mbali ushabiki, Huyu Lowasa afai ata kupangisha mitaa karibu na magongoni.y

Huyu jamaa kwa anayeishi Arusha atakubaliana na mimi kuwa amewateka matajiri karibu wote wa Arusha na kuzitumia pesa zao katika harakati zake za kuusaka uraisi.

Mathias Manga mmiliki wa jengo la gorofa 13 lililopo sakina darajani ni mmoja wa matajiri ambae Lowasa anatumia pesa zake katika kuusaka uraisi, na kwasasa huyu tajiri amesimamisha ujenzi wa gorofa lake ambalo lilikuwa likamilike january 2014 na kuzielekeza mabilioni yake katika kuipa nguvu harakati za Lowasa.

Sasa cha kujiuliza ni nani atakae walipa hao mabilionea pesa zao?
Like jengo limesimamishwa kwa sababu limejengwa kimakosa pale ni sehemu ya mto na alitumia pesa kupata kibali kujenga eneo ambalo alistahili kabisa itakuwa madiwani wa Chadema wamelizuia.
 
Back
Top Bottom